SoC01 Namna ya kulea watoto: Mama ni kulea na siyo kuzaa na baba ni yule anayewajibika kwa watoto wake

Stories of Change - 2021 Competition

Vallekh

New Member
Jul 14, 2021
2
4
TATII YA YA MALEZI NA WAZAZI
“kuwa mama ni kulea na siyo kuzaa na baba ni yule anayewajibika kwa watoto wake”

Vijana wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa sababu labda kwa kutokujua au kujua lakini wasijue hisia sahihi za adhabu za sheria kwa kile wanachofanya au kujua vyote ila wanadharau, hakuna adhabu duniani kama kutengwa na sheria kwa mambo ambayo uliweza kuyaepuka.

Chanda ni Mvulana mwenye miaka 23(2010) ambaye anaishi na baba yake wa kambo katika moja ya familia zilizofanikiwa zaidi kwa wakati huo, wana nyumba mbili Moja ni kubwa na nyengine ni ndogo ambayo ina vyumba viwili na huku ikizungukwa na mabanda ya kuku, bata na mbuzi sambamba na kupigwa uzio huku ndiko anakoishi Chanda na muda mwingi ushinda na Rafiki zake ambao ni Carlos, Robert na Hamoud wote awa wamemaliza kidato cha nne na kupata matokeo mabaya.

wakati mwengine ni muhimu tukawa wadadisi kwa watoto wetu, kwa mara ya kwanza namuona Chanda macho yangu yalimtambua kama aidha ni mtu mwenye mawazo sana au ana jambo linalomuumiza au kama ana dhambi hivi anayoificha si mtu aliependa sana kuongea na watu isipokuwa marafiki zake na mara kwa mara alikuwa anamjibu Mama yake Vibaya hii ilitosha kama familia kuanza kufatilia maisha ya mtoto huyu, baada ya miezi minne ya kuwa karibu na Chanda niligundua makosa mengi ya wazazi wake moja walimpa uhuru mkubwa sana kufanya chochote labda sababu ya uwezo wao wa kifedha sijui au kumfanya ajione yuko na baba yake halisi sijui, nilipoingia chumbani kwake kulikuwa na runinga na Deki ya DVD lakini kulikuwa kuchafu sana wakati ameniacha ndani kwa haraka nilichukua shati lake lilokuwa chafu na kunusa kwenye kora ya shati hili na niligundua alikuwa aidha anavuta sigara au bangi na kurudisha.

Aliporudi aliniuliza kama napenda kuangalia filamu nikasema hapana napenda kuangalia picha za utupu(nilitaka kujua haswa akili ya Chanda asa baada ya kumtilia mashaka), aliniomba kuinuka kwenye kitanda na kisha aliinua kitanda na kuvuta boksi ambalo lilikuwa na madaftari yake lakini ndani yake kulikuwa na DVD zaidi ya sabini zote zilikuwa za filamu za utupu( akili yangu ilifuahi na bila kujijua nilitabasamu sababu ilikuwa imefanikiwa)

Chanda: anko chagua yeyote hapo hata za wao kwa wao zipo kibao sema nyengine amechukua Hamoud. Aliniambia huku akiwa anaunganisha waya
Nilimjibu: hapana leo sitaangalia lakini nimezipenda sana sasa cha msingi hapa nitachukua hizi chache. Haliacha kuunganisha na kusimama. Tuliongea mengi ya familia mara niligundua pia alikuwa na tatizo na mama yake juu ya baba yake mzazi, tuache hili tuendelee na changamoto za ngono kwa vijana.

Baada ya wiki mbili na zaidi nilikuwa karibu pia na Jackline ambaye alikuwa na uhusiano na Chanda lakini waliachana na kilicho nisaidia kujuana na Jackline sababu tulikuwa tumepanga na Happy ambaye alikuwa dada yake na Jackline.

Jackline hakupenda Mimi kuwa karibu na Chanda lakini hakunipa sababu zaidi ya kusema kuwa ni mtu mbaya sana na Mimi nilikuwa najua jambo hili lakini nilitaka kujua zaidi moja kwanini Chanda anapenda kumjibu Mama yake vibaya, kwanini urafiki wake na marafiki zake una siri kubwa wakiwa wanaongea mtu akienda kati yao hawataongea tena

Kwanini? Jackline sasa ananiambia kuhusu Chanda? Baada ya mwaka kuisha nilipata majibu.

Wakati mwengine kuishi kama watu wengine wanavyoishi inakusaidia kujua siri za wengine

Nakumbuka ilikuwa tarehe 23/11/2010 nikiwa nimekaa na Chanda wawili katika fukwe za Ziwa Vickoria Chande alianza kuniambia yeye mwenyewe ilitokea tu( wakati mwengine watu uwa uongea siri zao kwa watu wanaowaamini na kuwa nao karibu au uwa sababu nyengine ikiwemo kujionyesha kuwa ni mtu Fulani kwa mtu anayemwamini hii uja baada watu awa kuzoeana sana)

Unajua mjomba Mimi wanawake wananipenda sana mpaka wengine nawakataa( sababu ya kuwa katika familia yenye uwezo kuliko zote katika wilaya kwa wakati huo) alafu Mimi,Carlos. Robert na Hamoud tumekubaliana mtu akipata mwanamke lazima tumpige mtungo(kufanya tendo la ndoa kwa wanaume kumchangia mwanamke mmoja kwa wakati)
Mimi: kweli mjomba? Sasa mnafanyeje au wanakubali?

Chanda: uwa tunachanga hela na kumpa mtu mmoja ambaye atamfatilia mwanamke mmoja mpaka ampate alafu akimpata uwe anamleta kule kwangu sasa tunachofanya sisi tunatangulia kulala chini ya kitanda(uvunguni) taa inazimwa sasa anaweza kuanza Carlos akimaliza kufanya mmoja wetu anatoka chini kitanda kwa taratibu wanapichana na Carlos na anaendelea ivyoivyo mpaka tunamaliza wote

Mimi: kwa hiyoo huyo mwanamke anakua hajui?(uso wangu unafurahi na hii unamfanya Chande kuwa huru kuongea zaidi)
Chanda: ngumu yeye anakuwa anajua mtu mmoja Yule na taa si inakuwa imezimwa mtu akimaliza anatoka nje mwisho anabaki Yule aliyemleta mwanamke
Mimi: uwa mnatumia kinga?
Chanda: ndio nilisahau kukuonyesha ndani kuna maboksi kibao ya Kinga
Mimi: hakuna siku hata mmoja ambayo ilitokea mwanamke akataka kujua au kuondoka hakiwa na mashaka
Chanda: siku moja nakumbuka tena Mimi nilimleta mwanamke kisha Carlos na Robert walikuwa chini lakini wakati namaliza Robert akaja nyuma Yule mwanake alihisi jambo ghafla akainuka na kunitaka niwashe taa, ilikuwa siku mbaya kweli taa sikuacha na Robert alikuwa nyuma yangu ghafla akamuona, alipomuona akataka kupiga kelele tulimuwai na kumziba mdomo na Robert alikimbia nje mbio na ndio tukamwachia akaanza kulia na kuondoka

Mimi: unajua kuwa ulikuwa unataka kumuua? Sababu ulimziba mdomo na akili ikiwa na hofu kubwa ufanya mwili kupoteza hisia sababu ya kutaka kulifanya jambo moja ambalo linaleta hofu kwake kwa wakati huo kwa hiyo kama ilitokea ungemziba na pua basi ungeweza sababisha kifo bila wewe kujijua na watu wengi wamejikua wanaua kwa njia hii

Chanda: anacheka kwa kicheko, John bwana wewe unajua mambo mengi sana kwanini?

Mimi: nasoma sana vitabu lakini pia natenga muda kutafakari kila ninacho kiona, kukisikia au kukisoma jiulize kama unakimbia jambo baya linalokupa hofu, unaweza kupishana na Mama yako njiani na usimjue?

Chanda: ni kweli Mjomba kuna siku tulikuwa tunavuta bangi ghafla wakaja askari tulikimbia na kufika nyumbani kulikuwa na wageni hata sikuwaona na wakati walikuwa nje lakini niliwapita
Mimi: unajua wewe ni kama mdogo wangu na nataka kuwa sehemu ya mafanikio yako, nimekaa na wewe na kugundua kwana una akili nyingi sana sema hutaki kuzitumia, baba yako yupo lakini hana uwezo

(umajuaje mjomba)

Mimi ni Rafiki wa mama yako au hujui?(anashangaa) mlichokuwa mnafanya wewe, Carlos, Robert na Hamoud ni ubakaji na adhabu yake ni miaka 30 jela lakini pia watu wengine walikuwa wanafunzi, na kulikuwa na uwezekano mkubwa kuambukizana magonjwa hata kama mlikuwa mnatumia kinga kuanzia leo hacha kabisa tabia hii na nitawafuata Rafiki zako.

Chanda amekaa kimya haongei tena nikaendelea ……“ kwanini uliachana na Jackline?” Chanda hakujibu tena wote tukawa tumekaa kimya kwa muda

Chanda: “nisamehe Mjomba unajua ndio maana nilikuwa na mawazo sana maana nimewafanyia wanawake wengi jambo hili lakini kuanzia leo naacha na naenda kupima”

Jibu la Chanda lilinipa matumaini makubwa sana. Wazazi na Walezi tumekuwa na mapungufu makubwa sana kulea, watoto wengi wamekuwa gerezani kwa mambo ambayo kama wazazi au walezi tuliweza kuwasaidia kwa kuwashauri na kufatilia juu ya tabia zao lakini tukadharau tukasubiri serikali itusaidie kulea watoto wetu na inapolea serikali watoto ujuwe itawalea wakiwa gerezani., jiulize yafauatayo:
Mara ngapi umechukua muda kufatilia maisha ya mtoto wako? Kwasababu kwa lolote baya wewe ndio utawajibika kumsaidia

Mara ngapi umefikiria kufatilia maisha ya Rafiki wa mtoto wako?kwakuwaona wasafi, wanasoma wote na wazazi wao wanauwezo basi umelizika?

Mara ngapi umeenda shule si kufatilia matokeo ya mtoto wako bali tabia yake akiwa shuleni?

Mara ngapi umekaa na mtoto wako na kumueleza kuhusu sheria za uharifu na adhabu zake kwa makosa? Namna magonjwa ngono yanavyoambukiza na gharama yake katika kuyatibu?

Mara mwisho lini ulikumbatiana na mtoto wako si kwa sababu katoka safari bali umefurahi kumuona? Mimi nilikuwa namkumbatia Chande kila ninapokutananaye na kumwambia wewe una akili sana sema hutaki kuzitumia.

Vitendo vya Chande na Rafiki zake mpaka sasa vinafanywa kwa namna tofauti, nimeona, nasikia na wengine wakiniambia wenyewe kuwa waanga wa unyama huu, kwenye mavyuo ambako tuna wasomi wanaofanya mambo aya aya, mtaani pia kuna hadithi za watu kuwa wamekuwa wanatumia vinywaji au dawa za kulevya na kuwalevya wanawake kisha kuwafanyia unyama kama huu kama sehemu ya kuwakomoa na mbaya zaidi waanga wa matukio aya hawasemi sababu ni mambo ya aibu kubwa kwa jamii kwamba “Pili alilala na wanume kumi jana” na matokeoa yake wanajikuta kuwa watu wa visasi kwa watu wasiokuwa na hatia.
Mama Chande alipaswa kujua kuwa:

“ MTU MWENYE MSONGO WA MAWAZO SANA WAKATI MWENGINE HUJIBU VIBAYA AU KUFANYA MAMBO YASIYO YA KAWAIDA KAMA SEHEMU YA KUPUNGUZA MAWAZO YAKE BILA YEYE KUJIJUA”

Hali hii utokea sana kwenye mahusiano, ndoa na hata kwenye familia unapoona unapaswa kuchukua atua za ziada kwanini mwenzako kabadilika au mtoto wako? na siyo kulalamika.

Kama baba, mama au mlenzi jifunze kuwa jasusi kwa watoto wako utajua kweli na utaokoa watoto wako,jirani yako na nchi yote.

NANI ATAWEZA KUWASAIDIA WATOTO KAMA CHANDE? NI SISI ZOTE.
 
Back
Top Bottom