Pole kwa mazito yaliyo kukuta, hizo ni mmoja ya changamoto katika suala zima la mapenzi.
Kwa mtazamo na ushauri wangu kwa ujumla,
Haijalishi ni kiasi gani umempenda moyoni, lakini ni vyema ukasahau yaliyo kukuta na kuendelea na maisha yako,
Na isitoshe kwa umri uliyokuwa nayo ( 21 ) bado ni mdogo, hivyo unahitaji ufanye mambo yako ya maana na ni vyema ukaolewa ukiwa na miaka ( 25 ) - ( 35 ) hicho ni kipindi ambacho mwanamke amekomaa kiakili na kuweza kufanya maamuzi sahihi katika mambo yake, na hata kuwa imara kwenye ndoa na masuala yote ya uzazi.
Hii inaonesha mwanaume uliye nae kwa sasa hakupendi, kwa sababu yeye tayari ana mke wake na watoto, kutokana na ile tamaa ya ngono, ameona akuchukue wewe ikiwa bado mdogo, kifupi amekufanya hawara wake, sidhani kama anayo mapenzi ya dhati kwako, zaidi ya kutaka kukuchezea tu!!!
Cha kufanya, kaa umueleze ukweli kuwa haupo tayari kuolewa nae, wala kuendelea nae kimapenzi, ila usimchukie ongea nae, Cheka nae, kama kawaida zungumzeni vizuri muwe kama marafiki na si wapenzi/ wapendanao.
Na jaribu kuwa mwangalifu baada ya kuchukua uamuzi wa kumuacha maana anaweza akakulaghai tena kwa maneno mazuri, na kujifanya anahitaji huruma yako kusudi mrudiane, angalia hili, sisima imara, jipe moyo yote yanawezekana kilichobaki ni kuchukua maamuzi sahihi,
Najua umesema bado unampenda ila hutaki kuolewa nae,
Hii kauli inaonesha ni jinsi gani bado upo kwenye kundi la vijana, nikiwa na maana ya kwamba, ni akili ya ujana bado ila kadri unavyokuwa na kuoata akili ndivyo utakavyo elewa kuwa ulikuwa unakosea kuongea hiyo kauli,