Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

Namna ya kuokoa CHADEMA isife...

yamindinda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
1,589
Reaction score
1,320
NAMNA YA KUOKOA CHADEMA ISIFE
Hakika chama kikuu cha upinzani kinaugua na kiko ICU. Kime ”paralaizi”.
Sio jambo la kufurahisha hata kidogo. Ni msiba wa taifa. Taifa linahitaji upinzani imara na ulio makini ili liweze kusonga mbele. Bahati mbaya sana uongozi wa CHADEMA haswa mwenyekiti wake anaonekana kukata tamaa na kuishiwa mikakati.

Ukisikiliza kauli zake sasa ni za mtu aliyeamua kumwachia mungu! Mkiti wa chama kikuu cha upinzani hapaswi kutoa kauli anazotoa Mbowe hivi sasa. Kauli za “anayetaka kuondoka na aondoke” ni za mtu aliyeshindwa!

Kwa kuwa tupo wengine tunaotaka kuona upinzani ukiimarika ni wajibu wetu kumsaidia Mbowe. Japo kachelewa sana Mbowe kama kiongozi mkuu anapaswa kufanya yafuatayo:

1. Kuitisha mkutano mkuu wa dharura ili kujadili hatma ya chama.
2. Kusitisha mara moja utaratibu wa wabunge kuchangia chama kila mwezi
3. Kutayarisha taarifa yakinifu ya mapato na matumizi ya chama na kuisambaza kwa wanachama na viongozi.
4. Kuvunja mara moja kamati isiyo rasmi. Kamati inayotuhumiwa kuendesha chama kinyemela.
5. Kuacha mara moja tabia ya kutoa maamuzi binafsi kwenye masuala mazito.
6. Kutayarisha mara moja sera za chama kuhusu kilimo, maji, elimu, etc
7. Kutangaza kuwa hatagombea tena kiti kwenye uchaguzi ujao wa chama
8. Kuhakikisha kila mgombea wa chama anahudumiwa bila ubaguzi
9. Kuweka wazi kuwa 2020 nafasi ya mgombea uraisi kwa tiketi ya CDM iko wazi yeyote anaweza kugombea na hatamuunga yeyote mkono.
10. Kutumia ruzuku kujenga ofisi za chama
11. Awaagize viongozi wake waache mara moja kupinga na kukosoa juhudi za serikali ambazo zinawanufaisha wapiga kura.

Haya ndio haswa matatizo yanayofanya viongozi waikimbie CHADEMA na wananchi waidharau CHADEMA.
Ikiwa hatazingatia basi ategemee muda si mrefu kukimbiwa hadi na wajumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu.
Nawasilisha
 
Last edited by a moderator:
Umesema kweli tupu Mkuu..
Naongezea..
12. Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama haitekelezi wajibu wake ipasavyo na imepwaya. Mashinji abadilishwe na kupewa mwingine mwenye uwezo huo mfano John Heche.
Ikiwezekana Sekretarieti ya Chama iundwe upya.
 
CHADEMA ndio bye bye hakuna dawa wala uganga inakufa kifo cha Nccr mageuzi,CUF hivi vyama viwili vilipita katika njia wanazopitia chadema kwa hivi sasa,

Nccr baada ya kutamba uchaguzi wa 95 kwa kumpokea kada mkuu wa CCM Lyatonga mrema baada ya hapo ikawa ni mtifuano na kufifisha chama machoni mwa watu mpaka leo hii Nccr haipo labda ukisikia mbatia ndio unakumbuka kuna kitu kinaitwa Nccr mageuzi

Cuf ilipita njia hizi hizi za CHADEMA baada ya kutamba uchaguzi wa 2000 Cuf rasmi iliingia kwenye mitifuano isiyo kwisha mpaka kilizaliwa chama cha kingine kupitia aliyekuwa kada wao maarufu Hamadi Rashidi leo hii kama tunavyoisikia Cuf inapumulia mashine kuna ya zanzibar na ya bara

Historia inatuonyesha CHADEMA baada ya kumchukua kada wa Ccm maarufu Lowassa leo hii CHADEMA ipo kwenye minyukano ya chini kwa chini japo wenyewe wanajaribu kuifunika lakini kwa muonekano tu CHADEMA inayumba na imepoteza muelekeo watu kila kukicha wanaikimbia Chama na wameanza kutuhumiana tuhuma za usaliti wao kwa wao!
Swali kwanini kila kada mkuu wa CCM akihamia chama cha upinzani hukumbwa na dhoruba!
 
Ramli hizo hazijaanza leo alitabiri mzee Wasira miaka ya 2010 kafa yeye instead.

IMG_20181017_093157.jpg
 
Wana Ufipa ukiwaambia Chadema utakufa wanadhan tunamaanisha kufa Kama kifo Cha binadamu

Tunamaanisha kifakufa Kwa maana kitakuwa Kama NCCR Au CUF

Hata akiondolewa Kubenea ataibuka mwingine tu Halafu Mara nyingi wale watu wa karibu Na Mbowe anaewaamini Sana ndio huja kum challenge

Alianza Chacha Wangwe, akaja Zitto Kabwe, akaja Dr Slaa Na Sasa Mwandani Na maiti wa Mbowe Ndugu Kubenea Na Komu nao wamechoka

Hata Hawa kina YericKo nao watakuja kumzingua Na kumchoka Mbowe
 
Chadema ndio bye bye hakuna dawa wala uganga inakufa kifo cha Nccr mageuzi,Cuf hivi vyama viwili vilipita katika njia wanazopitia chadema kwa hivi sasa,

Nccr baada ya kutamba uchaguzi wa 95 kwa kumpokea kada mkuu wa CCM Lyatonga mrema baada ya hapo ikawa ni mtifuano na kufifisha chama machoni mwa watu mpaka leo hii Nccr haipo labda ukisikia mbatia ndio unakumbuka kuna kitu kinaitwa Nccr mageuzi

Cuf ilipita njia hizi hizi za Chadema baada ya kutamba uchaguzi wa 2000 Cuf rasmi iliingia kwenye mitifuano isiyo kwisha mpaka kilizaliwa chama cha kingine kupitia aliyekuwa kada wao maarufu Hamadi Rashidi leo hii kama tunavyoisikia Cuf inapumulia mashine kuna ya zanzibar na ya bara

Historia inatuonyesha Chadema baada ya kumchukua kada wa Ccm maarufu Lowassa leo hii Chadema ipo kwenye minyukano ya chini kwa chini japo wenyewe wanajaribu kuifunika lakini kwa muonekano tu Chadema inayumba na imepoteza muelekeo watu kila kukicha wanaikimbia Chama na wameanza kutuhumiana tuhuma za usaliti wao kwa wao!
Swali kwanini kila kada mkuu wa CCM akihamia chama cha upinzani hukumbwa na dhoruba!
Sawa sababu kuu ya haya yote mkuu chanzo nini!
 
Wana Ufipa ukiwaambia Chadema utakufa wanadhan tunamaanisha kufa Kama kifo Cha binadamu

Tunamaanisha kifakufa Kwa maana kitakuwa Kama NCCR Au CUF

Hata akiondolewa Kubenea ataibuka mwingine tu Halafu Mara nyingi wale watu wa karibu Na Mbowe anaewaamini Sana ndio huja kum challenge

Alianza Chacha Wangwe, akaja Zitto Kabwe, akaja Dr Slaa Na Sasa Mwandani Na maiti wa Mbowe Ndugu Kubenea Na Komu nao wamechoka

Hata Hawa kina YericKo nao watakuja kumzingua Na kumchoka Mbowe
Hizo ramli hazijaanza leo. Nyie wapiga ramli wa sasa ni sisimizi tu.
Alianza yule wa Bunda. Sijui yuko wapi sasa.
 
Back
Top Bottom