Ishmael2012
Member
- May 23, 2014
- 58
- 42
Habari zenu wadau poleni na majukumu ya kujenga taifa, kama thead inavojieleza hapo juu, mm nikijana wa miaka 24 ni miezi miwili sasa nipo kwenye mahusiano na mwanamke ambae tulikutana kwenye eneo langu la kazi nilimpenda sana sikusita kumweleza hisia zangu japo alikuwa mbishi sana kunikubali hatimaye akani kubalia. Nikaanza kubanjuka nae kama kawaida ijapokuwa hapo mwanzo alinieleza kabisa kuwa ana mtoto mmoja namm nikakubaliana nae kuwa hakuna shida yoyote, sasa leo wakati tuko pamoja alionekana kukosa amani kuliko siku zote ndipo nikamuuliza nini tatizo akasema kuna kitu sikukwambia kuwa sina mtoto mmoja ila ninao wawili , akaniambia kuwa ndio maana alikuwa hataki kupenda tena mwanaume kutokana na mume aliekua nae kumfanyia ukatili ikiwemo kumpiga pia alimnyang'anya watoto wote wawili mmoja akiwa ananyonya kabisa,kwakweli wadau mpaka nimelia na kulia pia ananiambia alikunywa vidonge ili afe kwani hakuona umuhimu wa kuishi imenibidi nimsihi asijaribu kujiua kwani nampenda kwelii namimi lengo langu ilikuwa kumuoa ila sasa ana watoto wawili namm sina hata mtoto mmoja namm nilimuahidi kuwa ningemlea huyo mtoto. Naombeni msaada wa mawazo nifanyeje kwani nipo njia panda
Ahsanteni
Ahsanteni