Namna ya kumtambua mwanaume suruali

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,381
1. Hana kazi lakini anaishi maisha ya hali ya juu kwa sababu ya kuishi kiujanja ujanja na ni mtu wa kujirusha kila weekend na maeneno anayokwenda ni ghali na hupendelea kukaa sehemu ya watu maarufu VIP awapo kwenye club halafu ni mtu wa stori nyingiiiii.

2. Siyo mtu wa kuhangaika kutafuta kazi wala kujishughulisha anakuwa ni mtu wa kujipendekeza kwa wakubwa au watoto wa wakubwa na kupenda kuwa mpambe au kuwadi wa wakubwa ili kujipatia kipato kiurahisi bila jasho.

3. Anapenda kujiremba sana na kupiga picha kila dakika kama mabinti hususan Selfie katikia maeneo ya hadhi tofauti na uwezo wake kifedha na picha hizo husirusha mitandaoni ya kijamii kama Twitter, Instagram, Facebook, Whatsupp nk, na mara nyingi hupenda kupiga picha kifua wazi ili kuonyesha kile anachodhani kwamba atababaikiwa na mabinti wenyewe huita Six Pack.

4.Anapenda kujikwenza na kujifanya anajuana na watu wazito na maarufu kwa sababu ya kutaka kutambuliwa na kuosha

5. Anapenda sana kujiweka karibu na wanawake maarufu wa umri wa kati wenye hadhi na pesa zao ili kuwachuna.

6.Ni mtu wa kupenda kuomba omba misaada au kukopa na kurudisha au kulipa deni ni mtihani.

7. Hupendelea kuishi kwenye nyumba za wageni za kiwango cha juu au cha kati au cha chini kulingana na pesa alizonazo kwa wakati huo ambazo huzipata kiujanjaujanja na hali ikiwa ngumu hupendelea kuishi kwa marafiki zake wanaomhifadhi

8.Vitu vya thamani anavyomiliki ni Nguo ambazo wakati mwingine kupewa na marafiki au kuazima, viatu na cheni za gharama na saa za mkononi tofauti tofauti.

9.Kingine ni u handsome, kiukweli ni wazuri kwa sura na watanashati na wana kauli nzuri zinazowawezesha kuwalaghai watu kiurahisi na ni watu ambao wanajua mambo mengi sana yaani wanakuwa na a lot of information ziwe ni za kitaa au kisiasa na mambo mengine muhimu yanayotokea kila siku.

10. Asilimia 90 ya majina ya watu anaowasiliana nao kwenye simu yake ni wanawake.

Thanks for stopping by.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom