Nampenda ila wameshamjaza maneno

Nampenda ila wameshamjaza maneno

Pelham 1

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
548
Reaction score
100
Habari zenu Wadau,

Nampenzi wangu ambae ni mpangaji kwenye nyumba ya Mama yangu ingawa mimi siishi hapo, tuna miezi 3 mpaka sasa katika mahusiano yetu, Upande wa ndugu zangu naochangia mama wapo vizuri kimaisha ila kwa kinvuli chao nami huonekana hivyo ingawa ni tofauti, Nikamweleza mpenzi wangu mtarajiwa hali halisi ya maisha yangu ila nilimficha ile code ya kinvuli cha ndugu zangu kinachofanya nionekane na mimi nipo vizuri kimaisha.

Miezi yote 3 mpaka sasa sijatembea nae tukiahidina mpaka tufunge ndoa, Nikiwa nachumguza kumbe nae pia alikuwa akinichunguza ndipo akapewa taariifa na wadau wanaonijua vizuri kama mi nimchovu tu nabebwa na kinvuli cha ndugu zangu! hivi kimenuka huku najaribu kumtuliza mpenzi wangu na kumuelewesha sababu ya kumficha ilikuwa nikupata uhakika kama kweli ananipenda ama alikuwa na yeye anajitega kupitia kivuli cha ndugu zangu kama kuna neema.

Naombeni ushauri nifanyeje? naona ameanza na kuniwekea pozi sasa hv napomuita tofauti na mwanzo alikuwa anapigia simu nikimuita fasta anakuja.
Kweli ndoa za siku hizi tusipoangalia tutavua chura badala ya samaki.

Naombe ushauri
 
Thread za muda huwa na ukweli fulani,..

Pole wee siku hizi wanaume mnajiaminisha kwamba pesa ni muhimu mnaishia kupretend,
mwisho wa siku mtu anapokuja kugundua ukweli anakutupilia mbali kwa sababu anaona umeshindwa kujiamini na kuwa mkweli..
Acheni kufake uhalisia wa maisha yenu.
 
Haha kijana ubaya wa kufake ndo hapo sasa anapokuja kugundua kumbe yote uliyokuwa ukimwambia ni uongo. Hakuna mtu asiyependwa kudanganywa mathalani mwanamke. If you lie, just be smart at lieing, na udanganye kwa kitu ambacho baada ya muda mfupi kile kitu ulichodanganya unakifanya kuwa kweli kwakuweka juhudi zote kukitimiza hata baadae kikidhihirika anajiridhisha mwenyewe kwa macho yake.
Kwa kweli hapo pameharibika na inahitaji utumie nguvu ya ziada kumrudisha mstalini kama zamani.
 
Kama unaishi kwa kutegemea ndugu na umeridhika na hali hiyo, basi ni haki huyo mpenzio kukupiga chini...
 
huwa natafakari haya mambo, sipati majibu, toka sekondari kuna watu walikuwa wanaazima suruali, buti, tisheti ili aonekane bora kwa galfrnd wake, daah....haisee hii nawashauri watu wote wasijaribu kozi ni aibu, mimi sijawahi kupretend sanasana huwa najishusha ili ukijakugundua ukweli unabaki mdomo wazi.
 
achana nae. hilo ni tatizo mbeleni.
tafuta anayekupenda for who you are and not what you are.
na ww usiweke uki vuli.
 
Its always good to be yourself, anaekupenda akupende for who you are.
 
Mtu unataka kumuoa halafi unamfanya aamini vitu ambavyo havipo.
hata kama hakukupendea pesa lakini kwa hilo ulilofanya atakudharau tu, na vilevile atakuamini vipi huko mbeleni kwenye huo uhusiano au ndoa.
 
Huyo hakukupenda wewe...alimpenda yule wewe wa nadharia uliomtengenezea kichwani na moyoni mwake.
Umeshaharibu...move on ila next time ukitaka serious relationship...Be yourself..!!
 
Habari zenu Wadau:
Naombe ushauri:
Nampenzi wangu ambae ni mpangaji kwny nyumba ya Mama yangu ingawa mi siishi hapo, tuna miezi 3 mpaka sasa ktk mahusiano yetu, Upande wa ndugu zangu naochangia mama wapo vizuri kimaisha ila kwa kinvuli chao nami huonekana hivyo ingawa ni tofauti, Nikamweleza mpenzi wangu mtarajiwa hali halisi ya maisha yangu ila nilimficha ile code ya kinvuli cha ndugu zangu kinachofanya nionekane na mimi nipo vizuri kimaisha, Miezi yote 3 mpaka sasa sijatembea nae tukiahidina mpaka tufunge ndoa, Nikiwa nachumguza kumbe nae pia alikuwa akinichunguza ndipo akapewa taariifa na wadau wanaonijua vizuri kama mi nimchovu tu nabebwa na kivuvu cha ndugu zangu!! hivi kimenuka huku najaribu kumtuliza mpenzi wangu na kumuelewesha sababu ya kumficha ilikuwa nikupata uhakika kama kweli ananipenda ama alikuwa na yeye anajitega kupitia kivuli cha ndugu zangu kama kuna neemaaa...
Naombeni ushauri nifanyeje: naona ameanza na kuniwekea pozi sasa hv napomuita tofauti na mwanzo alikuwa anapigia simu nikimuita fasta anakuja!!!
Kweli ndoa za siku hizi tusipoangalia tutavua chura badala ya samaki!!!

Piga kazi uwe na hela zako hcho kivul cha ndugu zako kitumie kupata mtaji wako binafsi vingnevyo MADEM WAZURI UTAISHIA KUWAITA SHEMU!
 
na wewe kwa nini ulijiweka kwenye nafasi ya wenye nao wakati sio?

kua kama ulivo upate atakaekupenda kama ulivo..usiigize maisha ambayo hauna
 
Labda niseme hivi:

Kwanza, Inaonyesha hujiamini kabisa, kwa maana hakukuwa na sababu yeyote ya msingi kutumia uwezo wa ndugu zako kujikweza au kujifanya unazo, ni vyema zaidi mtu akupende jinsi ulivyo maana katika hali hii, hata kama mapenzi yenu yatakuja kuendelea basi utakuwa umejiwekea ka dosari ka kuonekana muongo!

Lakini, on the other side, kama huyo binti atakumwaga au kukupiga chini kwa sababu ya hali yako ya uchumi, basi itakuwa huyo si wife material kwako maana anatanguliza maslahi zaidi kuliko upendo. Hii itakuwa imekusaidia kumuacha mapema na kutafuta wengine maana baadaye angekuja kukusumbua na pengine kuchukuliwa na wenye pesa akiwa tayari amekuwa mkeo, hii ingekuuma zaidi!
 
ungekuwa unazo halafu ukamficha akaja kugundua habari ingekuwa nyingne.
 
Hakuna kitu nachukia kama kudanganywa, be real nikupende kama ulivyo kama huna huna tu kwann upretend unazo wakati unategemea ndugu.
 
Ila asinge maind sana na nina hisia angekuwa mpole kama angegundua ninazo tofauti na kugundua sina ni kapuku!!
 
Always mkielezwa ukweli mnatunanga nakuacha solemba sijui kwa nini!!
 
Habari zenu Wadau,

Nampenzi wangu ambae ni mpangaji kwenye nyumba ya Mama yangu ingawa mimi siishi hapo, tuna miezi 3 mpaka sasa katika mahusiano yetu, Upande wa ndugu zangu naochangia mama wapo vizuri kimaisha ila kwa kinvuli chao nami huonekana hivyo ingawa ni tofauti, Nikamweleza mpenzi wangu mtarajiwa hali halisi ya maisha yangu ila nilimficha ile code ya kinvuli cha ndugu zangu kinachofanya nionekane na mimi nipo vizuri kimaisha.

Miezi yote 3 mpaka sasa sijatembea nae tukiahidina mpaka tufunge ndoa, Nikiwa nachumguza kumbe nae pia alikuwa akinichunguza ndipo akapewa taariifa na wadau wanaonijua vizuri kama mi nimchovu tu nabebwa na kinvuli cha ndugu zangu! hivi kimenuka huku najaribu kumtuliza mpenzi wangu na kumuelewesha sababu ya kumficha ilikuwa nikupata uhakika kama kweli ananipenda ama alikuwa na yeye anajitega kupitia kivuli cha ndugu zangu kama kuna neema.

Naombeni ushauri nifanyeje? naona ameanza na kuniwekea pozi sasa hv napomuita tofauti na mwanzo alikuwa anapigia simu nikimuita fasta anakuja.
Kweli ndoa za siku hizi tusipoangalia tutavua chura badala ya samaki.

Naombe ushauri

Mkuu tafuta hii movie....think like a man...
 
Shukrani nitaitafuta mkuu!!!Wamecheza watu wa nchi gani, nisije, inawezanipa mtazamo tofauti kuhusu wa hawa madada zetu.
 
Back
Top Bottom