NAMNA YA KUOKOA CHADEMA ISIFE
Hakika chama kikuu cha upinzani kinaugua na kiko ICU. Kime ”paralaizi”.
Sio jambo la kufurahisha hata kidogo. Ni msiba wa taifa. Taifa linahitaji upinzani imara na ulio makini ili liweze kusonga mbele. Bahati mbaya sana uongozi wa CHADEMA haswa mwenyekiti wake anaonekana kukata tamaa na kuishiwa mikakati.
Ukisikiliza kauli zake sasa ni za mtu aliyeamua kumwachia mungu! Mkiti wa chama kikuu cha upinzani hapaswi kutoa kauli anazotoa Mbowe hivi sasa. Kauli za “anayetaka kuondoka na aondoke” ni za mtu aliyeshindwa!
Kwa kuwa tupo wengine tunaotaka kuona upinzani ukiimarika ni wajibu wetu kumsaidia Mbowe. Japo kachelewa sana Mbowe kama kiongozi mkuu anapaswa kufanya yafuatayo:
1. Kuitisha mkutano mkuu wa dharura ili kujadili hatma ya chama.
2. Kusitisha mara moja utaratibu wa wabunge kuchangia chama kila mwezi
3. Kutayarisha taarifa yakinifu ya mapato na matumizi ya chama na kuisambaza kwa wanachama na viongozi.
4. Kuvunja mara moja kamati isiyo rasmi. Kamati inayotuhumiwa kuendesha chama kinyemela.
5. Kuacha mara moja tabia ya kutoa maamuzi binafsi kwenye masuala mazito.
6. Kutayarisha mara moja sera za chama kuhusu kilimo, maji, elimu, etc
7. Kutangaza kuwa hatagombea tena kiti kwenye uchaguzi ujao wa chama
8. Kuhakikisha kila mgombea wa chama anahudumiwa bila ubaguzi
9. Kuweka wazi kuwa 2020 nafasi ya mgombea uraisi kwa tiketi ya CDM iko wazi yeyote anaweza kugombea na hatamuunga yeyote mkono.
10. Kutumia ruzuku kujenga ofisi za chama
11. Awaagize viongozi wake waache mara moja kupinga na kukosoa juhudi za serikali ambazo zinawanufaisha wapiga kura.
Haya ndio haswa matatizo yanayofanya viongozi waikimbie CHADEMA na wananchi waidharau CHADEMA.
Ikiwa hatazingatia basi ategemee muda si mrefu kukimbiwa hadi na wajumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu.
Nawasilisha