Namshukuru Mungu (Nimezaliwa)

Paw

Content Manager
Nov 14, 2010
2,113
2,000
Nikiangalia nyuma yangu naona alama ya nyayo zikiwa zimekuja uelekeo wangu, nikitazama kwa umakini nagundua kuwa ni nyayo zangu hadi hapa niliposimama.

Sioni mwanzo wake ila naambiwa kuwa walioona mwanzo wa hatua zangu nilikuwa nashahibiana na haiba yangy ya leo. Lakini yote ni heri maana tangu nianze hatua za maisha nimekuwa ninasonga mbele nikivuka kila aina ya vikwazo. Kwa uchache naomba niwajuze kuwa nimeshawahi kulala juu ya miti na hata kushindia mizizi ili kunusuru maisha yangu hapo awali. Hakuna wa kulaumiwa ktk hili bali sana sana nimejifunza Upendo, Kujali na Utu wema kupitia maswahibu na mafanikio ya hatua za maisha.

Hivi leo najiangalia kwenye kioo nikijichunguza how handsome Am I, na kujua kilichomvuta King'asti kuamua kuyahaini maisha ya nyumbani kwao na kuja kuishi na kapuku mimi all the way. Looh si nimegundua kuna ndevu moja kama si mbili nyeupe, hivyo nikaangalia ukutani na kugundua kuwa leo nimeongeza Umri wa mwaka mmoja kuelekea uzeeni.

Nawashukuru Wana JF wote na marafiki zangu kwa kuwa nami all the way. Nimejifunza mengi kwa kufanya kazi na Administrators wetu (Invisible) na nimshukuru rafiki na kaka yangu Maxence Melo kwa kutenga muda wake kujibidiisha kunifundisha how hard work ninavyopaswa kuwa.

Ninamshukuru Mungu kwa kumjalia mama yangu kujifungua salama na kunilea hadi kufikia hatua ya mimi kulea wengine.
Namshukuru Mungu kwa Baba yangu alivyomwezesha kunifundisha how fathery should I be.

Blessings kwenu nyote
 
Last edited by a moderator:

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,756
2,000
Sasa baba haya mambo ya kujielezea uhandsome wako humu utaleta zahma.
Happy birthday baba watoto. Wewe ni baba mwema kwetu sote. Mungu azidi kukuongeza kila iitwapo leo. Wifi AshaDii anatuandalia sapraizi wote kwa sababu ukizaliwa wewe nami nakuwa mupya.

Kuna mtu hapa anangojea tuachane, miaka kama laki nane ijayo hivii....
 
Last edited by a moderator:

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,627

Nilikuwa nifungue case kama King'asti usinge tokea hapa!
 
Last edited by a moderator:

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,156
2,000
Paw, nimesoma vizuri ila nilipokuta jina la mkeo, ndo hamu ya kuendelea kusoma ikaishia hapo hapo.
 
Last edited by a moderator:

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,252
2,000
Shosti keki wapi???

Sasa baba haya mambo ya kujielezea uhandsome wako humu utaleta zahma.
Happy birthday baba watoto. Wewe ni baba mwema kwetu sote. Mungu azidi kukuongeza kila iitwapo leo. Wifi AshaDii anatuandalia sapraizi wote kwa sababu ukizaliwa wewe nami nakuwa mupya.

Kuna mtu hapa anangojea tuachane, miaka kama laki nane ijayo hivii....
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Paw

Miss Neddy

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,699
2,000
Sasa baba haya mambo ya kujielezea uhandsome wako humu utaleta zahma.
Happy birthday baba watoto. Wewe ni baba mwema kwetu sote. Mungu azidi kukuongeza kila iitwapo leo. Wifi AshaDii anatuandalia sapraizi wote kwa sababu ukizaliwa wewe nami nakuwa mupya.

Kuna mtu hapa anangojea tuachane, miaka kama laki nane ijayo hivii....
yaan ulikuwa unasubiri asubmit uwe wa kwanza ku comment huchez mbali
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom