Nampongeza Zari The Boss kwenye hili

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,557
18,881
Hivi karibuni Mwanamama zari the boss lady ametoa povu kubwa kwa baadhi ya watanzania wanaomfuatilia Sana maisha yake ingawa Zari ana mapungufu yake binafsi lakini kwa Hili povu aliyotoa nimemuunga mkono kwa asilimia 100 Na hii imekuja baada ya tetesi ya yeye kurudiana na diamond lakini pia kwa kuzungumziwa vibaya mwanaye Tiffah nimnukuu baadhi ya maneno aliyoongea

"Nikiwa ninaambiwa Niko desperate Mara nawatumia watoto kurudiana na diamond hivi nikirudiana nae Nini kinachofanya mteseke? Kuna wengine wana nionea wivu kwa Sababu me ni rich wakati wao ni masikini wanauza nyanya vitunguu uko, me ni mwanamke mzuri wakati wao wanasura mbaya,una kuta mtu ana vocha ya 100 anawasha hotspot kwa wenzake 7 wanalala kwenye godoro moja alafu wanakuja kunitukana Mimi ambaye ninatoka kwangu Nina gari Kali naenda ofisini"

Akaongeza pia sijawahi kuona mtu mwenye Mafanikio anamchukia mtu mwingine mwenye Mafanikio Mara nyingi watu wenye wivu ambao Ni masikini ndio wanachukiwa watu matajiri Leo hii siwezi Mimi zari kutoka Africa eti nimchukie Oprah wa Marekani hata nikimchukia ninapata faida gani? Kwani itamzuia yeye asipate Mafanikio? Aliyepewa kapewa tu watanzania wanatakiwa wawe inspired badala ya kuwa na chuki.

NB: Hili suala la wivu alilolizungumzia Zari ndio tabia halisi walionalo Watanzania Jana wakati nimepanda daladala naenda sehemu fulani mbele ya daladala niliyopanda kulikuwa na mark x dereva wa hiyo gari alikuwa anaendesha taratibu dereva wa daladala niliyopanda akasema Hawa wakishapata vigari vyao vya mkopo wanatusumbua Sana barabarani imagine unakuta huyo dereva hata tu baskeli Hana alafu anaongea kauli Kama hizo sijui watanzania tuna shida gani? sometimes ndo maana watu hawapati Mafanikio kutokana na hizi tabia.

Numbisa Leo naona meno nje
 
Back
Top Bottom