Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

Chadema ndio bye bye hakuna dawa wala uganga inakufa kifo cha Nccr mageuzi,Cuf hivi vyama viwili vilipita katika njia wanazopitia chadema kwa hivi sasa,

Nccr baada ya kutamba uchaguzi wa 95 kwa kumpokea kada mkuu wa CCM Lyatonga mrema baada ya hapo ikawa ni mtifuano na kufifisha chama machoni mwa watu mpaka leo hii Nccr haipo labda ukisikia mbatia ndio unakumbuka kuna kitu kinaitwa Nccr mageuzi

Cuf ilipita njia hizi hizi za Chadema baada ya kutamba uchaguzi wa 2000 Cuf rasmi iliingia kwenye mitifuano isiyo kwisha mpaka kilizaliwa chama cha kingine kupitia aliyekuwa kada wao maarufu Hamadi Rashidi leo hii kama tunavyoisikia Cuf inapumulia mashine kuna ya zanzibar na ya bara

Historia inatuonyesha Chadema baada ya kumchukua kada wa Ccm maarufu Lowassa leo hii Chadema ipo kwenye minyukano ya chini kwa chini japo wenyewe wanajaribu kuifunika lakini kwa muonekano tu Chadema inayumba na imepoteza muelekeo watu kila kukicha wanaikimbia Chama na wameanza kutuhumiana tuhuma za usaliti wao kwa wao!
Swali kwanini kila kada mkuu wa CCM akihamia chama cha upinzani hukumbwa na dhoruba!
Chadema haifi mamluki wanajiondoa wenyewe
 
na kila anayekufa anaona hafi, mpaka anakufa na kukosa muda wa kujiuliza why

wanachama wote ni nyumbu


kikifa nyumbu wanahamia jengo lingine
Upinzani hautakufa lakini si chadema. Wameshupaza shingo kufanya mabadiliko. Chadema inafutika kwa staili ile ile ya NCCR kwa tuliokuwa tunafatilia siasa tunakumbuka vyema.
 
Wana Ufipa ukiwaambia Chadema utakufa wanadhan tunamaanisha kufa Kama kifo Cha binadamu

Tunamaanisha kifakufa Kwa maana kitakuwa Kama NCCR Au CUF

Hata akiondolewa Kubenea ataibuka mwingine tu Halafu Mara nyingi wale watu wa karibu Na Mbowe anaewaamini Sana ndio huja kum challenge

Alianza Chacha Wangwe, akaja Zitto Kabwe, akaja Dr Slaa Na Sasa Mwandani Na maiti wa Mbowe Ndugu Kubenea Na Komu nao wamechoka

Hata Hawa kina YericKo nao watakuja kumzingua Na kumchoka Mbowe
Mtapata tabu sana na Chadema, eti sio kufa kama binadamu ruksa kubadilika kama kinyonga.
 
na CCM inafuata itakufa kama wale walio zama maji ukerewe
 
Mtapata tabu sana na Chadema, eti sio kufa kama binadamu ruksa kubadilika kama kinyonga.


Siku hizi Mbona mmekuwa Wapole sio Kama enzi Za Mkwere?

Mkwere angewaambia Marufuku Mikutano ya Kisiasa mngetii Kama mnavyomtii Mwenye heri John Magufuli?
 
Upinzani hautakufa lakini si chadema. Wameshupaza shingo kufanya mabadiliko. Chadema inafutika kwa staili ile ile ya NCCR kwa tuliokuwa tunafatilia siasa tunakumbuka vyema.
Kwani wakati wa NCCR ulikuwepo peke yako ina maana wengine hatukuwepo, enzi za Mrema upinzani ulikuwa mchanga haukuwa na mbinu madhubuti wala resources za kupambana figisu za CCM, mihemuko ilizidi uhalisia.

Matatizo ya NCCR yalikuwa tofauti na ya Chadema intelijensia ya NCCR ilikuwa tofauti na intelijensia ya Chadema leo, vile vile kitaasisi huwezi kuilinganisha Chadema na NCCR ya kina Mrema na Marando.
 
Changamoto kubwa ya vyama vya siasa afrika ni kutojisahihisha. hivi vyama vinatumia falsafa ya kutetea wananchi kumbe ni magenge ya watu wachache kwa kivuli cha kutetea wanyonge. chadema walilewa umaarufu. changamoto yao kubwa wameshindwa kumaintain umaarufu.kila anayetoa mawazo tofauti na uongozi ni msaliti au ananunuliwa na ccm, japo suala la ccm kununua wapinzani lipo lakini lisijekuvunja haki za wanachama kuhoji mambo ya msingi kwa nguzo ya usaliti. binafsi mpaka sasa siijaona chama cha siasa cha kumkomboa mtanzania zaidi ya kuiba pesa za wanyonge kupitia ruzuku.
 
Siku hizi Mbona mmekuwa Wapole sio Kama enzi Za Mkwere?

Mkwere angewaambia Marufuku Mikutano ya Kisiasa mngetii Kama mnavyomtii Mwenye heri John Magufuli?
Politics is not static is dynamic, kila wakati na siasa zake, siasa za ustaarabu ni tofauti na siasa za kidikteta.
 
Politics is not static is dynamic, kila wakati na siasa zake, siasa za ustaarabu ni tofauti na siasa za udikteta.
Kwa hiyo kwenye Siasa Za kistaarabu ndio mnapiga mikwara kwenye Siasa Za kidikteta mnaufuata
 
Kwa hiyo kwenye Siasa Za kistaarabu ndio mnapiga mikwara kwenye Siasa Za kidikteta mnaufuata
Hayo sasa ni malumbano yasiyokuwa na hoja ndani yake tafuta swali au hoja nyingine nikujibu.
 
Sa kamakinakufa sindo utulie ushuhudie hicho kifo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom