Namtafuta baba yangu mzazi

Namtafuta baba yangu mzazi

Hivi unamtafutaje mtu ambaye alikukimbia au kutekekeza kisa baba? Yaani ni kwa kuwa tu sikuwahi kuzaa nje ila kama ningekuwa nimetelekeza mtoto ukweli asinitafute maana sistahili kuitwa baba na mtoto ambaye sikumjali wala kumpenda. Wanaume tujikague maana jehanamu ni yetu.
Hakunitelekeza wala hakunikimbia. Ni mazingira ya kimaisha yalilaazimu hivo na shid ya mawasiliano kwa kipindi hiko
 
Habari za leo wana jukwaa.

Ninaitwa Neema. Namtafuta baba yangu niliyepotezana nae miaka ya 90 kwa kifupi sijawahi kumuona. Mama aliniambia jina moja anaitwa Shafuri ni mpare wa wilaya ya Same kijiji ni Gonja-Maore.

Kipindi hicho walikua wanaishi Gongo la Mboto walikua majirani. Yeye baba alikua anaishi kwa kaka yake aliyeitwa Mr Mbwambo (alikua anafanya kazi tazara) na mkewe alijulikana kwa jina la mama Nasemba. Mama yeye alikua anaishi kwenye nyumba hiyo hiyo mabanda ya nje.

Walipotezana baada ya mama na familia yake kuhama sehemu hiyo na kuhamia sehemu nyingine na baade akahama mkoa. Hadi leo hawana mawasiliano na mimi nilipewa jina la baba mwingine.

Kwa yeyote atakaeweza kunisaidia awasiliane na mimi kupitia namba 0772719646.

Alikua anafanya biashara ndogondogo

Nahitaji kumfahamu
Mkuu mm nina mashemeji yanyu anatokea kwenye familia ya akina shafuri ila sijajua kama itakuwa ndio hao
 
Hivi unamtafutaje mtu ambaye alikukimbia au kutekekeza kisa baba? Yaani ni kwa kuwa tu sikuwahi kuzaa nje ila kama ningekuwa nimetelekeza mtoto ukweli asinitafute maana sistahili kuitwa baba na mtoto ambaye sikumjali wala kumpenda. Wanaume tujikague maana jehanamu ni yetu.

Ndo maana tunasema ukioa singo mama usijisahau tu, mtoto akikua ni lazima amtafute baba’ke.

Unaona hapo keshalaumu kupewa jina la baba wa kambo, ambaye kimsingi ndo mlezi wake.!
 
Bora ata wewe umemtafuta baba mzazi, Mung atakusaidia utampata si inasemekan Kuna dada yetu kazaliwa nje na ndo mkubwa familia tumemtafuta katutoa shit et kisa specialist. Katuoana mafala flan hiv na wakati kwetu hamna njaa kali
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]njaa kali
 
Sipati picha na nie nitakavyotafutwa baada ya miaka 20 ijayo na wanangu niliowaacha Mwanza (1), Morogoro (1) na Kigoma (1).

Mimi sina tatizo ila mama zao ndio wananinyima wanangu kisa eti nimewazalisha pasipo kuwaoa [emoji57]
Lakn Huduma s unatoa kwa watoto?
 
Sipati picha na nie nitakavyotafutwa baada ya miaka 20 ijayo na wanangu niliowaacha Mwanza (1), Morogoro (1) na Kigoma (1).

Mimi sina tatizo ila mama zao ndio wananinyima wanangu kisa eti nimewazalisha pasipo kuwaoa 😏
Hudumia watoto wako mkuu kwa utaratibu sahihi. Ila pia usiwe unazaa watoto bila kuwa na mpango na mama zao hili liko ndani ya uwezo wako
 
Hakunitelekeza wala hakunikimbia. Ni mazingira ya kimaisha yalilaazimu hivo na shid ya mawasiliano kwa kipindi hiko
Mhhh....au Kuna kitu kimetokea huko kwa baba wa Jambo!Mwanaume anayejiamini hawezi telekeza mtoto
 
Ndo maana tunasema ukioa singo mama usijisahau tu, mtoto akikua ni lazima amtafute baba’ke.

Unaona hapo keshalaumu kupewa jina la baba wa kambo, ambaye kimsingi ndo mlezi wake.!
Kuna sehemu umeona kuna lawama?
 
Kuna sehemu umeona kuna lawama?

Umepewa jina la baba mwingine!

Mama’ko anajua jina la baba’ko, na kijiji chao anakijua... ni taarifa za kutosha kuanza nazo.

Kama kuna namna yoyote mama hakupi ushirikiano basi ujue ipo sababu, na ukute ni kweli baba hajulikani.

Ni haki yako kumjua baba na ukoo wako, kama kweli una nia thabiti... mtumie mama angali hai.
 
Habari za leo wana jukwaa.

Ninaitwa Neema. Namtafuta baba yangu niliyepotezana nae miaka ya 90 kwa kifupi sijawahi kumuona. Mama aliniambia jina moja anaitwa Shafuri ni mpare wa wilaya ya Same kijiji ni Gonja-Maore.

Kipindi hicho walikua wanaishi Gongo la Mboto walikua majirani. Yeye baba alikua anaishi kwa kaka yake aliyeitwa Mr Mbwambo (alikua anafanya kazi tazara) na mkewe alijulikana kwa jina la mama Nasemba. Mama yeye alikua anaishi kwenye nyumba hiyo hiyo mabanda ya nje.

Walipotezana baada ya mama na familia yake kuhama sehemu hiyo na kuhamia sehemu nyingine na baade akahama mkoa. Hadi leo hawana mawasiliano na mimi nilipewa jina la baba mwingine.

Kwa yeyote atakaeweza kunisaidia awasiliane na mimi kupitia namba 0772719646.

Alikua anafanya biashara ndogondogo

Nahitaji kumfahamu
NAOMBA NIKUULIZE MASWALI YAFUATAYO .......

1.NI KWANINI UMEAMUA KUMTAFUTA BABA YAKO MZAZI KIPINDI HICHI TANGIA MIAKA YOTE ULIKUWA WAPI ?????

2.MUULIZE MAMA YAKO AKUELEZE NI SABABU IPI ILIYOPELEKEA YEYE NA BABA YAKO WAKATENGANA KIPINDI KILE TATIZO LILIKUWA NI NINI

3.MUULIZE MAMA YAKO KWANINI ALISHIDWA KUYASIMAMIA MAHUSIANO YAKE NA BABA YAKO YAVUNJIKE

4.MIAKA YOTE UNAISHI MAMA YAKO UKIWA MDOGO ULISHAWAHI KUMUULIZA MAMA BABA YANGU YUKO WAPI AU ALIKUWA ANAKUFICHA

5.MWISHO KABISA BAADA YA KUMFAHAMU BABA YAKO UNA MALENGO GANI NA YEYE ????
 
Halafu nimekuja kugundua watoto wa kike ndio huwa na hiki kichaa cha kutafuta baba zao walowatelekeza.

Wanaume huwa mnajisifia ujinga kuzaa na kutelekeza, ona sasa mnavyotesa watoto. Mkishajiona mafurushi hebu bakini na mbegu zenu, msizitapanye hivi mnatesa watoto wasio na hatia kwa ujinga wenu.
 
Poleni sana. Mkuu! Sister mkubwa hajitambui! Sa nyie mna kosa gani? Hamuhusiku na yeye kuzaliwa Nje
Bora hata wewe umemtafuta baba mzazi, Mungu atakusaidia utampata si inasemekan Kuna dada yetu kazaliwa nje na ndo mkubwa familia tumemtafuta katutoa shit et kisa specialist. Katuoana mafala flan hiv na wakati kwetu hamna njaa kali
 
Alikua anafanya kazi miaka hiyo ya 90 mwanzoni na mm siishi dar kwa miaka 27 sasa na sijawahi fika nampatia wapi?

Acha kuwa kichwa ngumu unaanzia Tazara ofisini taarifa za wastaafu na makwao zipo na walipojenga, na unadhani hata Kama alistaafu hamna watumishi aliowaacha ambao hawajastaafu?unamaelezo mazuri hadi ya mkewe na kijijini Gonja uneshindwa kwenda hata upareni, hata huyo Mbwambo ukifika upareni watakupa mawasiliano yake, Acha kupenda ubwete kila kitu unacho
 
Mm Msure alintelekeza na baadae alintafuta mwenyewe (of coz alishajua nimetoboa)! Nakampokea nikijua yake atamalizana na Mungu wake na after all na Mm Maza alishafariki!

Ya Mungu mengi... kumbe Mzee alintafuta akiwa ktk kipindi chake cha mwisho mwisho cha safari yake Duniani. Uhusiano wetu mpya na Mzee haukumaliza 5yrs akafariki!

Huko alikopoteleaga alipata watoto wa kike wawili.... Naenda nao sawa.
 
Kulikuwa kuna kipindi cha searchline cha RFA...kilikuwa msaada mkubwa sana.

Sijui kama bado kipo.
 
Halafu nimekuja kugundua watoto wa kike ndio huwa na hiki kichaa cha kutafuta baba zao walowatelekeza.

Wanaume huwa mnajisifia ujinga kuzaa na kutelekeza, ona sasa mnavyotesa watoto. Mkishajiona mafurushi hebu bakini na mbegu zenu, msizitapanye hivi mnatesa watoto wasio na hatia kwa ujinga wenu.
Umeandika utopolo gani na wewe?embu msome vizuri mleta mada hakuna sehemu amesema babaake alimkataa.
 
Lakn Huduma s unatoa kwa watoto?


Nimejaribu kwa kila namna kujiweka karibu na kutaka kuendelea kuhudumia mtoto ila inashindikana.

Huyu mdada tuliishi wote kwa takrivani miaka miwili, tukashindwana tabia na tukaachana. Alitoka hapa kwangu kurudi kwao akiwa na mimba yangu ya miezi mitano.

Niliendelea kumhudumia mpaka alipojifungua mtoto wa Kike (Viva/Lulu), nikamhudumia pia yeye na mtoto kwa zaidi ya miezi 6, likaja kuzuka la kuzuka mwanamke akawa mwongo balaa yaani anadanganya kuwa mtoto anaumwa figo na ameshauriwa apelekwe Muhimbili wakati huo anasema wanatibiwa St Francis Ifakara mie nipo zangu Swanga.
Nikawa natuma tu hela za matibabu kumbe mtoto wala hata haumwi ila anatumia kigezo cha ugonjwa ili kunipiga pesa. Nikaja kugundua ukweli wote

Baada ya hapo nikachukua maamuzi ya kumwacha jumla na nikaoa na kufunga ndoa na mwanamke mwingine.
 

Attachments

  • 20200712_113122.jpg
    20200712_113122.jpg
    29.4 KB · Views: 20
  • 20200712_113032.jpg
    20200712_113032.jpg
    56.6 KB · Views: 21
  • 20200712_114927.jpg
    20200712_114927.jpg
    49 KB · Views: 19

Similar Discussions

Back
Top Bottom