Nampenda lakini ana watoto watatu ushauri wenu please

Nampenda lakini ana watoto watatu ushauri wenu please

Habari zenu wadau poleni na majukumu ya kujenga taifa, kama thead inavojieleza hapo juu, mm nikijana wa miaka 24 ni miezi miwili sasa nipo kwenye mahusiano na mwanamke ambae tulikutana kwenye eneo langu la kazi nilimpenda sana sikusita kumweleza hisia zangu japo alikuwa mbishi sana kunikubali hatimaye akani kubalia. Nikaanza kubanjuka nae kama kawaida ijapokuwa hapo mwanzo alinieleza kabisa kuwa ana mtoto mmoja namm nikakubaliana nae kuwa hakuna shida yoyote, sasa leo wakati tuko pamoja alionekana kukosa amani kuliko siku zote ndipo nikamuuliza nini tatizo akasema kuna kitu sikukwambia kuwa sina mtoto mmoja ila ninao wawili , akaniambia kuwa ndio maana alikuwa hataki kupenda tena mwanaume kutokana na mume aliekua nae kumfanyia ukatili ikiwemo kumpiga pia alimnyang'anya watoto wote wawili mmoja akiwa ananyonya kabisa,kwakweli wadau mpaka nimelia na kulia pia ananiambia alikunywa vidonge ili afe kwani hakuona umuhimu wa kuishi imenibidi nimsihi asijaribu kujiua kwani nampenda kwelii namimi lengo langu ilikuwa kumuoa ila sasa ana watoto wawili namm sina hata mtoto mmoja namm nilimuahidi kuwa ningemlea huyo mtoto. Naombeni msaada wa mawazo nifanyeje kwani nipo njia panda
Ahsanteni
Hili ni la wazee wa kimila
 
Owaaaaa mjomba.Mimi wangu alikuwa NA watat kila moja NA baba take lakin tunaish nami kaniongezea watat nunafamulia ya watoto sita tunapiga kaz NA mama huku sala mbele kama tai.mungu anasaidia watoto watano wanasoma tena siyo kayumba.malengoj braza.tena huyo alinyanganywa ? Oa kaka huyo ndo mwanamke.love them cherish with them maisha saaaafiii na penzi lenu litakuwa saaaaaafiiii
 
bro ndoa sio mchezo kama unavyofikiria,,me mwenyewe bado sijaoa lakini nime-experience baadhi ya mambo mbalimbali ya ndoa kutoka kwa ndugu zangu na watu wangu wa karibu. nakushauri jaribu kukaa chini ufanye uchunguzi zaidi kuhusu huyo mwanamke.kumbuka kuna mambo mawili.kulia na kujutia ndoa au kufurahia ndoa. miezi miwili tu halafu una mpango wa kumuoa!!? then anakuambia tena ana mtoto mwingine?kama ulimwambia kwa dhati unampenda na una mpango wa kumuoa,basi nayeye angekuweka wazi kuhusu maisha yake na hao watoto wake,na sio kufichaficha mambo.sijashauri umwache ila inahitaji utulize akili fanya uchunguzi zaidi usije ukatumbukia shimoni.
 
Inbox kuna mafuriko, tuendelee hapa hapa[emoji3] [emoji3]
😀....usiogope mafuriko, hata Lowasa alikuwa nayo lakini hayakuwa na madhara kwa chaguzi.
Hao watoto wana miaka mingapi?....wana baba tofauti tofauti au ni mmoja?
 
Huyo mwanamke mshikilie sana hao watoto wanaweza kukusaidia kuliko hata ulio wazaa wewe kama ana mapenzi na wewe
 
Mkuu achana nae huyo duuh ana tukale wapi wawili haaa...! maisha yamekuwa magumu sana achana na majukumu si yalazima.
 
Kama umejiridhisha watoto sio tatizo
Ila jipange muwe na msimamo mmoja msije yumbishwa na ndugu na watoto Walee wapende kama wanao kabisa hutajutia


Ila ukiwatenga tuuu kuna kitu wanakuwa wanakijenga kichwani
Wakiwa wakubwa wakubwa watawasumbueni
 
Najua hutokosa maneno ya kuwa kwanini unaoa ambaye ana watoto na si ambaye hana watoto kutoka familia yako na hata marafiki.Cha muhimu ni kuwa huyo mwanamke anatakiwa aone thamani uliompa kwa kumuoa akiwa na hiyo status maana kawaida yao ni kuwa ukishaweka ndani anasahau na anakuanzishia mziki,hapo ndipo utakapolia na kusaga meno.Muhimu anatakiwa alielewe hilo hata kabla hamjafunga ndoa.
 
Mtoto wako ndio atakua ndugu wa wanawe, cha msingi fuata Moyo wako unasemaje ukiridhika weka ndani
 
Back
Top Bottom