Namtafuta baba yangu Gervas Kalilo

Namtafuta baba yangu Gervas Kalilo

Pole sana kwa changamoto hyo

Ila cha kukushauri nenda facebook kuna ukurasa unaitwa crubTz kule ndo wafanya kazi hii ya kuunganisha familia zilipotezana kwa muda mrefu
Yan ndani ya muda mfupi tangazo lako likipandishwa tu mtu wako atapatikana awe hai au la
Nimepost huko mara kadhaa bila mafanikio hata hiyo namba unayoiona hapo ni ya club tz club nimeweka hiyo kwa sababu nilianzia kwake na yeye ndo atakae nipa taarifa akitafutwa maaa mimi sipo Tanzania kwa wakati huu
 
Pole yake aisee ila mimi sihitaji mali wala chochote ila kumjua tu ndo nia LENGO
Mimi nakuelewa sana na pole kwa majibu mabovu kutoka kwa members wengine. Kujua chimbuko lako ni jambo la faraja na umefanya vizuri sana kutumia social media. Kama kweli baba yako hilo ni jina lake halisi, uwezekano wa kumpata ni mkubwa. Wasiwasi unakuja kama jina lake halisi ndilo hilo hapo kwenye cheti. Kuna watu wengine hutumia majina fake hasa linapokuja suala la msichana ambaye hamjapanga kuoana anaposhika mimba. Je, bibi yako anaweza kukumbuka huyo baba yako alipokeaje habari za ujauzito wa mama yako na kama alitoa ushiriano mara baada ya kujifungua? Ushauri mwingine ni kutembelea eneo (kama unalijua) ambalo huyo mwajiri wa baba yako, mwenye duka alipokuwa anaishi. Na pia jaribu kutafiti jina ''Kalilo'' ni la ukoo au ni jina ambalo liko common sehemu fulaniili ku-narrow down search area yako.
 
Mimi nakuelewa sana na pole kwa majibu mabovu kutoka kwa members wengine. Kujua chimbuko lako ni jambo la faraja na umefanya vizuri sana kutumia social media. Kama kweli baba yako hilo ni jina lake halisi, uwezekano wa kumpata ni mkubwa. Wasiwasi unakuja kama jina lake halisi ndilo hilo hapo kwenye cheti. Kuna watu wengine hutumia majina fake hasa linapokuja suala la msichana ambaye hamjapanga kuoana anaposhika mimba. Je, bibi yako anaweza kukumbuka huyo baba yako alipokeaje habari za ujauzito wa mama yako na kama alitoa ushiriano mara baada ya kujifungua? Ushauri mwingine ni kutembelea eneo (kama unalijua) ambalo huyo mwajiri wa baba yako, mwenye duka alipokuwa anaishi. Na pia jaribu kutafiti jina ''Kalilo'' ni la ukoo au ni jina ambalo liko common sehemu fulaniili ku-narrow
Okay sawa ila uhindini pale sijui ni sehemu gani ila nitajitahidi niende
 
Habari za wakati huu wapendwa, mimi naitwa PENDO GERVAS KALILO. Nilizaliwa mwezi Septemba mwaka 1993, Kahama. Kwa sasa ninamtafuta baba yangu mzazi ambaye anaitwa GERVAS KALILO. Sijawahi kumuona baba yangu, na jina lake nililiona kwenye kadi yangu ya kliniki likiwa na majina hayo mawili tu.

Mama yangu aliitwa KHADIJA OMARY KABONA, mwenyeji wa Masumbwe. Kwa maelezo niliyopewa na bibi yangu, mama alitoka Masumbwe na kwenda Kahama kufanya kazi za ndani. Akiwa huko alipata ujauzito. Inasemekana baba yangu alikuwa mfanyakazi wa dukani, wakati mama yangu alikuwa akifanya kazi za ndani.

Mama alipofikia kipindi cha kujifungua, alishindwa kujifungua kawaida na alifanikiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji. Bibi yangu hakuwa na taarifa kuhusu hali hiyo. Boss wa mama yangu alisafiri hadi Masumbwe kwa teksi kumjulisha bibi kwamba mwanawe amejifungua mtoto wa kike, lakini amejifungua kwa upasuaji, hivyo alihitaji kwenda kumuuguza.

Bibi yangu, pamoja na mtoto wa kaka yake aitwaye ELIZA, walipanda teksi pamoja na huyo boss wa mama na kwenda Kahama. Walipofika Kahama, bibi alikaa kwa muda, kisha akarudi Masumbwe. Mimi na mama yangu tuliendelea kubaki kwa boss wake mama, ambaye inasemekana aliishi katika eneo la Uhindini.

Baadaye, mama yangu aliwahi kusafiri kwenda Singida kwa kaka yake na alikaa huko kwa miaka kadhaa. Aliporudi Kahama, alifika tena kwa yuleyule boss wake wa zamani. Mama yangu alifariki mwaka 1999.

Kwa sasa nimeamua kumtafuta baba yangu. Bibi yangu ana umri mkubwa na kuna mambo mengi hayakumbuki vizuri, hivyo ninapojaribu kumuuliza siwezi kupata maelezo ya kutosha kuhusu baba yangu.

Baba, kama bado uko hai, natamani sana siku moja nikuone. Natamani pia kukufahamu wewe ni nani, maisha yako yalikuwaje, na kama una familia nyingine ningependa pia kuwafahamu.

Sina nia nyingine yoyote zaidi ya kutafuta ukweli wa nilikotoka na kumfahamu baba yangu mzazi. Kama kuna mtu yeyote anayemfahamu GERVAS KALILO, aliyewahi kuishi au kufanya kazi Kahama, hasa katika eneo la Uhindini, au ana taarifa yoyote inayoweza kunisaidia kumpata, naomba anisaidie kwa kunipa taarifa.

Asanteni sana kwa msaada wenu. Mungu awabariki. 🙏

kwa yeyote mwenye taarifa za uhakika ani PM au apige namba hii+255 689 848 090🙏
Naomba nikuulize. Huyo baba yako ana ndugu yake anaitwa Samson Karilo? Huyu Samson Karilo nae ni Mkazi wa Kahama. Kama ni kweli njoo Inbox ukutane na ndugu zako
 
Back
Top Bottom