Ushasema mfanyabiashara!! Mbona unaujichanganya hata hujui category za biashara. Au kwa kuwa kiongozi wa malaika ndio katoa hivyo vitambulisho? Acheni upumbavu kushabikia hata ujinga, kisa tu mfalme ndio kafanya. Poleni sana, kama mmeshindwa kuendesha nchi jiondoeni tu, sio mpaka mje muondolewe.
Mlidhani kununua upinzani ndio kukusanya kodi, mlidhani kuzuia mikutano ya siasa ndio kuboresha maisha ya mtanzania, mlidhani kuchota hela za hazina bila kibali cha bunge, ndio kuongeza ajira kwa watanzania, au mlidhani kuzuia bunge kurushwa live ndio kuongeza viwanda? Mkaenda mbali mkaanza kugombana na matajiri, wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji wa kila sekta, wawe wazawa au wageni ndio mkajua itaweza kulipa deni la taifa?
Poleni sana, naona mwisho umefika. Sasa mmerudi kuwatisha wananchi, tunajua mpango ulioko nyuma. Mkifanikiwa hili basi mtawale milele!!
Sent using
Jamii Forums mobile app