Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

Hili ni andiko la George Kahangwa nafikiri unamfahamu vizuri ....soma katikati ya mstari ...

Muuliza swali nashawishika kuamini kwamba ulitaka kujua kweli. Kama ni utafiti naomba uzingatie taarifa hizi

1. Vuguvugu la wanamageuzi lilianza miaka ya 80 wakati wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam walipoanza kuhoji uwepo wa mfumo wa chama kimoja. Ni katika kipindi hicho Ndg. Mabere Nyaucho Marando (Katibu Mkuu wa kwanza wa NCCR) alifanya presentetion hapo chuoni kuhusu suala hilo. (Kama nakala ya presentation yake inaweza kupatikana basi siku moja tutaiweka hapa, kwa ajili ya kuweka kumbukumbu vizuri)
2. Mnamo mwaka 1984, Ndg.James Mapalala (makamu mwenyekiti wa kwanza wa NCCR) alimwandikia Mwalimu Nyerere barua ya wazi akitaka mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini (kumbuka ulikuwepo awali Mwalimu akaufuta)

3.Miaka saba baadaye (1990) Mwalimu akaanza kuelewa (wakati huo alishaacha urais) akaanza kusema si vibaya mfumo wa vyama vingi ukirejeshwa nchini
4. Mnamo mwaka 1991 wasomi wa UDSM, pamoja na wanaharakati wakaianzisha NCCR. Ikawa chini ya Uenyekiti wa Marehemu Chifu Abdallah Fundikira (waziri wa zamani wa Mwalimu), Makamu; Mapalala, Katibu Mkuu; Marando.
5. Mwaka huo huo 91 Rais Ali Hassan Mwinyi akaunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kama vyama vingi viruhusiwe au visiruhusiwe. Watanzania wengi hawakuvitaka, lakini wapo waliosema virudi.
6. Mzee Mwinyi akaheshimu mawazo ya wachache, mwaka 1992 akaruhusu virudishwe.
7. Mwaka huo 1992 (hapa ndipo sura ya sasa ilipotoka) waliokuwemo ndani ya NCCR wakagawanyika. Fundikira Mwenyekiti akaunda chama; UMD (japo kabla hajafa alirejea CCM), Mapalala huyo naye akaunda CCW ambayo kwa kushirikiana na Shaban Mloo wa KAMAHURU ya Zanzibar wakaunda CUF (sasa Mapalala yuko CHAUSTA). Marando akaendelea kuiongoza NCCR kwa kuiboresha na neno Mageuzi (sasa naye yuko CHADEMA), baadhi ya wajumbe wengine wa NCCR wakashiriki kuiunda CHADEMA wakitumia kaulimbiu ya NCCR 'demokrasia na maendeleo'. Na wengine wakaendelea kuunda vingine, matharani hata Mziray wa APPT-Maendeleo anatokea NCCR.

Kwa ufupi NCCR ilisambaa kabla ya ujio wa Mrema. 'ikawa kama maandiko; nitampiga mchungaji wa kondoo, na kondoo wa kundi lake watatawanyika)
8. Ndio sinema ya 1995 ikaanza (Hii sasa usome Kitabu cha Ndimara Tegambwage)

Ndugu asante sana kwa hii highlight nzuri sana

Historia tamu sana mno..na kwa sababu ni iliishatokea huwa haibadiliki, ishatokea na inabaki kuwa dira, mwalimu wa yajayo
 
CHADEMA ndio bye bye hakuna dawa wala uganga inakufa kifo cha Nccr mageuzi,CUF hivi vyama viwili vilipita katika njia wanazopitia chadema kwa hivi sasa,

Nccr baada ya kutamba uchaguzi wa 95 kwa kumpokea kada mkuu wa CCM Lyatonga mrema baada ya hapo ikawa ni mtifuano na kufifisha chama machoni mwa watu mpaka leo hii Nccr haipo labda ukisikia mbatia ndio unakumbuka kuna kitu kinaitwa Nccr mageuzi

Cuf ilipita njia hizi hizi za CHADEMA baada ya kutamba uchaguzi wa 2000 Cuf rasmi iliingia kwenye mitifuano isiyo kwisha mpaka kilizaliwa chama cha kingine kupitia aliyekuwa kada wao maarufu Hamadi Rashidi leo hii kama tunavyoisikia Cuf inapumulia mashine kuna ya zanzibar na ya bara

Historia inatuonyesha CHADEMA baada ya kumchukua kada wa Ccm maarufu Lowassa leo hii CHADEMA ipo kwenye minyukano ya chini kwa chini japo wenyewe wanajaribu kuifunika lakini kwa muonekano tu CHADEMA inayumba na imepoteza muelekeo watu kila kukicha wanaikimbia Chama na wameanza kutuhumiana tuhuma za usaliti wao kwa wao!
Swali kwanini kila kada mkuu wa CCM akihamia chama cha upinzani hukumbwa na dhoruba!
kwani CHADEMA nayo mumeiteka?.
 
OK nendeni mkasherehekee ikulu mjipongeze
 
Upinzani utaendelea tu, Tanzania ni nchi ya vyama vingi na CHADEMA inazidi kuimarika. Peoples✌🏾
Ilishindwa kufa ANC ife chadema, hiyo status haiko, the worse it will go underground, na chama kikienda underground hakuna aliye salama tena
 
Mawazo yakoo tuuu mkuu uwee na fikraa chanya dhidi ya wenzakooo usiwe na hasiii
waombee wenzakoo mema ilii na CCM yako iimarikeeeeee Bila CHADEMA imara
Adui muombee njaa ila nimetoa historia ya mfano ya wenzao walivyodhoofika kwa kuitana wasaliti kisa tu watu wamegusia maslahi ya mtu!
 
CHADEMA for life. Nawaambieni CCM kabla ya 2025 itakuwa ishakaribia kufa kabisa! Watu watakuwa washaanza kupata pata akili. Si unajua CCM mtaji wao ni wa watu wajinga wajinga?
 
CHADEMA for life. Nawaambieni CCM kabla ya 2025 itakuwa ishakaribia kufa kabisa! Watu watakuwa washaanza kupata pata akili. Si unajua CCM mtaji wao ni wa watu wajinga wajinga?
Kwanza wabunge wenye ushawishi watatoka chadema kwenda kukiteka chama, let's wait
 
Back
Top Bottom