Namtafuta baba yangu Gervas Kalilo

Namtafuta baba yangu Gervas Kalilo

Achana naye hakupendi, angekuwa anajali kuhusu wewe lazima angekutafuta au angejulisha familia yake kuwa kuna sehemu aliacha mtoto…!!
 
Habari za wakati huu wapendwa, mimi naitwa PENDO GERVAS KALILO. Nilizaliwa mwezi Septemba mwaka 1993, Kahama. Kwa sasa ninamtafuta baba yangu mzazi ambaye anaitwa GERVAS KALILO. Sijawahi kumuona baba yangu, na jina lake nililiona kwenye kadi yangu ya kliniki likiwa na majina hayo mawili tu.

Mama yangu aliitwa KHADIJA OMARY KABONA, mwenyeji wa Masumbwe. Kwa maelezo niliyopewa na bibi yangu, mama alitoka Masumbwe na kwenda Kahama kufanya kazi za ndani. Akiwa huko alipata ujauzito. Inasemekana baba yangu alikuwa mfanyakazi wa dukani, wakati mama yangu alikuwa akifanya kazi za ndani.

Mama alipofikia kipindi cha kujifungua, alishindwa kujifungua kawaida na alifanikiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji. Bibi yangu hakuwa na taarifa kuhusu hali hiyo. Boss wa mama yangu alisafiri hadi Masumbwe kwa teksi kumjulisha bibi kwamba mwanawe amejifungua mtoto wa kike, lakini amejifungua kwa upasuaji, hivyo alihitaji kwenda kumuuguza.

Bibi yangu, pamoja na mtoto wa kaka yake aitwaye ELIZA, walipanda teksi pamoja na huyo boss wa mama na kwenda Kahama. Walipofika Kahama, bibi alikaa kwa muda, kisha akarudi Masumbwe. Mimi na mama yangu tuliendelea kubaki kwa boss wake mama, ambaye inasemekana aliishi katika eneo la Uhindini.

Baadaye, mama yangu aliwahi kusafiri kwenda Singida kwa kaka yake na alikaa huko kwa miaka kadhaa. Aliporudi Kahama, alifika tena kwa yuleyule boss wake wa zamani. Mama yangu alifariki mwaka 1999.

Kwa sasa nimeamua kumtafuta baba yangu. Bibi yangu ana umri mkubwa na kuna mambo mengi hayakumbuki vizuri, hivyo ninapojaribu kumuuliza siwezi kupata maelezo ya kutosha kuhusu baba yangu.

Baba, kama bado uko hai, natamani sana siku moja nikuone. Natamani pia kukufahamu wewe ni nani, maisha yako yalikuwaje, na kama una familia nyingine ningependa pia kuwafahamu.

Sina nia nyingine yoyote zaidi ya kutafuta ukweli wa nilikotoka na kumfahamu baba yangu mzazi. Kama kuna mtu yeyote anayemfahamu GERVAS KALILO, aliyewahi kuishi au kufanya kazi Kahama, hasa katika eneo la Uhindini, au ana taarifa yoyote inayoweza kunisaidia kumpata, naomba anisaidie kwa kunipa taarifa.

Asanteni sana kwa msaada wenu. Mungu awabariki. 🙏

kwa yeyote mwenye taarifa za uhakika ani PM au apige namba hii+255 689 848 090🙏
Duh...historia imeniumiza sana
 
Aisee najiona mimi kabisa miaka ijayo huko mbele,nimeenda mkoa X nimekutana na kibint cha 2000

Tukapima wote tupo clean,nikamwambia mapema sipo tayar kuzaa kwasasa,nilijua sio mkaaji huo mkoa

Kumbe mwenzangu anataka mtoto nami sijui,mwisho wa siku ikawa imo

Na mwenyewe anasema huyo ni binti yake na hata jina kamuandika la kwao

Ingawa alikuwa ana mambo mengi,pamoja na kupima nae lakini bado alikuwa mwingi wa mambo

Ikanibidi kupima tena,maana best yake alipenyezea za chini kuwa hajatulia,kwahiyo hata mtoto nikahisi huenda sip wangu

Ila nikaona siku moja picha yake whatsapp , anafanana na mimi,hata nikamuonyeshq mfanyakazi mwenzangu kutaka maoni yake akasema mzee hili chata lako

Na mwamba mmoja nae mkoa huo huo akasema hapa huruki

Sasa shida itampata huyo binti baadae akija kujitambua,namba ya huyo binti ninayo,siku za awali alikuwa anaomba msaada mdogo mdogo tena mara chache sana,nilimsaidiaga ila baadae nikawa nakuasha lengo nisiweke ukaribu nae tena,huwa naona tu status zake

Sometimes nawaza nimblock tu ingawa hanisumbui kwa lolote now

Namuona binti atakaye kuja kumtafuta Silent King baadae huko,so sad
wewe ni MPUMBAVU
 
Me nakushauri achana nae kwanini yeye hakutafutii wewe ni mkubwa Sasa unapaswa kutulia na mume wako.
By Experience, Watoto wa kike au Wanawake huwa wana uchungu sana na Baba zao, hata akimkuta amechoka sana hatamwacha baba yake au kutomsamehe kisa hakumlea

Ilishamtokea ndugu yangu mmoja wakike huko Mombasa alimtafuta Baba yake sana akaambiwa ni konda wa magari ya kwenda Malawi akamfuatilia mpaka akampata, huyu Dada anafanya kazi na benki moja ya nje hapa Zanzibar na amemjengea Baba yake
 
Pierina Vicka unaifahamu pamba secondary iko mwanza?
Nenda hapo kuna mwalimu kalilo ni mtoto wa mojawapo na kina kalilo walioko kahama ukoo wa Emmanuel kutoka kasiro.
Mtafute mweleze story atakusaidia kivyovyote vile hata kwa kukutanisha na wazazi wake ambao watakusaidia zaidi kama wanafahamu ukweli wowote kuhusu Gervas kalilo.
 
Pierina Vicka unaifahamu pamba secondary iko mwanza?
Nenda hapo kuna mwalimu kalilo ni mtoto wa mojawapo na kina kalilo walioko kahama ukoo wa Emmanuel kutoka kasiro.
Mtafute mweleze story atakusaidia kivyovyote vile hata kwa kukutanisha na wazazi wake ambao watakusaidia zaidi kama wanafahamu ukweli wowote kuhusu Gervas kalilo.
Naifaham hiyo shule lakini hii taarifa nimeopost sehemu nyingi wengekua wahusika wabgenitafuta maana dunia kiganjan otherwise waogope kwa kuhis nataka kitu kutoka kwao kiukweli huyo kalilo nikimpata kama atakua hai dakika 10 za kukaa nae na kumuuliza baadhi ya maswali kadhaa zitatosha kabisa.
Mimi nakuelewa sana na pole kwa majibu mabovu kutoka kwa members wengine. Kujua chimbuko lako ni jambo la faraja na umefanya vizuri sana kutumia social media. Kama kweli baba yako hilo ni jina lake halisi, uwezekano wa kumpata ni mkubwa. Wasiwasi unakuja kama jina lake halisi ndilo hilo hapo kwenye cheti. Kuna watu wengine hutumia majina fake hasa linapokuja suala la msichana ambaye hamjapanga kuoana anaposhika mimba. Je, bibi yako anaweza kukumbuka huyo baba yako alipokeaje habari za ujauzito wa mama yako na kama alitoa ushiriano mara baada ya kujifungua? Ushauri mwingine ni kutembelea eneo (kama unalijua) ambalo huyo mwajiri wa baba yako, mwenye duka alipokuwa anaishi. Na pia jaribu kutafiti jina ''Kalilo'' ni la ukoo au ni jina ambalo liko common sehemu fulaniili ku-narrow down search area yako.
Nahis ni jina FAKE maana kwa jinsi nilivyomtafuta angekua kapatikana kuna muda nahis labda hayupo dunian
 
Pole, natumaini uwapate nduguzo tena wawe angalau na umoja kuna familia zimefanyika kama miguu za pweza ni balaa tupu. Shida utakayopata ni kuwa watu wa kijijini huchangia majina utakuta akina kalilo wengi
 
Pole, natumaini uwapate nduguzo tena wawe angalau na umoja kuna familia zimefanyika kama miguu za pweza ni balaa tupu. Shida utakayopata ni kuwa watu wa kijijini huchangia majina utakuta akina kalilo wengi
Kabisa na kina kalilo ni common tofaut na majina mengine ukisikia tu unaju asili yake
 
Back
Top Bottom