Namsaidiaje?

Namsaidiaje?

huu wala sio uzungu ni uzumbukuku!!
Hivi wanaume wengine wamekoma kuwa wanaume etieeee!!
Babuuuu hebu kwanza rudisheni jando jamani kweli huyu ni mwanaume kabisaaa aliyetahiriwa na baba yake??

Roho mbaya tu inakusumbua teacher...

Kwani hukuona mshikaji anasema kuwa aliletewa Laptop bomba akawa anachezea??

Duuuuuuuuuuuuu,......wengine hata ukiona pant mpya unauliza tu kiungwana huku mdau hastuki mkewe kupewa GBP 450 (Tsh, 1.15m)!!

Babu DC!!
 
Unajua ukioa ni vizuri pia uwe matured up stair......unaleta mambo ya kishamba na kizungu kwenye ndoa ......ujinga sana huu...
 
Rijali eee Ubuheri kweli mkuu? Natanguliza Samahani, Kumradhi ! Kama kweli wewe una Moyo au heartless ? huyu sii dada yako huyu ni mkeo. Uzungux2 wao usiwe juu ya mgongo wako.!! To stop msongo huu is 2 things:- Uongee na huyo fedhuli haraka (faragha au mbele ya mkewe/jamaa zake) ili ukate mzizi wa fitina once and for all. Na pili Mzungu wako kieleweke afuate maadili ya Dini yako(imani) LIMIT ZAKO udraw the redlines. Lazima ajue feelings zako haswa katika Umri huu ulafikia !! Since wewe hunaupungufu au kasoro zozote juu yake unafullfill ipasavyo. kusave ndoa ...je mna watoto? sasa chagua hapo. kwa upande wangu Nakuombea kwaMwenyeezzi Mungu amuondoe Ze Man kwenye masha yenu, Naupate unafuu.AMIN Goodluck
 
Kaka mkubwa hii ndoa yako umeivunja kwa ukosefu wako kuona mbali...
Ukiwa mwanandoa lazima uwe selfish, hakuna mtu anapaswa kuchezea mkeo...kuna mistari huwa inachorwa na hakuna mtu anapaswa kuvuka.
Wanawake siku zote hupenda kuwa na mtu ambaye anajua kulinda...
Weka kikao kizito kati yako wewe, mkeo, huyo shemeji yako na mkewe aliyetengana naye...
Kiwe kikao kizito kweli kama cha G8...na agenda ya kikao iwe ni wewe kueleza msimamo na terms zako...zaidi weka wazi boundaries.
Mpige kabisa marufuku huyo bwana kuingilia ndoa yako au lah muulize mkeo anachagua nani kati yenu aseme wazi...

'Miluzi mingi siku zote humpoteza mbwa'...ndivyo ambavyo mkeo anakaribia kupotea hivyo maana miluzi imemzidi masikioni mwake.
 
Polee saana..

naona mkeo ni 'mzungu' kiaina
na wewe 'mtoto wa uswazi' kiaina..
na hyo jamaa nae ni 'mzungu' kiaina

sasa kilichopo hapo 'hao wana natural chemistry' inawavuta pamoja

kazi kwako....

Hapo hakuna cha uzungu wala nini, hivyo vitu haviingii akilini. Lazima walikuwa na uhusiano fulani (siyo sexual).

Labda walikuwa wakipendana na akamuahidi kumuoa halafu kitu fulani kikaingia kati hapo na kila mtu akachukua njia yake. Matokeo yake hivi sasa wote wawili wanajuta. Na kwa maoni yangu ni huyo mwanamme ndiye anayemshawishi mkeo na anamuweka kwenye majaribu makubwa.

Samahani kama nimekuudhi hasa ukizingatia kwamba huyo ni mke wako wa ndoa, ni lazima huyo jamaa uzungumze nae kwa urefu (tete a tete) na umpe makavu live.
 
Yaani hiyo kesi ilikuwa ya kumaliza tokea day one, ni kwamba siku ile aliyokubali kuwa na wewe ndiyo siku ulitakiwa kudefine boundary na kucreate territory kama kobra.Hivo ndivo inavotakiwa mwanaume inatakiwa uwe na principles la sivo ukileta habari za uzungu zinakuumiza baadae.Mimi nilivomuoa mke wangu lazima nikuambie ukweli alikuwa anataka kuniletea habari za oooh alikuwa mate wangu hata discussion tulikuwa group moja mara sijui nini na alianza kwa kutaka mimi niwazee wasichana ambao walikuwa marafiki zake ili na yeye apatie mwanya wa kuendelea kuzoeana na company yake ya wavulana.
PetCash ndugu yangu kama nilivokwambia niliset principles nikaziwekea boundary then nikacreate territory kama ya nyoka yule anaeitwa Kobra nakuambia mpaka leo ni heshima hakuna ujinga ujinga nipo zangu busy na maisha ya mjini then nasimamishwa na tuvulana eti shem hajambo, shem hajambo my foot tupilia mbali wote.Mkishaoana mnatakiwa mwe na akili za kikubwa, ndoa siyo boyfriend wala girlfriend, ndoa ni taasisi kubwa tena nyeti kuliko hata BOT na TRA kwa hiyo ukibug imekula kwako.Pole sana angalia wapi ulitereza rudi nyuma kwa speed kubwa tena anzia hapo hapo kwenye laptop chimba mkwara mzito tena pachimbike hasa na hiyo ndiyo iwe starting point nakuambia uwe mbogo
 
Pet cash umepotea kweli siku hizi kiongozi!!

Naomba nikwambie haya ila ni machungu lkn dawa
......hivi wewe unaamini kwamba ulimzibua mkeo kisa tu alimwagika damu siku ya kwanza je unajua kwamba hata vizibo vya mchina vipo??
...sasa usemapo tukupe ushauri wafikiri sisi tutaweza kuvaa viatu vyako ya kwamba ww umeshindwa kuwa mume ndani mwako??

Hapo kwenye bold hata kwa Saleh madawa Zanzibar vipo! Waulize wa dada wa Zenji ha ha haaaa....
 
1.(Kwa mfano kwa sababu mimi ndo mwenye ex tunayewasiliana bado,
mazungumzo yetu hayaruhusiwi kuwa zaidi ya kujuliana hali).

hii ni hatari zaidi mpenzi wako kujua chochote kuhusu ex wako,the greatest mistake you ever did to your wife.
kwanza usifikiri kuwa anachukulia kawaida na kwake kukuruhusu kuwasiliana nae ni kujiwekea kinga kwake kuendelea kuwasiliana na huyo rafiki yake na mbaya zaidi anajua ulikuwa unadate nae na yeye hakuwahi kudate na mtu,automatically wewe unakosa uhalali wa kumhoji kwa sababu atakuuliza iweje wewe ulisex kabisa hakuhofii kuongea na ex wako lakini wewe umuhofie kuongea na rafiki ambaye hata kumtongoza hakuwahi.UMEJIFUNGA.
2.(
Najua kwa sababu hakuna kabla yangu aliyewahi)
(a)inawezekana kusex na demu partially na usimtoe bikra,una unauhakika gani kama demu wako hajawahi kumvulia jamaa nguo zote akatouch kila kona na hata kusex partially?
(b)inawezekana kutumia utaalamu wa kiafrika kurudisha bikra ama ule wa kichina to fake men,je una uhakika gani kuwa bikra ya demu wako ilikuwa original?
(b)kama ulishangaa kiss tu,je unajua wakiwa wao peke yao wanaenda mbali kiasi gani?je hawafanyi deep kiss,hawatomasani vile watakavyo?
ANZA KUFIKIRI TOFAUTI IMANI ULIYONAYO HAIPASWI KUFIKIA 100%
3.uzunguuzungu ulikuwa mwingi
wengine hupitia humuhumu si huna wasiwasi

4.(Na kama wanakuwa wapenzi ni kwa nini miaka yote hiyo wako close wasiwe?(No body was stopping them. Na nnajua hawajawahi kuwa hivyo)
kushiriki mapenzi siyo lazima wawe walishafanya sex,romance na kuzoeana kupita kiaasi wanaweza hata kukaa uchi wakachezeana na hii pia ni hatari zaidi mana wanaza kufikia huko muda wowote.

5.naamini itakuwa ngumu sana kwake kuvuka mipaka
ni ngumu ila inawezekana pia

6.(mnisaidie second year mimi)
pole sana ndo naenda kutoa ushauri maana wengi wanaonekana kupata wakati mgumu zaidi kukushauri na kiukweli kwa mada hii lazima uumize kichwa.
7.How do i rescue her before she breaks her heart?
-kwanza muite umueleze kuwa sasa huna raha na umekosa imani kama uhusiano huo ni wa kawaida kama ulivyooamini,usiogope mweleze mazingira yanayokupa wasiwasi zaidi.
-ili kuiokoa ndoa yako lazima sasa ubadili mfumo wa maisha na ile mipaka mliyowekeana inabidi muipitie upya mfano kama akihoji kwa nini wewe uendelee kuongea na mpenzi wa zamani inabidi uwe tayari kuachana na huyo ex wako naamini ukimweleza kuwa sasa wife hataki muongee anaona wivu atakuelewa
.hii itasaidia kuondoa kinga kwa demu kuendelea kuwa na ukaribu unaotiliwa mashaka
-pia mwambie kuwa uhusiano wa karibu unahatarisha ndoa zote mbili na hivyo kuna ulazima wa kubadili mfumo wa urafiki na maisha
-kimsingi hakuna tatizo kwa hizo zawadi hata kama ya mkeo ina pesa kubwa,ina tegemea alipanga kuwanunulia nini,kama alipanga kumnunulia laptop mke wako akakuta inauzwa
paundi 450 ulitaka afanyaje asinunue?hapana na hakupaswa kutumia gharama kupanga amununulie nini mkeo na mpenzi wako,mkufu ni zawadi sahihin kwa mke wake bila kujali gharama,hebu jiulize kama angemnunulia mkufu demu wako kwa pauni 300 na akamnunulia mke wake laptop kwa pauni 450 ingekuwaje?vuta picha hata mke wake angejisikiaje?ingekuwa balaa zaidi,mfano mwingine tuseme jamaa angenunua vyote viwili kwa mke wake alafu mke wako akamletea zawadi hata ya underwear,hivi hapo utafikiria kupitia gharama ama kupitia aina ya zawadi/jibu unalo mwenyewe
HII SASA HAPANA
(Mke wangu amekuwa mkimya too much hata siku moja tulikuwa tunatoka kazini kila nikianzisha stori
inakufa niakaamua kunyamaza nimuobserve almanusura apitilize nyumba(alikuwa anaendesha).
HAPO KUNA KITU KINAMSUMBUA SANA NA HAJUI AFANYE NINI JUU YA MAAMUZI MAGUMU ANAYOYAFIKIRIA.
na maamuzihayo yanakuhusu wewe na si mtu mwingine na pengine anafikiria ni namna gani anaweza kukuacha mana hana raha tena na ndoa yake na kama kinachomsumbua hakikuhusu ama si kibaya kwako angekuwa mwepesi zaidi kukushirikisha ili umusaidie lakini hapa anafikiria aanzaje kukuambia ukweli ama kuanzisha tatizo
(Siku moja nilimuacha mke akichat naye sebuleni narudi namkuta anafuta machozi fasta! Nilimbana cku hiyo hadi karibu tugombane.
Ni kazi? hapana, nyumbani? hapana wazazi? hapana nimekuudhi? hapana. Ni hormones? hapani Nikamtaja jamaa aliyechati naye
labda kamuudhi akashtuka kidogo then hapana!Nikamkomalia tukaelekea kugombana ikabidi nimuache.)

HATA KAMA NILIKUWA USINGIZINI NINGESHITUKA NA USINGIZI UNGEPOTEA GHAFLA.
pamoja na kumuuliza alikaa kimya kwa sababu yaliyomfanya atoe machozi si mambo madogo na jiulize WEWE AMESHAKUTOLEA MACHOZI KWA JAMBO LA KAWAIDA?kwa wenye akili hakuna hata sababu ya kuendelea kuhoji kama alikataa kutoa ushirikiano wowote na kwa USHAMBA WAKO KAMA WA MSHINGA UKAONA UPOTEZEE

Polee saana..

naona mkeo ni 'mzungu' kiaina
na wewe 'mtoto wa uswazi' kiaina..
na hyo jamaa nae ni 'mzungu' kiaina

sasa kilichopo hapo 'hao wana natural chemistry' inawavuta pamoja

kazi kwako....
itakula kwake ni hatari sana
 
Yaani hiyo kesi ilikuwa ya kumaliza tokea day one, ni kwamba siku ile aliyokubali kuwa na wewe ndiyo siku ulitakiwa kudefine boundary na kucreate territory kama kobra.Hivo ndivo inavotakiwa mwanaume inatakiwa uwe na principles la sivo ukileta habari za uzungu zinakuumiza baadae.Mimi nilivomuoa mke wangu lazima nikuambie ukweli alikuwa anataka kuniletea habari za oooh alikuwa mate wangu hata discussion tulikuwa group moja mara sijui nini na alianza kwa kutaka mimi niwazee wasichana ambao walikuwa marafiki zake ili na yeye apatie mwanya wa kuendelea kuzoeana na company yake ya wavulana.
PetCash ndugu yangu kama nilivokwambia niliset principles nikaziwekea boundary then nikacreate territory kama ya nyoka yule anaeitwa Kobra nakuambia mpaka leo ni heshima hakuna ujinga ujinga nipo zangu busy na maisha ya mjini then nasimamishwa na tuvulana eti shem hajambo, shem hajambo my foot tupilia mbali wote.Mkishaoana mnatakiwa mwe na akili za kikubwa, ndoa siyo boyfriend wala girlfriend, ndoa ni taasisi kubwa tena nyeti kuliko hata BOT na TRA kwa hiyo ukibug imekula kwako.Pole sana angalia wapi ulitereza rudi nyuma kwa speed kubwa tena anzia hapo hapo kwenye laptop chimba mkwara mzito tena pachimbike hasa na hiyo ndiyo iwe starting point nakuambia uwe mbogo

Umeongea mambo matatu ya mhimu sana kwa ajili ya kuwa salama katika ndoa ambayo ni principles, boundary then territory yaani ukiyaweza haya hata mtoto wa Obama unamuweka ndani na anatii kama maji mtungini lakini ukiingiza ugirlfriend na uboyfriend wafya lelo
 
Huo ujinga uliulea mwenyewe toka mwanzo,we mwafrika utaruhusu vp mkeo awe na ukaribu na rafiki wake wa kiume namna hyo?
 
Sasa waungwana nahisi mke wangu anaanza kufall kwa jamaa(Na jamaa vilevile). Natamani kumuuliza wife lakini
1) Sipendi kuonekana mwanaume mwenye wivu kumuingilia wakati tulishadefine mipaka na hajacross...
2) Na kama wanakuwa wapenzi ni kwa nini miaka yote hiyo wako close wasiwe?(No body was stopping them. Na nnajua hawajawahi kuwa hivyo)
3) Nimekomaa sana kumjali na kumtunza mke wangu na yeye pia vilevile na naamini itakuwa ngumu sana kwake kuvuka mipaka,
lakini nafanyaje sasa kumrudisha wakati moyo wake unaenda huko? How do i rescue her before she breaks her heart?
4) Naombeni mnishauri kwa sababu mtu akimpenda mtu hata nipige mikwara kama kweli wakidhamiria kufanya mi naepushaje?
5) Mliishije/Mnaishije kwenye ndoa zenu kuepuka haya?(mnisaidie second year mimi)

Kweli wewe ni fedha tu ya matumizi madogo (Petty Cash)
Huna mke hapo wewe.
Lazimisha kupata ukweli
Ukishindwa mrudishe kwako
Huku ukifuatilia inakuwaje.
Kama huwezi, lazimisha kuiona simu yake,
Au kuwa jasusi tafuta password ya mawasiliano na kuiyaingilia.
Ukishindwa andika talaka.

Ndimi Bazazi!
 
Jaribu kuupeleka huu uzungu kwa mke wa jamaa uone. Yaani hata mke wa jamaa amekuzidi akiri ya kujua kuwa Mwanamke anaweza kuwekwa reserve kwa muda lakini ipo siku atakuja kuliwa tu. Binafsi uzungu kama huu sioni mantiki yake, kama ni Patrilineal family komesha hili na kama ni matrilineal family subiri mpaka ukute vikombe vya uji aliokunywa jamaa ndio utakua na maamuzi mazuri.
 
naona unamfariji kwa kumpa panadol, kaka malaria hiyo tena anatakiwa awekewe drip za kwinin kabisa.
ahaha Mi nnachoona hapo ni kuwa hamna cheating wala nini..sema uzungu uzungu umezidi..afu we mwenyewe hujui mambo hayo ahahha ndo inabidi ujifunze sasa...dont change the players change the game... anza kumualika huyo mshkaji hapo home makusudi uone wanavokuwa mbele yako ...mwisho utaelewa ni nini..ila kuhusu cheating sio kweli.wangefanya kwanzia kipindi hicho...hai make sense.
 
Ulitoa mahari kweli?

Siwwezi kuteswa na mahari yangu mwenyewe, ningemrudisha kwao hadi atakapojifunza adabu.
 
Nipo mwalimu gfsonwin,
Dah! Mkuu hebu punguza jazba kidogo. I am a man in my home, na ningeweza kukupa mfano jinsi nnavyohandle mambo.
Halafu hii ni unhandled issue. Ningelianzisha wakati wa laptop then nisingeona kina cha tatizo lenyewe, na hapa nnawaza how to handle hii issue with minimum casualty. Nikimind akaenda kwao then nikaweka stop kwenye huo urafiki, kama kweli wamependana, ndo ntakuwa nimewazuia wasifanye? Do i know they are doing it?
Nikimpa talaka ndo solution?

BTW: Haiwezekani kuwa alifoji kuwa virgin kwa sababu hakuwahi kuniambia yuko hivyo na sikutegemea alikuwa hivyo, ilitokea tu nikamkuta hivyo.

Halafu sioni kuwa kumgombeza mke kila afanyapo kosa ndiyo hulka za kiume, na haiwezekani niwe less of a man kwa kufanya mambo yote sawa ila hilo. Hao wanaokuwa wakali ndo ndoa zinadumu?

huu wala sio uzungu ni uzumbukuku!!
Hivi wanaume wengine wamekoma kuwa wanaume etieeee!!
Babuuuu hebu kwanza rudisheni jando jamani kweli huyu ni mwanaume kabisaaa aliyetahiriwa na baba yake??

Lakini jamani ukweli tuseme, mwanaume bila hulka za kiume wewe si mwanaume hata uwe mzuri, una pesa na mali kiasi gani bila kuwa na ile misingi ya kiume weee ni mbulula tu
 
Last edited by a moderator:
Thank u Mkuu, Ntajaribu kufuatilia hatua kwa hatua

1.(Kwa mfano kwa sababu mimi ndo mwenye ex tunayewasiliana bado,
mazungumzo yetu hayaruhusiwi kuwa zaidi ya kujuliana hali).

hii ni hatari zaidi mpenzi wako kujua chochote kuhusu ex wako,the greatest mistake you ever did to your wife.
kwanza usifikiri kuwa anachukulia kawaida na kwake kukuruhusu kuwasiliana nae ni kujiwekea kinga kwake kuendelea kuwasiliana na huyo rafiki yake na mbaya zaidi anajua ulikuwa unadate nae na yeye hakuwahi kudate na mtu,automatically wewe unakosa uhalali wa kumhoji kwa sababu atakuuliza iweje wewe ulisex kabisa hakuhofii kuongea na ex wako lakini wewe umuhofie kuongea na rafiki ambaye hata kumtongoza hakuwahi.UMEJIFUNGA.
2.(
Najua kwa sababu hakuna kabla yangu aliyewahi)
(a)inawezekana kusex na demu partially na usimtoe bikra,una unauhakika gani kama demu wako hajawahi kumvulia jamaa nguo zote akatouch kila kona na hata kusex partially?
(b)inawezekana kutumia utaalamu wa kiafrika kurudisha bikra ama ule wa kichina to fake men,je una uhakika gani kuwa bikra ya demu wako ilikuwa original?
(b)kama ulishangaa kiss tu,je unajua wakiwa wao peke yao wanaenda mbali kiasi gani?je hawafanyi deep kiss,hawatomasani vile watakavyo?
ANZA KUFIKIRI TOFAUTI IMANI ULIYONAYO HAIPASWI KUFIKIA 100%
3.uzunguuzungu ulikuwa mwingi
wengine hupitia humuhumu si huna wasiwasi

4.(Na kama wanakuwa wapenzi ni kwa nini miaka yote hiyo wako close wasiwe?(No body was stopping them. Na nnajua hawajawahi kuwa hivyo)
kushiriki mapenzi siyo lazima wawe walishafanya sex,romance na kuzoeana kupita kiaasi wanaweza hata kukaa uchi wakachezeana na hii pia ni hatari zaidi mana wanaza kufikia huko muda wowote.

5.naamini itakuwa ngumu sana kwake kuvuka mipaka
ni ngumu ila inawezekana pia

6.(mnisaidie second year mimi)
pole sana ndo naenda kutoa ushauri maana wengi wanaonekana kupata wakati mgumu zaidi kukushauri na kiukweli kwa mada hii lazima uumize kichwa.
7.How do i rescue her before she breaks her heart?
-kwanza muite umueleze kuwa sasa huna raha na umekosa imani kama uhusiano huo ni wa kawaida kama ulivyooamini,usiogope mweleze mazingira yanayokupa wasiwasi zaidi.
-ili kuiokoa ndoa yako lazima sasa ubadili mfumo wa maisha na ile mipaka mliyowekeana inabidi muipitie upya mfano kama akihoji kwa nini wewe uendelee kuongea na mpenzi wa zamani inabidi uwe tayari kuachana na huyo ex wako naamini ukimweleza kuwa sasa wife hataki muongee anaona wivu atakuelewa
.hii itasaidia kuondoa kinga kwa demu kuendelea kuwa na ukaribu unaotiliwa mashaka
-pia mwambie kuwa uhusiano wa karibu unahatarisha ndoa zote mbili na hivyo kuna ulazima wa kubadili mfumo wa urafiki na maisha
-kimsingi hakuna tatizo kwa hizo zawadi hata kama ya mkeo ina pesa kubwa,ina tegemea alipanga kuwanunulia nini,kama alipanga kumnunulia laptop mke wako akakuta inauzwa
paundi 450 ulitaka afanyaje asinunue?hapana na hakupaswa kutumia gharama kupanga amununulie nini mkeo na mpenzi wako,mkufu ni zawadi sahihin kwa mke wake bila kujali gharama,hebu jiulize kama angemnunulia mkufu demu wako kwa pauni 300 na akamnunulia mke wake laptop kwa pauni 450 ingekuwaje?vuta picha hata mke wake angejisikiaje?ingekuwa balaa zaidi,mfano mwingine tuseme jamaa angenunua vyote viwili kwa mke wake alafu mke wako akamletea zawadi hata ya underwear,hivi hapo utafikiria kupitia gharama ama kupitia aina ya zawadi/jibu unalo mwenyewe
HII SASA HAPANA
(Mke wangu amekuwa mkimya too much hata siku moja tulikuwa tunatoka kazini kila nikianzisha stori
inakufa niakaamua kunyamaza nimuobserve almanusura apitilize nyumba(alikuwa anaendesha).
HAPO KUNA KITU KINAMSUMBUA SANA NA HAJUI AFANYE NINI JUU YA MAAMUZI MAGUMU ANAYOYAFIKIRIA.
na maamuzihayo yanakuhusu wewe na si mtu mwingine na pengine anafikiria ni namna gani anaweza kukuacha mana hana raha tena na ndoa yake na kama kinachomsumbua hakikuhusu ama si kibaya kwako angekuwa mwepesi zaidi kukushirikisha ili umusaidie lakini hapa anafikiria aanzaje kukuambia ukweli ama kuanzisha tatizo
(Siku moja nilimuacha mke akichat naye sebuleni narudi namkuta anafuta machozi fasta! Nilimbana cku hiyo hadi karibu tugombane.
Ni kazi? hapana, nyumbani? hapana wazazi? hapana nimekuudhi? hapana. Ni hormones? hapani Nikamtaja jamaa aliyechati naye
labda kamuudhi akashtuka kidogo then hapana!Nikamkomalia tukaelekea kugombana ikabidi nimuache.)

HATA KAMA NILIKUWA USINGIZINI NINGESHITUKA NA USINGIZI UNGEPOTEA GHAFLA.
pamoja na kumuuliza alikaa kimya kwa sababu yaliyomfanya atoe machozi si mambo madogo na jiulize WEWE AMESHAKUTOLEA MACHOZI KWA JAMBO LA KAWAIDA?kwa wenye akili hakuna hata sababu ya kuendelea kuhoji kama alikataa kutoa ushirikiano wowote na kwa USHAMBA WAKO KAMA WA MSHINGA UKAONA UPOTEZEE

Kaka mkubwa hii ndoa yako umeivunja kwa ukosefu wako kuona mbali...
Ukiwa mwanandoa lazima uwe selfish, hakuna mtu anapaswa kuchezea mkeo...kuna mistari huwa inachorwa na hakuna mtu anapaswa kuvuka.
Wanawake siku zote hupenda kuwa na mtu ambaye anajua kulinda...
Weka kikao kizito kati yako wewe, mkeo, huyo shemeji yako na mkewe aliyetengana naye...
Kiwe kikao kizito kweli kama cha G8...na agenda ya kikao iwe ni wewe kueleza msimamo na terms zako...zaidi weka wazi boundaries.
Mpige kabisa marufuku huyo bwana kuingilia ndoa yako au lah muulize mkeo anachagua nani kati yenu aseme wazi...

'Miluzi mingi siku zote humpoteza mbwa'...ndivyo ambavyo mkeo anakaribia kupotea hivyo maana miluzi imemzidi masikioni mwake.

Hahaha,kikao zaidi ya kile cha G8....wapi Condoleeza Rice
 
Back
Top Bottom