Spika Ndugai: Nyani wanashangilia kifo cha mkulima wa mahindi wanasahau mwakani hawana pa kula

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,860
2,000
Hii kauli ya Spika wa bunge mh Ndugai inafikirisha sana.

Hao nyani wanaofurahia kifo cha hayati Magufuli ni akina nani?

Je, ni Ufipa?

Na kwanini mwakani watakosa chakula?

Hata hivyo Ndugai amesema wanaoshangilia wanajidanganya Tanzania haitarejea kuwa shamba la bibi kamwe.

Maendeleo hayana vyama!

========================

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewashukia watu wanaofurahia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli (61), kilichotokea Jumatano ya tarehe 17 Machi 2021.

Kiongozi huyo wa mhimili wa bunge, amewashukia watu hao leo Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, wakati mwili wa Hayati Rais Magufuli ukiagwa na wabunge kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma.

Hayati Magufuli amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.

Akizungumzia kifo hicho, Spika Ndugai amewafananisha watu hao na nyani waliofurahia kifo cha mwenye shamba la mahindi, ambaye alikuwa anawazuia kula mahindi yake.

“Sasa iko hadithi ya wale nyani walioshambulia shamba la mkulima kwenye mahindi, wakifurahi sana mahindi yanapokuwa yanaiva wanavuna wanakula, walipopata habari mwenye shamba amefariki wale nyani walifurahi sana.”

“Naamini katika nchi yetu manyani wa namna hii hawakosekani, lakini wakasahau mwaka uliofika wakati mahindi kuiva wakarudi shambani kula mahindi wakasahau mwenye shamba alifariki mwaka jana wakawa wanasikitika,” amesimulia Spika Ndugai.

Spika Ndugai ameshauri Watanzania, wasiwe kama ngedere hao kwa kutofanya mambo mabaya ambayo hayati Rais Magufuli aliyakataza.
 

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,666
2,000
Waislam wengi ni watu waungwana sana (though mimi sio Muslim). Kwenye hotuba ya Speaker wa baraza la wawakilishi na yule mbunge (mwislam) aliyeenda kusoma dua wamemeombea Hayati Magufuli msamaha kwa kuwa wanatambua kuwa Magufuli alikuwa binadamu hivyo kuna watu aliwakosea. Hawa wa kwetu wameanza kuita wenzao manyani. Inasikitisha sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom