Namna gani nitawazuia Nyani kula mahindi shambani

Duh kuna watu wana Roho za Wanyama,Yaani Nimkamate Nyani au Ngedere alafu nimchune ngozi sababu kala Mahindi,Mi ntakuwa na njia mbadala ya kuwakomesha.
 
Mbwa hapana, kuna siku mbwa wangu alikuwa anawakimbiza nyani shambani, walipofika mbali nyani wakamgeukia wakamzingira, walimpiga sana makofi nusu afe. Alirudi akiwa na alama za mabanzi mwili mzima
Duh! Umenikumbusha mbali sana kuna siku mbwa wetu alijidai kumfukuza nyani , aliambulia viboko si mchezo
 
Nimewahi kusikia hivyo ukimdaka mmoja ukamtundika hawasogei kabisa, au washirikishe serekali kitengo cha wanyama pori, utawapata ofisi ya wilaya iliyopo karibu na ww.
Sio kazi rahisi, na hao nyani wenzake muda huo unamchuna NGOZI mwenzao wao wapo wapi? Nyani naweza kusema ndio mnyama pekee ambae mmoja akinasa ktk mtego huwa wanamvuta ili kumuokoa na kusepa nae, ingawa wanapomvuta ndio wanarahisisha kumuua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakupa mbinu hii
Ukiweza kumkamata mfunge zile kengele ndogo wanazovisha ng'ombe au mbuzi hakikisha iyo kengele umeibana vizuri,sasa mwachie aende atakavyokuwa anawakilimbia wenzake basi nao watakuwa wazidi kimkimbia na mwisho wa siku wataama na watakuwa wameingia wilaya nyingine

Amini nakwambia nilimfunga mmoja waliakimbia na kuama takribani kilometa 20 na nyani uyo nilimkuta amekufa na nikatoa kengele yangu
Na wale wengine walikuwa wamedhoofu sana kwa kukimbia sana na ile sauti ya kengele ndo iliwamaliza kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama wanakimbia sauti ya kengele si unaweza ifunga kwenye njia zao mtini ili upepo ukija zinapiga kengele
 
Tafuta mapapai yaliyoiva,toboa weka sumu,watapukutika balaa,lakini jamaa wa wanyapori wakigundua msala...
Sio salama atumie mechanical technician ,hata ukigoogle utaona India wanafanya nn.
Mfano tembo au nguruwe pori,au swala na wote walao nyasi waharibifu Kama una shamba kubwa ukitumia drones zinafanya kazi vizuri Sana wanyama wanakimbia balaa
 
Duh kuna watu wana Roho za Wanyama,Yaani Nimkamate Nyani au Ngedere alafu nimchune ngozi sababu kala Mahindi,Mi ntakuwa na njia mbadala ya kuwakomesha.
Zipo nyingi Google friendly tusiwatendee ukatili wanyama tusiharibu ecologia.
 
Back
Top Bottom