Nampenda sana lakini ana mke

Nampenda sana lakini ana mke

Miaka 21 ushatembea na mume wa mtu.... Tafuta shule usome au fani yoyote usome wewe bado ni Mdogo usigombanie wanaume kwa sasa ....work hard
 
saizi umemfahamu mke mmoja endelea kumganda akuoe ila utakapokuja kushtuka we ni mke wa 6 ndio akili itakusogea
 
Achana na Mume wa Mtu.

Epuka matatizo yanayohepukika/yanayokwepeka.

Umri wako bado unakuruhusu sana kuendelea na Masomo, na mambo mengine mengi ya kimaendeleo.

Jamaa, anataka kukutumia. Na siku ya siku likitokea la kutokea (Ujauzito) ujue zigo litakuwa lako, atakutelekeza.

Kaa mbali na Mume wa Mtu.

Kama angekuwa na Mapenzi ya kweli na wewe, hasingekuficha ya kuwa ana Mke.

Macho unayo, na Masikio unayo.

Uamuzi ni wako
 
Huyo amefaulu kigezo cha uzoefu wa ndoa. Heri zimwi ulijualo. Usipoangalia utaenda kudanganywa tena. aidha maneno yngu sio sheria
 
Endelea kuzini tu maana hushituki, yaani hata huo mpango wa Mola wa kumuumbua huyo jamaa ili ujue ana mke, bado hujauona? ACHA kupenda kwa hisia tu bila kutumia akili angalau kidogo.
 
Hawa ndio tukiwatongoza wanajibu nina mchumba wa kinioa kumbe mchumba aliyenaye ni mchumba hewa,akifika 30yrs anaanza kutapatapa kama samaki aliyetolewa kwenye maji?
 
Ungekuwa hutaki kuwa mke wa pili, ungeshamuacha siku uliyojua.

Uamuzi ni wako na ya mbeleni utajijua.
 
Habari zenu, naitwa Issabella natokea Tanga nina umri wa miaka 21, Nina boyfriend ambae nipo naye takribani miaka miwili sasa, katika mahusiano yetu hajawahi kuniambia ana mke wala watoto na hajawahi kunionyesha dalili yeyote ile kama ana mke.

Lakini siku kadhaa niliambiwa na rafiki yake kuwa mtu ambaye nipo naye ni mume wa mtu, na nikweli nilithibitisha nikaona kweli ana mke, nimemuuliza amekubali na ameniambia hajaniambia kwasababu aliogopa nitamuacha lakini bado ananipenda na atanioa......ushauri kwenu nifanyaje?

Nimuache au niendelee naye? Kiukweli mimi pia bado nampenda sana lakini sipo tayari niolewe na mtu ambaye ni mume wa mtu. Naombeni ushauri wenu plz

Unataka tusemeje??
Masingo tumejaa mnakaa na waliooa...
your days are numbered!
 
Habari zenu, naitwa Issabella natokea Tanga nina umri wa miaka 21, Nina boyfriend ambae nipo naye takribani miaka miwili sasa, katika mahusiano yetu hajawahi kuniambia ana mke wala watoto na hajawahi kunionyesha dalili yeyote ile kama ana mke.

Lakini siku kadhaa niliambiwa na rafiki yake kuwa mtu ambaye nipo naye ni mume wa mtu, na nikweli nilithibitisha nikaona kweli ana mke, nimemuuliza amekubali na ameniambia hajaniambia kwasababu aliogopa nitamuacha lakini bado ananipenda na atanioa......ushauri kwenu nifanyaje?

Nimuache au niendelee naye? Kiukweli mimi pia bado nampenda sana lakini sipo tayari niolewe na mtu ambaye ni mume wa mtu. Naombeni ushauri wenu plz
Hyo prfl Pc ni ww??
 
isabela umempendea ninI huyo jamaa?
Kwanini unatamani Mali ya mwenzio tuambie ukweli tu kwamba we ulikua mchepuko ila sasa unataka kupindua ndoa ya mwenzio?
umesema hutaki kuolewa na mume wa mtu na wewe umekazania kumpenda mume wa mtu kwaiyo unataka tukushauri umwambie aachane na mke wake ili akuoe wewe si ndio maanaaake!
miaka 21 we bado mdogo sana hebu tafuta wa kwako peke ako ukishindw kumpata karibu PM.
 
Back
Top Bottom