Nampenda sana Nargis Mohamed

Sio kihivyo, ni mtu ninayetumia muda mwingi kujua vitu vingi kadiri ubongo wangu unavyoweza...

Huku mbele sijawahi kuwa mnazi wa mashindano ya ulimbwende...

Niliacha kufuatilia mwaka 2015 hapo aliposhinda Lilian Kamazima, baada ya hapo kuna mamiss ninayemjua ni kama Queen Makune tu, wengine siwajui hata mmoja...

Zamani za Lundenga na wale wahindi wa White Sands walijua kuyaweka sawa hayo mashindano, ashukuriwe kitu kingine cha zamani cheusi mangala Basila Mwanukuzi kwa kuyaokoa mashindano hayo...
Nimeelewa mkuu
 
Huyu msichana na sasa mwanamama wa miaka 2003 miss Tanzania nampenda sana. Sinaga muda mwingi kumtazama ila angejua wengi tunavyovutiwa naye basi angefungua pazia.View attachment 2963632View attachment 2963633

Si upendo wa kiuchafuchafu ngonoana hapana. Nampenda alivyo tuuu hata sijui alikosaga vipi kuwa miss namba moja miaka ile.
Hivi bado anaishi?
 
....... kwakweli lundenga alistaafu na miss Tz yake, toka aachie hayajawahi kuwa na mvuto, huwa nadhani alistaafu kutokana na mamiss wa miaka ya 2000s kuendekeza skendo kutokana na umaarufu wanaopata.......hivi huyo wa 95 si ndo alishika taji la miss Tz akiwa form 3!?.......
 
Umeanza kufuatilia Miss TZ mwaka gani?

Mimi tangu enzi za Aina Maeda, wakati huo akichuana kindakindaki na Tabasamu Ngongoseko...

Kati ya wachuchu wote buana, kuna kitu kilikuwa kinaitwa Lisa Jensen...
Mpambano mkali wa ma miss ilikua Miss Ilala..Mbiki Msumi na Hoyce Temu....kisha ukahamia tena Miss Tanzania..Mbiki tena na Hoyce Temu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom