Namsifu Kikwete kuwekeza katika kujenga uchumi bora wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namsifu Kikwete kuwekeza katika kujenga uchumi bora wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Barubaru, Jul 17, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wanajamii.

  Kama waTanzania hususan wale waliotoka Bara (Tanganyika) msingekuwa watu wa kulalamika na kulaumu kwa kila jambo na kusahau kabisa kuwa wazalendo na kushukuru kwa kile kidogo mnachopata na kujewekezea.Nitakuwa mbadhilifu wa Fadhila kama sikusema kuwa Tz imejitahidi sana kuweka miundo mbunu bora ya kujenga uchumi imara wa Tz.

  Hapo awali nilizungumzia WAANDISHI wa habari wa Tanzania wamekosa uzalendo kwa nchi yao. Napenda kusimamia kwa kauli hii kwani nimeona mengi kwa hizi siku sabaa nilizokaa tanzania.

  Ningependa kuwarudisheni katika Uchumi utaona Sera bora za kukuza uchumi wa nchi yoyote ile na hususan nchi masikini ni kuweka miundo mbinu Bora ya Usafiri kama barabara, Kuwa na nishati ya uhakika na kuwa na Sera bora za uwekezaji ikiwemo pamoja na Amani na utulivu wa sehemu hisika na vivutio natural kwa wawekezaji kama madini, ardhi safi n.k.

  Kwa hayo hapo juu utaona Tanzania hususan Tanganyika wamebarikiwa kila kitu kasoro kulikuwa hakuna miundombinu Bora ya barabara na Nishati ya stima yyenye uhakika.

  Kwa kipindi kifupi sana nimetembelea Mwanza kwa kupita barabara kupitia geita, Buseresere, Bwanga, Chato mpaka Muleba na kukomea kamachumu. Na kurudi nilipitia Biharamulo, Lusaunga, Nyakanazi, Lunzewe, ushirombo mpaka kahama, nzega na kuingia Tabora na baadae kurudi mpaka Mwanza kupitia Nzega, Tinde, shinyanga kufika Mwanza.

  Jana niliingia Mtwara na leo nimetembea mpaka Kilwa kilanje lanje mpaka Ngurukuru kuona Kiwanda cha Rufiji Cement . Hakika Rais Kikwete amejitahidi sana kuweka miundo mbinu bora ya barabara za lami. Takriban lami imetawala kwingi kinachosubiriwa ni upatikanaji wa nishati ya Stima.

  leo ningependa kuwashauri waTz acheni kulalamika Mtwara kuna fursa nyingi sana za uwekezaji. Kwani pamoja na kuwa na Gas na hivyo kuwa na umeme wa uhakika, lakin pia kuna mables ambazo ni malighafi safi kwa utengenezaji wa Saruji, Ardhi ni bora sana kwa kilimo cha alizeti, ufuta, korosho. Vile vile kuna beach nyingi sana na nzuri sana kuanzia msanga mkuu na maeneo yote a mikindani mpaka Lindi.

  Lakin kubwa zaidi ni kuwa kuna Bandari kubwa sana. Kwani i lango kuu l kusafirishia bidhaa na la kupokelea malighafi za viwanda. Nilikuwa nikipitia sera ya Tz kuhusu Mtwara Corridor nimezipenda sana na kuona kuwa kuna mengi sana sio tu ya kujifunza lakin pia kuwekeza.

  Nawashauri wana JF. Mkumbuke kuwa mtaji mkubwa wa kiuchumi ni AKILI ZENU, mengine yote ni matokeo. Acheni kulalamika umaskini wakti fursa zipo nyingi sana zipo kwenu. Kuna mahotel mazuri sana ya kulala vile vile kuna Makonde beach club, maisha Club, safari Lounge na mengine. Vile vile kuna Radio mbili maarufu Pride FM na Safari Radio. Zote hizo zinatoa taswira safi sana kwa mji wa Mtwara. Flight za uhakika nimekuja na 540. lakin hata precission nao wanakuja mara mbili kwa siku.

  Namaliza kwa kumpongeza sana sana Rais Kikwete kwa kuweka na kujenga Msingi mkuu wa kuinua uchumi wenu kwa kutengeneza barabara bora na kuanza project ya kuhakikisha Umeme unakuwa wa uhakika.
   
 2. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [h=2]Mkuu unatoa data wapi za UCHUMI?
  BOFYA HAPA...

  Tanzania

  Tanzania[/h]

  Tanzania is one of the few countries in Africa, which has enjoyed peaceful political development. Stable political leadership has kept the country out of numerous conflicts, which have been afflicting a number of neighbouring countries. Since 1995, Tanzania has benefited from high annual GDP growth, averaging almost 6 percent since 2000. However, despite the government's efforts to address poverty, Tanzania's income levels continue to be amongst the lowest in Africa. Today, half of all Tanzanians live below the poverty line and approximately one-third live in abject poverty. Infant and maternal mortality rates remain amongst the highest in the world, literacy rates are low and more than one third of all children under five are malnourished. Nonetheless, the country has made progress towards achieving some of the Millennium Development Goal targets, in particular primary education, water and infant health. However, much more needs to be done if all targets are to be met.


   
 3. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @Barubaru. no comment.... ila nimalizie kwa kusema wewe ni kubwa jinga. Sorry for that.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mzalendo.

  Kwa bahati nzuri mimi ni mchumi kitaaluma lakin kikubwa zaidi nimefanya kazi kwenye serikali JMTz tena kwenye idara na wizara inayohusu hilo . Hivyo naujua uchumi wa Tanzania ndani nje nje ndani. Ila kama umenisoma vizuri hapo nimejikita katika kujenga miundombinu imara ya kukuza uchumi wa Tanzania. Na nimebainisha kuwa Barabara nzuri, Umeme wa uhakika, Sera safi za uwekezaji, natural resources na Political stability ni vitu muhimu sana kwa kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza.

  Kwa Tanzania hususan maenea ya Mtwara kuna fursa nyingi zaidi na faida zake na nimezibainisha. naomba unielewe lakin nimemaliza kwa kusema MTAJI MKUBWA WA UWEKEZAJI NI AKILI ZAKO mengine yote baadae.

  masawe,

  Siku zote Nyani haoni kundule bali huona la mwenzake.

  nakushauri ukipunguza USHABIKI na kuangalia uchumi wenu kwa mapana yake utajifunza mengi sana na utaacha KALAMIKA. kwani mtaji wa uwekezaji ni AKILI ZAKO na sio za ushabiki wako wa kisiasa.

  nakupa pole sana

  Nakupa pole sana
  .
   
 5. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ndugu katika bwana nakuonea huruma sana watakuja vijana hapa watakutukana na kukukashifu wao wanchotaka uweke mambandiko ya KULALAMIKA na YAKUIKASHIFU SERIKALI hapo utaelewana nao ila yakuisifu SERIKALI hata kwa mazuri inayoyafanya ni tatizo subiri uwaone wakija hapa
   
 6. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ninyi ndio wale wapinga kristo ila baada ya kristo kuondoka sasa ndio mmeanza kumkubali ila hata huyu aliyoko madarakani mtakuja kumkubali pale atakapoondoka
   
 7. k

  kamajana Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  barubaru nashaka na hiyo taaruma yako ya uchumi, kasome income inequality and the impact of uwekezaji unazosema then uje ufanye research ndani ya nchi hii na utuambie umepata nini. si kusema tu umeona mabarabara sijuii kwenda wapi mwanza kwani hayo yamejengwa na kikwete???
   
 8. N

  Nambombe Senior Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kanyoe ndevu hizo,zezeta wewe...uliolewa uarabuni nini.Du huku bara hakuna mabasha ni heri urudi huko huko. Yaani sisi ndio unatuona hatujui kitu,wewe na utahira wako ndio unajua mambo.
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Wakoloni wa Kijerumani ndio wa kwanza kujenga miundombinu ya reli nchini Tanganyika, Hata hivyo waliijenga kwa makusudi kabisa ya kusafirisha rasilimali za Watanganyika kwenda nje na kwmawe si kuwasaidia Watanganyika. Leo inapokengwa miundombinu hata ifike mbinguni, kama miundombinu hiyo haimuinulii mwnanachi hali yake ya maisha, miundombinu hiyo haina maana mbele ya macho ya wananchi.
   
 10. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Barabara nyingi zimejengwa ili utitiri wa magari ya Mtoto wake Rizone yapite pia ili Hoteli zake ziweze kufikika kiurahisi, pia unatakiwa ujue haya maendeleo unayoyaona sasa CCM walitakiwa wawe wameishayaleta tangu miaka yathemanini mwishoni hivyo hawana la kujitetea kwani wamechelewesha maendeleo yetu hivyo mabadiriko ni lazima ili kasi ya ukuaji wa uchumi na maendelea ya watanzania iende kwa usawa kusiwe na matabaka kama ilivyo sasa.
   
 11. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hivi uko serious au unatania?
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Barubaru,

  ..nadhani kwenye umeme serikali hii na CCM wameamua kulihujumu taifa.

  ..mgao wa umeme ulianza toka JK ni waziri wa nishati na bado umedumu mpaka leo hii.

  ..kwa upande wa barabara nadhani tunakuwa wachoyo wa shukrani kwa kutotaja jitihada za Raisi Mwinyi ktk kufufua barabara zetu. barabara ya kwenda kusini ilianza kujengwa wakati wa Mzee Ruksa, lakini sifa zote analundikiwa JK.
   
 13. ruhi

  ruhi JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,409
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  ungesema hoja hii kenya kwenu ungepigwa vibaya mno,ila kwa vile unaongee ukiwa Tanzania mi nakurusu ende kenya kwenu ili siku nyingize urudi uone mabadiliko kwani uwatakii watanzania mema....acha acha uongo ivi indicators za national development per income unazijua?
   
 14. a

  annalolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sitaki uchokozi hiyo ban ikupate mwenyewe
   
 15. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kwaiyo umeamua kuwa msemaji wa watanganyika? mungiki mna mambo!!!!!!!
   
 16. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jiambie wewe na wenzako mnaolalamika kila kukicha hapa...
   
 17. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  '...Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe eeee!...' Hata majambazi walitumia wimbo huo wakati wanateka mabasi na malori na kupora mali za walalahoi huko maporini. Wewe ni mchumi, tunakuheshimu kwa taaluma yako maana wengine sisi tupo tupo tu na akili zetu hazitoshi kuwekeza. Ulichosema ni kweli kuwa kwa Tanzania unahitaji akili tu kuwekeza ndiyo maana kuna mtu alikuja na buku moja lakini akawa bilionea ndani ya miaka michache tu. Kwa sababu ukiwa na akili, wapo watu kwenye system ambao watakufungulia milango 'ya uwekezaji'. Kama na wewe ni miongoni mwa hao wenye akili, basi heri yako. Hata hivyo, naomba unisaidie kujibu swali lililomshinda mheshimiwa JK huko ughaibuni, "KWA NINI TANZANIA/WATANZANIA NI MASKINI?"...pamoja na hayo uliyoyataja, pamoja na raslimali zote zilizopo, n.k.
   
 18. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Huyu aliyeko madarakani watu wataendelea kumkubali tu hata akiondoka madarakani au akifariki. Lakini watu hao ni wale tu , repeat, wale tu ambao hadi leo wanamkubali na mambo yake anayofanya kila siku, yaani wafuasi wake, mtandao wake na wale wote wanaotumiwa kwa manufaa binafsi au kwa kutokujua kwao... Hakuna mwingine atakayesema kuwa yule alikuwa mzuri sana labda atokee mwenye matatizo mengi sana kuliko yeye!
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nina wasiwasi na elimu yako. That is all.
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kama si yule anayenufaika moja kwa moja kutokana na kuwepo kwa serikali ya sasa madarakani, mwingine yeyote atakaye sema serikali ya sasa imefanya kazi nzuri atakuwa na matatizo makubwa ya akili, au atakuwa hajui anachoongea, au atakuwa na sababu za kidini, kabila, chama au mjinga. Ukweli ni wazi kuwa uchumi wetu kwa sasa si mzuri, huna haja ya kuangalia takwimu za watu, angalia tu sembe unayonuna inavypanda bei au sukari nyanya, chumvi na mkate. Huna haja ya kumsoma John Mills!
   
Loading...