Namsaidiaje?

Namsaidiaje?

huyo tiyari jamaa keshamgonga cha muhim hapo chukua time zako.na hizi mambo zko sana kwa watu wanaojidai kuwa wako very close sana na mapatners wa wenzao .
 
Toka tufunge ndoa maisha yetu yamekuwa mazuri na simple sana.
Ni mke tunayeelewana na ni mshkaji wangu sana tu.
Tumepeana uhuru mkubwa sana ila pia una mipaka. Kuna mipaka ya kawaida ambayo mwanajamii
yeyote anaielewa na kuna ambayo si muhimu sana ila tumeamua tu kujiwekea
(Kwa mfano kwa sababu mimi ndo mwenye ex tunayewasiliana bado,
mazungumzo yetu hayaruhusiwi kuwa zaidi ya kujuliana hali).


Basi ana rafiki yake(jst friends) wa toka o'level, na familia zao ziliko jirani na ni family friends.
Huyu jamaa alikuwa close sana na wife enzi hizo ila hawakuwahi kwenda zaidi
(Najua kwa sababu hakuna kabla yangu aliyewahi). Ila ukaribu wao ulikuwa unatisha,
kwa mfano one day walienda beach na friends wengine wa jirani
(mtaani kwao wife walikuwa mambo safi kidogo tofauti na nlipokulia mimi). enzi hizo tunaanza kuwa wachumba
wife kanipigia simu niende na nilipofika jamaa alimkiss kidogo kwenye lips. Nikashtuka sana cku hiyo,
nilipomuuliza akasema ni normal na kweli jamaa alimkiss mdada mwingine ambaye boyfriend wake alikuwepo
hivyo hivyo. Basi nikafunguka kumuambia kuwa mambo hayo mi siyawezi na akanisikia. Wife ni mpole kiasi
na kakulia sehemu yenye maadili mazuri ila uzunguuzungu ulikuwa mwingi hata hivyo baadae tukawezana.


Sasa miaka kadhaa mbele ndo mwezi jana, yeye kaolewa(na mimi) na jamaa ana mke. Sasa juzi kati jamaa katoka
edinburg. Wife alipotoka kazini akaniaga anaenda kuwatembelea. Alipokuja home akaja na laptop,
akaniachia akaenda rum sasa mimi nikawa naishangaa(touch screen) na kuitumia nikasahau hata kumuuliza alipewa zawadi,
ni ya kazini ama alinunua. NIkawa tu naitumia hata wife hakuwa na time nayo tena. Sasa wiki iliyopita nakuja gundua
kuwa wife alivyoenda kwa jamaa(ile mwezi jana) aliacha ndoa yake mashakani baada ya siku chache.


Kiukweli ni kwamba laptop alipewa na jamaa kama zawadi ya kuja, jamaa hela alizopewa kwa safari ya Uskoti si nyingi sana
na alileta zawadi mbili tu! pauni 300 mkufu wa mkewe na laptop pauni 450 for my wife!!!!
Sasa mkewe alivyoambiwa hivyo na mmewe akammind, akaondoka usiku kulala kwa wazazi wa mume. Usuluhishi umefanyika wiki
nzima jamaa analala alone ndo mambo yakawa poa, mke akataka laptop wazazi wakambembeleza amwachie(si wanamjua wife).


Sasa huku kwangu mimi na laptop, laptop na mimi, sina nnalolijua na wife anajua hajajishunghulisha nao anaogopa na
hakuniambia chochote. Hiyo wiki jana sasa mke wa jamaa kaniambia shem nna mazungumzo nawe. Nikapitia kwao(mmewe hayupo)
akaniambia yote. Mimi nikataka kumuuliza wife kwa nini alinificha, nikawazaa nikaingiwa na wasiwasi. Kwanza kwa nini
jamaa amnunulie gift expensive kuliko mkewe?Ile laptop nzuri vile y jamaa asiifanye yake?


Basi na mimi nikaamua kunyamaza. Niakaanza kukumbuka vitu vidogovidogo vilivyokuwa vinanitatiza. Kwanza wiki ile
(mwezi jana) jamaa kaondokewa nyumbani na mkewe alikuwa anaenda sana kazini kwa wife
(Nilishamkuta mara2 wakati nampitia wife na mara ya2 ilikuwa ghafla sana kiasi kwamba kwa mbali ni kama hawakutaka niwakute pamoja).
Mke wangu amekuwa mkimya too much hata siku moja tulikuwa tunatoka kazini kila nikianzisha stori
inakufa niakaamua kunyamaza nimuobserve almanusura apitilize nyumba(alikuwa anaendesha).
Siku moja nilimuacha mke akichat naye sebuleni narudi namkuta anafuta machozi fasta! Nilimbana cku hiyo hadi karibu tugombane.
Ni kazi? hapana, nyumbani? hapana wazazi? hapana nimekuudhi? hapana. Ni hormones? hapani Nikamtaja jamaa aliyechati naye
labda kamuudhi akashtuka kidogo then hapana!Nikamkomalia tukaelekea kugombana ikabidi nimuache.


Sasa waungwana nahisi mke wangu anaanza kufall kwa jamaa(Na jamaa vilevile). Natamani kumuuliza wife lakini
1) Sipendi kuonekana mwanaume mwenye wivu kumuingilia wakati tulishadefine mipaka na hajacross...
2) Na kama wanakuwa wapenzi ni kwa nini miaka yote hiyo wako close wasiwe?(No body was stopping them. Na nnajua hawajawahi kuwa hivyo)
3) Nimekomaa sana kumjali na kumtunza mke wangu na yeye pia vilevile na naamini itakuwa ngumu sana kwake kuvuka mipaka,
lakini nafanyaje sasa kumrudisha wakati moyo wake unaenda huko? How do i rescue her before she breaks her heart?
4) Naombeni mnishauri kwa sababu mtu akimpenda mtu hata nipige mikwara kama kweli wakidhamiria kufanya mi naepushaje?
5) Mliishije/Mnaishije kwenye ndoa zenu kuepuka haya?(mnisaidie second year mimi)
kwa kifupi kutanisha familia ya jamaa na yakwako mu-discuss inaweza kuwapa mwanga ikishindikana washirikishe wazazi wenu.....
 
ahaha Mi nnachoona hapo ni kuwa hamna cheating wala nini..sema uzungu uzungu umezidi..afu we mwenyewe hujui mambo hayo ahahha ndo inabidi ujifunze sasa...dont change the players change the game... anza kumualika huyo mshkaji hapo home makusudi uone wanavokuwa mbele yako ...mwisho utaelewa ni nini..ila kuhusu cheating sio kweli.wangefanya kwanzia kipindi hicho...hai make sense.

Halafu akigundua ni kweli anamkaaaazza????!!
 
Mkuu ni watu wengi sana wanatoka na kazi kuja kufanyia home baada ya masaa, na mimi mwenyewe ni mmojawapo. Na si mara ya kwanza wife kuja na laptop tofauti na yake kuja kufanyia kazi. Sikutilia maanani kwa sababu haiwezekani nimuulize laptop ni yako ama ya kazini kila mara nionapo mpya.
Halafu mke wangu huwa ananiambia vitu vingi sana kwa hiyo saa nyingine huhitaji kuuliza anasema. Sasa mtu kaingia ndani tumeongea kidogo kaniachia vitu vyake kaingia rum. Namuulizaje?


Roho mbaya tu inakusumbua teacher...

Kwani hukuona mshikaji anasema kuwa aliletewa Laptop bomba akawa anachezea??

Duuuuuuuuuuuuu,......wengine hata ukiona pant mpya unauliza tu kiungwana huku mdau hastuki mkewe kupewa GBP 450 (Tsh, 1.15m)!!

Babu DC!!
 
Akutane na manyoya mara ngapi??

Hivi kweli mume au mke analeta kitu kipya kama Laptop na haulizwi kaipata wapi??

Nahisi kama kuna ndoa ambazo watu wanaogopana kama maafande!

Babu DC!!


Babu umeonaee... na hiyo Justfriend kama vile anaifuga sanaaa, ndio maana anashindwa hata kufanya maamuzi muhimu ya kulinda ndoa yake. Eti wanakiss kwenye lips, zawadi za madolar.. What!!!!!!
 
Huo ujinga uliulea mwenyewe toka mwanzo,we mwafrika utaruhusu vp mkeo awe na ukaribu na rafiki wake wa kiume namna hyo?
Nimeukuta mkuu na kuna vitu walikuwa wanafanya nikakataza kama nilivyosema hapo awali. Na pia baada ya ndoa obviously ukaribu ulipungua. Nilicholea ni nn?
 
Mkuu ni watu wengi sana wanatoka na kazi kuja kufanyia home baada ya masaa, na mimi mwenyewe ni mmojawapo. Na si mara ya kwanza wife kuja na laptop tofauti na yake kuja kufanyia kazi. Sikutilia maanani kwa sababu haiwezekani nimuulize laptop ni yako ama ya kazini kila mara nionapo mpya.
Halafu mke wangu huwa ananiambia vitu vingi sana kwa hiyo saa nyingine huhitaji kuuliza anasema. Sasa mtu kaingia ndani tumeongea kidogo kaniachia vitu vyake kaingia rum. Namuulizaje?

Mkuu PetCash,

Hapa hatuongei nadharia bali yale tunayokutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku.

Ila kama ndiyo maisha uliyozoea kuishi, kiasi kwamba huwezi kuuliza mke wako akibadili vitu muhimu kama laptop, basi jua kuwa wewe ndiye umetoa mwanya wa kufanyiwa yanayokukuta. Na huna sababu ya msingi kulalamika!

Pia nakuomba usome tena hiyo kauli yako hapo chini,


Wife alipotoka kazini akaniaga anaenda kuwatembelea. Alipokuja home akaja na laptop,
akaniachia akaenda rum sasa mimi nikawa naishangaa(touch screen) na kuitumia nikasahau hata kumuuliza alipewa zawadi,
ni ya kazini ama alinunua. NIkawa tu naitumia hata wife hakuwa na time nayo tena. Sasa wiki iliyopita nakuja gundua
kuwa wife alivyoenda kwa jamaa(ile mwezi jana) aliacha ndoa yake mashakani baada ya siku chache.



Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Nimeukuta mkuu na kuna vitu walikuwa wanafanya nikakataza kama nilivyosema hapo awali. Na pia baada ya ndoa obviously ukaribu ulipungua. Nilicholea ni nn?

Inaonekana unataka kuwa defensive zaidi badala ya kusikiliza maoni ya watu, ambayo yanatokana na maelezo yako. Badala yake umeanza kuwa mkali. Nakushauri ujibu maswali ya wadau ili wakupe ushauri unaoeleweka.

Kwa maoni ya wengi, it seems you have been grossly irresponsible!!

Babu DC!!
 
Kaka mkubwa hii ndoa yako umeivunja kwa ukosefu wako kuona mbali...
Ukiwa mwanandoa lazima uwe selfish, hakuna mtu anapaswa kuchezea mkeo...kuna mistari huwa inachorwa na hakuna mtu anapaswa kuvuka.
Wanawake siku zote hupenda kuwa na mtu ambaye anajua kulinda...
Weka kikao kizito kati yako wewe, mkeo, huyo shemeji yako na mkewe aliyetengana naye...
Kiwe kikao kizito kweli kama cha G8...na agenda ya kikao iwe ni wewe kueleza msimamo na terms zako...zaidi weka wazi boundaries.
Mpige kabisa marufuku huyo bwana kuingilia ndoa yako au lah muulize mkeo anachagua nani kati yenu aseme wazi...

'Miluzi mingi siku zote humpoteza mbwa'...ndivyo ambavyo mkeo anakaribia kupotea hivyo maana miluzi imemzidi masikioni mwake.
fuata huu ushauri ,african culture should remain african culture haiwezekani mkeo leo hii amlilie mtu mwingine kimapenzi halafu useme ni uzungu,huo ni ujinga
 
daaa...
wewe kweli unahitaji ushauri kabla hujakutana na MANYOYA... HorsePower Kaunga gfsonwin
babu @Aspirin ..mkuje huku kushauri jamani.. jahazi lisije zama.

Ushauri wangu ni mchungu sana, sijui kama atauweza ....
Anapaswa kumpa option mkewe achague kati ya rafiki na mume, nani anapenda kuendelea naye ...
Nahisi urafiki wao umevuka mipaka!!!
 
Rafiki pole sana kwa mkasa mzito uliojaa changamoto, ubaya ni kwamba ulikosea tangu mwanzo wa uchumba kwa ku-pretend kukubaliana na uzungu wakati unakuumiza, mchumbako anapigwa kiss mdomoni unatulia eti kwa sababu kuna mwingine alipigwa mchumbake akiwapo naye akakausha, kuwa na msimamo madhubuti palipo sahihi hata kama watu wote watakupinga ama utaonekana mshamba.


Wewe unahisi hakuvuka mipaka ila mimi naona kishavuka bila wewe kujua, inawezekana hawakuwa na mahusiano hapo awali ila hii haitozuia wao kuwa na mahusiano sasa, tena kiukweli ni rahisi kwa baadhi ya wanawake/wanaume kuwa na mahusiano wa watu waliokuwa karibu nao baada ya kuingia kwenye ndoa kwa sababu ni vigumu wenzi wao kugundua mahusiano hayo haramu na hiki ndicho kinachokutokea wewe.

Angalia matukio haya: Mchumba anapigwa busu mbele yako unapuuza, mkeo anapewa zawadi za gharama hujui aliyempa na wala huulizi ila unapuuza, mkeo anatembelewa na so called friend mala kadhaa na ukahisi hawakutaka uwakute ila ukapuuza, mkeo anachati na so called friend kisha unamkuta analia na unamuuliza anakujibu hamna kitu nawe unapuuza, ameyakoroga kwa so called friend mpaka mke kaondoka hata hakukuambia we bado unaona kawaida na hajavuka mipaka. Kaka acha kuwa mpuuzi kwa kupuzia mambo ya msingi.

Chakufanya: Chunguza nyendo zao, mkaribishe raki ya mkeo nyumbani kwako kuwa makini ku-trace mabadiliko yoyote au kama kuna hisia zozote maana mapenzi huwa hayajifichi, ukisha baini kuwa hao watu ni wapenzi ama wanaelekea kuwa wapenzi. Nakuomba simama kama mwanaume kwa mkeo mwambie madhara aliyosababisha kwenye ndoa ya rafikiye na usingependa kuona kitu hicho kinaendelea, yeye ni mkeo na si mke wa mtu mwingine.

Kwakuwa urafiki wao umeshindwa kusitawisha ndoa za pande zote mbili badala yake unabomoa basi hamna haja ya urafiki huo kuwepo, uvunje urafiki huo kwa namna yoyote wabaki tu wanaheshimiana kama watu wengine wa kawaida hapo mtaani, weka masharti mapya kwa mkeo kumbuka hiyo ni ndoa yako tena bado changa mno hata vikwazo bado hamjapitia, hivyo usipo simama kidete kama mwanaume hiyo ndoa itakusumbua. Ni kweli kama ulivyosema kuwa wakiamua kuwa wapenzi ni ngumu kuzuia ila ni bora uonyeshe kuwa nawewe kama mwanaume umeipigania ndoa yako, kama imeshindikana kuzuia wao kuwa wapenzi basi ni bora wafanye kwa kuipa sana kuliko kukufanya zuzu.

Ukweli ni kwamba safari ya ndoa yako bado ni ndefu sana ambapo utapitia changamoto nyingi sana ila sidhani kama kuna changamoto ngumu katika maisha kama ya wanandoa kutokuwa na mwelekeo na mtazamo mmoja juu ya maisha ya ndoa (alignment) hata hivyo hote unaweza pambana na ukashindwa cha msingi muombe sana Mungu muweza wa yote kwanza akuonyeshe kiza kilichoka mbele yako na nyuma ya pazia la ndoa yako kisha aitakase, mpango wa Mungu ni kuifanya ndoa ifurahiwe na wanandoa wote siku zote za maisha yao ila shetani anafanya kinyume chake. Mungu akutie nguvu na akubariki.
 
Nipo mwalimu gfsonwin,
Dah! Mkuu hebu punguza jazba kidogo. I am a man in my home, na ningeweza kukupa mfano jinsi nnavyohandle mambo.
Halafu hii ni unhandled issue. Ningelianzisha wakati wa laptop then nisingeona kina cha tatizo lenyewe, na hapa nnawaza how to handle hii issue with minimum casualty. Nikimind akaenda kwao then nikaweka stop kwenye huo urafiki, kama kweli wamependana, ndo ntakuwa nimewazuia wasifanye? Do i know they are doing it?
Nikimpa talaka ndo solution?

BTW: Haiwezekani kuwa alifoji kuwa virgin kwa sababu hakuwahi kuniambia yuko hivyo na sikutegemea alikuwa hivyo, ilitokea tu nikamkuta hivyo.

Halafu sioni kuwa kumgombeza mke kila afanyapo kosa ndiyo hulka za kiume, na haiwezekani niwe less of a man kwa kufanya mambo yote sawa ila hilo. Hao wanaokuwa wakali ndo ndoa zinadumu?
bestiee nisamehe kwa kuwa mkali sana manake sikutegemea kabisa mtu kama wewe jamb hili likushinde.

ngoja nikwambie principle moja ya kuish na mke, lazima uweke mipaka ambayo wewe unaitimiza kwanza na pia yeye anapaswa kuitimiza.

unapoona wewe huna mahusiano yaletayo maumivu kwa mkeo basi yeye naye hapaswi kuwa nayo na ukiona yapo mweleze wazi akikaidi mrudishe kwanza kwao akajifunze adabu. full stop. mbona ndoa sio ngumu ikiwa baba uko firm??
 
Roho mbaya tu inakusumbua teacher...

Kwani hukuona mshikaji anasema kuwa aliletewa Laptop bomba akawa anachezea??

Duuuuuuuuuuuuu,......wengine hata ukiona pant mpya unauliza tu kiungwana huku mdau hastuki mkewe kupewa GBP 450 (Tsh, 1.15m)!!

Babu DC!!
babuu mwanume unabaki kubonyeza laptop 450gbp mwenzio anakubonyezea mkeo.

hii haina tofauti na kwenda na mtoto gesti ukamwacha nje kwenye kiti na mapipi mengiii wewe ukaingia ndani kumaliza yako. sasa mtoto atachezanazoo mpaka achoke wee ushamalizamambo yako.

hahaha!!!!!!!!! nacheka sana eti mwanume unahadaiwa kama mtoto...
 
Kaka mkubwa hii ndoa yako umeivunja kwa ukosefu wako kuona mbali...
Ukiwa mwanandoa lazima uwe selfish, hakuna mtu anapaswa kuchezea mkeo...kuna mistari huwa inachorwa na hakuna mtu anapaswa kuvuka.
Wanawake siku zote hupenda kuwa na mtu ambaye anajua kulinda...
Weka kikao kizito kati yako wewe, mkeo, huyo shemeji yako na mkewe aliyetengana naye...
Kiwe kikao kizito kweli kama cha G8...na agenda ya kikao iwe ni wewe kueleza msimamo na terms zako...zaidi weka wazi boundaries.
Mpige kabisa marufuku huyo bwana kuingilia ndoa yako au lah muulize mkeo anachagua nani kati yenu aseme wazi...

'Miluzi mingi siku zote humpoteza mbwa'...ndivyo ambavyo mkeo anakaribia kupotea hivyo maana miluzi imemzidi masikioni mwake.

Mpwa umeanza lini kuitisha vikao vya kuweka terms za ndoa yako.?????
Ni lini mimi na wewe tumepitisha mswada kwamba wake zetu wakiwa wajinga eti tuitishe vikao ili aibu iwe yetu????
Mpwa nataka unijibu ni lini mimi na wewe tumekuwa wadhaifu wa kutaka mamluki kuendesha jambo la black and white??!!!
Yaaani tulivyokatazwa kupiga wanawake jandoni we ukajua hata msimamo huwezi kiweka mpaka vikao????!!!!
Usiniambie lile agano la kuwa hitler mambo yanapotaka kuwa magumu wewe uliliacha kule jandoni!!!!

Yaani wewe mpwa watu8 ukinnita mimi nije na balls hapo kwako uje kuniambia hii maneno mbele ya huyo "mume mwenzio" I guarantee you human rights will be violated and possibly kosa la jinai.
 
Mimi naona bado unalazimika kuongea naye, huenda kinachomsumbua na kumliza ni kuchangia (indirectly) kuharibu ndoa ya best friend wake.

Mara nyingi bond ya best friend ni zaidi ya ndugu au spouse hivyo huyo mkaka anapata comfort kwa mkeo na mkeo anajitahidi kumfariji, kumshauri jinsi ya kurudisha mahusiano yake na mkewe.

kwanini hakukuambia? Nafikiri somehow deep down in her heart anajua unastruggle kuukubali huo 'uzungu' wa ubest friend hivyo alikuspare matatizo au fikra negative kwa kutokukuambia.

Nini ufanye?
Be yourself and confront her, acha kupretend ugentleman au uzungu ambao haunao; mwambie what you are speculating na hata ikiwezeka ifanye isound worse than it is, ili afunguke na akuambie kinachoendelea. By the tone of her voice, a look into her eyes etc utajua ukweli ni upi na uongo ni upi.

Pole sana PetCash
 
Last edited by a moderator:
Hiviiii, kungekuwa na uhusiano wa usiri jamaa angempa zawadi ya laptop best friend wake mbele ya mkewe? Si angekuwa more careful basi angedanganya kuwa alimuagiza (kwa kumpa pesa kabla)?

Halafu what is more romantic, zawadi ya laptop au mkufu?

Sioni mapungufu ya 'umume' wa PetCash kwa kuihandle issue the way alivyoihandle, ila ili apate tulizo he has to spell all his worries kwa mkewe na labda wadiscuss terms zingine ili awe na amani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom