daaaaaaahhhh
PetCash kwanza nikueleze thread yako imenimaliza nguvu,nimeiona nikaishiwa pozi maanke najaribu kujiweka under your shoes na kuona jinsi hali unavyokabili ni ngumu kiasi gani nabaki naumia mwenyewe ndani ya moyo.Pole sana kwa kuwa katika wakati mgumu.Naomba nikushauri haya yafuatayo labda yatasaidia kwa kiasi fulani:
1.tambua kwamba hilo ni tatizo tayari ndani ya ndoa na maisha yako kwa ujumla,so kinachotakiwa hapo ni kulikabili na sio kulikimbia kwani kukimbia matatizo yetu sio suluhisho hata kidogo.
2.huenda tokea mwanzoni mkeo na rafikiye walikuwa wamefikia hatua ya upenzi ila sema ndo hivyo tena labda walikuwa kidogo na maadili na wakaweza kujiwekea mipaka,na labda hawakuishia kuoana kwa heshima iliyokuwepo baina ya familia zao mbili(lakini mioyoni kila mmoja anatamani wangekuwa pamoja its possible)
3.No way mkuu hii ndo njia peke itakayomaliza mgogoro wako ulionao kichwani kwa sasa,usifikie mkataa wa fasta kuwa mkeo anampenda jamaa(japo hilo pia lawezekana pia)
a).anza kufanya uchunguzi wa chini chini(mkeo aisshtukie chochote)chunguza anatumia muda mwingi kiasi gani kuwasiliana na jamaa kwa maongesi ya simu au hata sms.
b).panga hata visafari vya uwongo ili ujue akibaki peke yake anautumia muda mwingi peke yake akiendelea na shughuli zake au anutumia kuwa pamoja na huyo mbeste wake kama kumtembela nyumbani ofisini na n.k.
c).tembelea ofisini kwake bila taarifa na bila yeye kujua na mara kwa mara ili ujue ikiwa jamaa anamtembela wife mara kwa mara na kwa minajili ipi na wife anampokeaje na analichukualiaje hilo(hapa ukigundua jamaa huwa anenda ofisini kwa wife often na wife anaona poa tu na wala hakutonyi kitu jaribu kumuuliza kiujanja aisishtukie kitu akikuambia ukweli pumua kidogo na ujue kuwa huenda kweli wenzetu uzungu untaka kuwaponza,ila aikpiga chenga tu oohh hapa huwa haji kabisa au mara moja moja shtuka washa taa nyekundu kichwani)
d).panga mlo wa jioni au outings yoyote mkiwa wote watatu au wanne(kama mke wa jamaa akirudi)huko utaona reaction itakoyoweza jitokeza baina yao(kwani penzi ni kikohozi,na hope we pia uliona baadhi ya ishara kutoka kwake kuwa amefall kwako na kukupa go ahead ya kumuaproah,tumia hizohizo pia kujua ana feel nini kwa mjamaa)
Mwisho mkuu ukishafanya utafiti wako na kugundua kuwa watu hao wanapendana,mchukue wife kaa naye chini na umuulize kwa upole bila kugomba mfanye ajihisi salama na huru,mweleze matokeo ya utafiti wako ukiwa na proof halafu usikie maoni yake(kama si msaliti na si mwongo ukimpa evindence za kutosha huenda akafunguka na kukueleza ya moyoni hasa akijua pote alipokuwa anapita ulipita pia hatakuwa na jinsi ya kudanganya soo ni obvious atakwambia ukweli ikiwa na feelings kwa huyo jamaa au la)akikwambia kuwa anahisia naye(japo hii si rahisia sana ila kama mmkeuwa mnaishi vizuri inawezekana na huenda akaanza na am sorry my husband najua hili sio jambo zuri kwako hata kidogo lakini naomba tu niwe muwazi kweli nilikuwa nampenda sana lakini hivi nina wewe simuwazi yeye tena na hata ukaribu niliokuwa nimeanza kuwa naye naufuta kama unakauumiza mwanzoni sikujua kuwa unaumia ila as long as umeniambia i promise i will be faithfull to you na nitapunguza ukaribu ili uwe na furaha)hii inawezeakana ikiwa tu mmekuwa mnaishi naye vizuri na ikiwa ana lepe la aibu na maadili fulani ndani yake,na kwa kuwa ulisema u were the first huenda hiyo pia ikamimpress kustick na wewe as inasemekana a woman will never forget the first man to make love with,ikitokea akakiri makosa yake na kuomba muendelee basi waweza mpa nafasi na kuzidisha upendo kwake,na ukiona najisahau na jamaa wake unamshtua then u go on.
Lakini kama ikitokea akakueleza ukweli kuwa anampenda jamaa sana na anahsi kuwa moyo wake haupo kwako tena mpe uhuru(inahitaji kujikaza kiume vinginevyo utajikuta hujui unachokiongea na mwishowe kuwa chizi)mwambie muende mahakamani mpeane talaka kila mtu ajijue,kama atavunja ndoa ya jamaa ili ye achukue nafasi au nini ni juu yake huku na we unatafuta ustaarabu mwingine(mkuu it's not easy lakini itakubidi ufanye hivyo kwani tofauti na hapo mtakuwa ndani ya ndoa kwa ajili ya mazoea na si mapenzi jambo ambalo halifai kwani ndoa inapaswa iunganishwe na mapenzi tu na si vinginevyo,na pia unaweza kujikuta umekuwa mtumwa wa mapeznizi unafanya mambo ili tu kumimpress wife asimfikirie jamaa).
Kiukweli mkuu uko kwenye verryyy hard situation mi mwenyewe inaniumiza kichwa :confused2: :confused2: :confused2: :confused2:,samahani kwa hotuba ndeeeeffffuuu ni kwa kuwa hata mi natapatapa kutafuta solution ya hilo janga,hope nitakuwa nimesaidia kwa kiasi fulani.