Namsaidiaje?

Namsaidiaje?

Kaka, kwa kweli pole kwa hayo yanayotokea kwenye ndoa yako. Tafadhali jua na amini kuwa si rahisi ukajijua wewe mwenyewe kwa 100% na hasa udhaifu wako. Ni dhahiri mdogo wangu unayo mapungufu ambayo mke wako hakuyajua mwanzoni wakati wa uchumba. Kwa jinsi walivyo wengi wao, amekustadi, akaona udhaifu wako ulipo na akakulinganisha na "rafiki yake wa kiume". Anadhani kuwa, kwa vile mlishaoana na watu wote wanajua basi ni aibu kukwambia baadhi ya mambo ambayo yatakuumiza, anaona ni bora iwe kimya kimya tu potelea mbali ukija gundua utaamua kumuuliza na atakataa... anaamini hutakuwa na ushahidi dhahiri kuwa anagawa p... nje. Na pengine kama anajua kuwa alishawahi kukuambia/kukulalamikia juu ya wewe kutomfikisha kunako theluji za Evarest,basi kwake yeye anachukulia hicho kama msingi wa uhalali wa yeye kuyakuza mahusiano yake na huyo mme mwenza wako. USHAURI WANGU: Hakikisha kila mmoja wenu anakuwa na Uhuru usiozidi 50% (Wewe 50% na yeye pia 50%) hii itawasaidia kwa kila mmoja wenu kujiona kuwa hakandamizwi, hanyonywi, hapuuzwi na wala hana haki ya kufanya jambo lolote zuri au baya pasipo kumshirikisha mwenzake.(Ndoa ni ya wawili, si mmoja bhana!) Pia kuwa na kiasi katika kumpenda. Usimpende hadi ukashindwa kumkaripia na kumshauri kwa tabia zake zinazokukera na ambazo kabisa unaziona ni hatarishi kwa ndoa yenu. Ukishindwa kabisa, basi hebu washirikishe watu wengine unaoamini wana hekima na heshima ili wawashauri nyote kwa pamoja ama peke yake kwa kadiri ya uwezekano. vinginevyo ningependa kujua hali ya ndoa yenu baada ya mwezi mmoja.
 
Kaka, kwa kweli pole kwa hayo yanayotokea kwenye ndoa yako. Tafadhali jua na amini kuwa si rahisi ukajijua wewe mwenyewe kwa 100% na hasa udhaifu wako. Ni dhahiri mdogo wangu unayo mapungufu ambayo mke wako hakuyajua mwanzoni wakati wa uchumba. Kwa jinsi walivyo wengi wao, amekustadi, akaona udhaifu wako ulipo na akakulinganisha na "rafiki yake wa kiume". Anadhani kuwa, kwa vile mlishaoana na watu wote wanajua basi ni aibu kukwambia baadhi ya mambo ambayo yatakuumiza, anaona ni bora iwe kimya kimya tu potelea mbali ukija gundua utaamua kumuuliza na atakataa... anaamini hutakuwa na ushahidi dhahiri kuwa anagawa p... nje. Na pengine kama anajua kuwa alishawahi kukuambia/kukulalamikia juu ya wewe kutomfikisha kunako theluji za Evarest,basi kwake yeye anachukulia hicho kama msingi wa uhalali wa yeye kuyakuza mahusiano yake na huyo mme mwenza wako. USHAURI WANGU: Hakikisha kila mmoja wenu anakuwa na Uhuru usiozidi 50% (Wewe 50% na yeye pia 50%) hii itawasaidia kwa kila mmoja wenu kujiona kuwa hakandamizwi, hanyonywi, hapuuzwi na wala hana haki ya kufanya jambo lolote zuri au baya pasipo kumshirikisha mwenzake.(Ndoa ni ya wawili, si mmoja bhana!) Pia kuwa na kiasi katika kumpenda. Usimpende hadi ukashindwa kumkaripia na kumshauri kwa tabia zake zinazokukera na ambazo kabisa unaziona ni hatarishi kwa ndoa yenu. Ukishindwa kabisa, basi hebu washirikishe watu wengine unaoamini wana hekima na heshima ili wawashauri nyote kwa pamoja ama peke yake kwa kadiri ya uwezekano. vinginevyo ningependa kujua hali ya ndoa yenu baada ya mwezi mmoja. Waweza bado ku PM in case of any query.
 
Mkuu hapa inabidi uwe ngangari na kupiga marufuku uhusiano uliopo kati ya mkeo na huyo jamaa na una sababu za kutosha za kufikia uamuzi huo. Hata mawasiliano ya simu usiruhusu, kwenda kazini kwa mkeo marufuku kwa kifupi wakate mawasiliano ya aina yoyote na wakati huo huo uendelee kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha maamuzi yako yanafuatwa. Kama hutajali rudi hapa kutufahamisha maamuzi yako na yatakayojiri siku za usoni. Kila la heri katika kunusuru ndoa yako.
Lkn umeona kwamba huyu ndugu ndiye aliyeweka mwanya wa haya ukisoma paragraph ya kwanza anasema "Kwa mfano kwa sababu mimi ndo mwenye ex tunayewasiliana bado,
mazungumzo yetu hayaruhusiwi kuwa zaidi ya kujuliana hali).


" Kwanini yeye anaendelea kuwasiliana na ex ili iweje, je bado ana hisia za huyo ex au anataka kuzidumisha hisia alizonazo kwa huyo ex. Nikirudi kwenye topic ni hivi PetCash huo sio uzungu wala nini mbona wazungu tunawaona hawana mambo hayo lbd hao wazungu wenye tabia hizo ni wa nchi gani.kwa mtazamo wangu naona bora uweke wazi mashaka yako ikiwa ni pamoja na kukaa ninyi 4 (hizo pair 2 ie familia ya jamaa na yako) kama ulivyoshauriwa weka msimamo wako wazi na ni haki yako. kumbuka ukiamua kuoa/kuolewa kuna vitu unapaswa kuviacha for the sake of marriage . Zingatia ushauri uliopewa naamini utapata suluhisho.
 
Last edited by a moderator:
Hii ngoma ni ngumu ila mimi nashauri yafuatayo
1.wewe binafsi acha kuwasiliana kabisa na huyo ex wako.
2.ukilifanikisha namba 1 hapo juu then mwambie mke wako aache kuwasiliana na huyo the so called friend
3.behave like a man. Kuna vitu kama mwanamume kiongizi wa familia unatakiwa kuhoji na kuvisimamia. Inakuwaje mke aje na kitu cha thamani kama hicho halafu wewe usihoji? Hata kama alikuwa kwa mfano amenunua je hamna policy ya matumizi katika ndoa yenu?je hamshauriani mnapotaka kufanya matumizi makubwa?
4.Hata kama mkeo amekulia uzunguni ila mnapooana mnatengeneza mfumo mpya wa kuishi. usifanye mfumo alioisho yeye au wewe utawale maisha yenu. Tengenezeni mfumo chotara ambao utawawezesha nyote kwa pamoja kuishi kwa amani bila
kukwazana. Mfumo huo wa kizungu mnaoutumia sasa ni majanga kwa ndoa yenu.
5. Funguka kwa mkeo jinsi unavyojisikia ili aelewe unavyotatizika na mahusiano yake na jamaa na mueleze pia mahusiano yake na huyo jamaa yanaharibu hata ndoa ya huo upande wa pili na yanakutia wasiwasi hata wewe.kwa hiyo kuokoa ndoa zote mbili ni muhimu mkeo aache kabisa kuwasiliana na jamaa
6.Mshauri mkeo kwa kuwa laptop imeleta hali ya sintofahamu, ni busara kama atairudisha, na amueleze wazi jamaa bila kumficha sababu ya yeye kuirudisha.
7.kama ni waumini wa dini yeyote, basi ishini kwa mfumo wa maisha ya dini hiyo,huu uzungu utawafikisha pabaya.
Pole sana mkuu, wivu ukizidi unakuwa gubu ila kuna nyakati unalazimika kufanya wivu kwa mkeo!
 
Hiviiii, kungekuwa na uhusiano wa usiri jamaa angempa zawadi ya laptop best friend wake mbele ya mkewe? Si angekuwa more careful basi angedanganya kuwa alimuagiza (kwa kumpa pesa kabla)?

Halafu what is more romantic, zawadi ya laptop au mkufu?

Sioni mapungufu ya 'umume' wa PetCash kwa kuihandle issue the way alivyoihandle, ila ili apate tulizo he has to spell all his worries kwa mkewe na labda wadiscuss terms zingine ili awe na amani.
Naunga unachosema ni kweli na inawezekana kabisa lakini kumbuka kuwa mtu akiamua kusaliti lazima kwanza ajue mapungufu yako ndipo aamue mbinu atakayo tumia ikiwa ni kuweka wazi sana ili iwe ngumu kushituka kama wewe usivyoamini kuwa ingewezekanaje wapenzi wakapeana vitu kwa uwazi kiasi hicho, lakini pia mapenzi yanaweza kuwa ya siri hata kugundua ikawa ngumu.

Hata hivyo kumbuka mtu anaweza aka-pretend hata kwa miaka mitano bila kugundulika hasa mwanamke, kibaya zaidi hawa watu wana mwaka mmoja katika ndoa kipindi ambacho huwa ni kitamu sana na cha furaha mno lakini wao kasoro zimeanza tena mpaka kusababisha mtu kwenda ukweni, kweli unahisi hii ni hali ya kawaida?????

Piga picha baada ya miaka mitano, kumi na kuendelea iatakuwaje. Huyu jamaa anatakiwa awe serious katika kushughulikia hili swala wakati ndoa ingali changa kabla haijaota mizizi kwani itakuwa ngumu kumbadilisha mkewe hapo badaye kuliko sasa, itakuja kuonekana kana kwamba yeye (mwanaume) ndiye aliyebadilika na kusababisha matatizo.
 
Naunga unachosema ni kweli na inawezekana kabisa lakini kumbuka kuwa mtu akiamua kusaliti lazima kwanza ajue mapungufu yako ndipo aamue mbinu atakayo tumia ikiwa ni kuweka wazi sana ili iwe ngumu kushituka kama wewe usivyoamini kuwa ingewezekanaje wapenzi wakapeana vitu kwa uwazi kiasi hicho, lakini pia mapenzi yanaweza kuwa ya siri hata kugundua ikawa ngumu. Hata hivyo kumbuka mtu anaweza aka-pretend hata kwa miaka mitano bila kugundulika hasa mwanamke, kibaya zaidi hawa watu wana mwaka mmoja katika ndoa kipindi ambacho huwa ni kitamu sana na cha furaha mno lakini wao kasoro zimeanza tena mpaka kusababisha mtu kwenda ukweni, kweli unahisi hii ni hali ya kawaida????? Piga picha baada ya miaka mitano, kumi na kuendelea iatakuwaje. Huyu jamaa anatakiwa awe serious katika kushughulikia hili swala wakati ndoa ingali changa kabla haijaota mizizi kwani itakuwa ngumu kumbadilisha mkewe hapo badaye kuliko sasa, itakuja kuonekana kana kwamba yeye (mwanaume) ndiye aliyebadilika na kusababisha matatizo.
Uko sahihi kwa kiwango kikubwa; lakini he has to be smart about it, maana ushauri mwingi alioupewa akiubeba the way ulivyo anaweza bomoa badala ya kujenga. Benefit of doubt ni muhimu, natumaini analielewa hili; na hilo la kuzuia mahusiano kati ya mkewe na friend wake, yaweza bomoa maana ni kumlazimisha achoose betwee two unequal yet important people. Umuhimu wa mume hauwezi kuwa sawa na wa rafiki, na wa rafiki hauwezi kuwa sawa na mume; so he might loose completely au akasababisha uhusiano wao ukawa wa siri na baadaye kwenda another level ambayo mume anaweza akaipanda kwa kumuhisi. Imagine, akimtuhumu kuwa ni bwana wake, tayari anamuwekea wazo au image ya friend kuwa bwana (in bed and all that), na kero (nagging) zikizidi; badala ya mwanzo alivyokua say anapata ushauri tu sasa itaenda kwenye kukumbatia na mambo mengine. Kwa maoni yangu alivyoihandle issue pettycash ni vyema zaidi ya mke wa best wa mkwewe. Anyway, ni mtazamo wangu tu.
 
Last edited by a moderator:
Uko sahihi kwa kiwango kikubwa; lakini he has to be smart about it, maana ushauri mwingi alioupewa akiubeba the way ulivyo anaweza bomoa badala ya kujenga. Benefit of doubt ni muhimu, natumaini analielewa hili; na hilo la kuzuia mahusiano kati ya mkewe na friend wake, yaweza bomoa maana ni kumlazimisha achoose betwee two unequal yet important people. Umuhimu wa mume hauwezi kuwa sawa na wa rafiki, na wa rafiki hauwezi kuwa sawa na mume; so he might loose completely au akasababisha uhusiano wao ukawa wa siri na baadaye kwenda another level ambayo mume anaweza akaipanda kwa kumuhisi. Imagine, akimtuhumu kuwa ni bwana wake, tayari anamuwekea wazo au image ya friend kuwa bwana (in bed and all that), na kero (nagging) zikizidi; badala ya mwanzo alivyokua say anapata ushauri tu sasa itaenda kwenye kukumbatia na mambo mengine. Kwa maoni yangu alivyoihandle issue pettycash ni vyema zaidi ya mke wa best wa mkwewe. Anyway, ni mtazamo wangu tu.
Ni kweli mpendwa, kwa ushauri wote aliopokea ni ngumu na haitafaa kuchukua mashauri yote tuliyotoa kama wadau bali atumie mashauri haya kama sehemu/chanzo cha kumfanya awe makini katika kupambanua na mwishowe afanye maamuzi yenye manufaa kwake binafsi, familiya yake na hata jamii inayomzunguka. Kwa nguvu za kibinadamu ni ngumu ila kwa Mungu muumba mbingu, nchi na vyote viijazavyo inawezekana, Mungu amfumbue macho na kumpatia hekima na maarifa ya kutatua hili jambo.
 
Huyo mkeo ulimzibua kotee? Wengine wapenz wetu Kabla ya ndoa tuliwapa kabang......
 
Siku ukijua how to trust ur guts, maisha yanakuwa rahisi japo maamuzi magumu yapo pale pale
 
Back
Top Bottom