kalanga1
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 318
- 432
Habari zenu wanajamvi, naimani mko poa sana, kwa ambao hamko poa nawaombea kwa mungu awasaidie mrejee katika hali zenu.... Bila kupoteza muda niende kwenye swali langu la msingi, kama ukibahatika kumiliki bastola kihalali na uwe na vibali vyote inajulikana kuwa ni kosa kuiweka hadharani ikaonekana, au ukiwa umebeba ikaonekana. Je hakuna kifaa maalum ambacho unakivaa mwilini ili kuficha silaha yako KWA MWANAUME?? Ukizingatia Wengi wao wanavaa manguo ya kubana siku hizi, suruali na tshirt za modo. Au mashati ya modo. hivi hakuna kitu chochote labda unakivaa ndani ya nguo au sehemu yoyote ili ufiche silaha ukiwa barabarani unatembea isionekane ?????? Plz naombeni majibu yenu wanajamvi ili nijue. Kwa mwanaume avae kifaa gani ili afiche silaha yake. Ukizingatia inatakiwa kubebwa kila siku