Namna English Medium zinavyoua elimu yetu

Namna English Medium zinavyoua elimu yetu

Kwanza naomba mnivumilie wale nitakaowakwaza. Nataka nizungumzie kuhusu elimu yetu ya msingi haswa kwenye hizi English medium schools ambazo tumetokea kuziamini sana.

Hizi shule zinaua elimu ya nchi kwa sababu kubwa zifuatazo.

1. Watoto wanafanyiwa mitihani ya ndani mpaka ya mwisho. Mitihani ya ndani inafanywa na walimu ili kuwaonyesha wazazi kuwa watoto wanafanya vizuri, hii inavutia biashara ya shule. Pia mitihani ya mwisho haswa ya standard 4 na 7 inafanywa chumba cha mtihani yote ni sababu matokeo mazuri yanaitangaza vizuri shule.

2. Walimu wa kigeni haswa Wakenya na Waganda, hawa ni tatizo kubwa sana kwenye elimu yetu, najua hawa watu wa huko ni wazuri sana kwenye lugha ya kingereza hivyo hata wamiliki wa shule na wazazi wanawapenda sana, mwanzoni waliingia kama walimu wa English na science kidogo, ila sasa wanafundisha mpaka somo la kiswahili. Unashangaa mwalimu wa geography kutoka Kenya hajui hata ziwa Manyara lipo wapi, hajui hata kama Tanga ni jiji.

Mwalimu wa civics hajui hata TANU wala ASP, hamjui hata Waziri kawawa. Mwalimu wa history hajui hata Amboni caves ipo wapi. Hapa unategemea nini zaidi ya mtoto asiyejua vitu.

3. Watoto wanakaririshwa kama kasuku.

Matokeo yake ni nini.

Watoto wanamaliza elimu ya msingi wanaongea na kuandika kingereza lakini hawana uelewa kiundani wa mambo mengi. Fanyeni majaribio ya kuwatahini watoto majumbani muone matokeo yake mlinganishe na wanayopata darasani.

Watoto wanapofika secondary schools wanaonekana wameshuka baada ya kuachwa mbali na wanaotoka Kayumba. Kiukweli hawajashuka ila hicho ndio walichovuna huko English medium schools baada ya kulipia mamilion ya pesa.

Mwisho, Naomba Serikali ifanye ukaguzi wa kina kwenye hizi shule japokuwa nyingi ni za wakubwa. Kuna walimu wengi sana sio walimu ila ni waongea kingereza wazuri hawa ndio wanageuka walimu wa kutumainiwa bila kujali content zao.

Hizi ni shule ni bomu ambalo wazazi wengi na Serikali litawalipukia.
Simple usiwapeleke wa kwako, just simple. Waache wengine wapotee njias. St Francis, Marian, Feza and the like zote ni bure! ni mbovu kuliko Kayumba
 
Kama huna fedha za kupeleka mtoto English medium acha umbea omba msaada ili na mwanao akasome huko!!! Maana marafiki zake sio wale wanaogawana pipi moja, andazi moja, kiatu kimepasuka upande, nguo haijanyooshwa pasi!!! Tafuta pesa umtafutie mwanao marafiki wenye upeo mkubwa na sio marafiki wa mtaani wa kuchezea vumbi na midoli!!!! Watoto wa English medium hukuti amechafuka kama watoto walio katika shule zetu tulosoma enzi hizo!!! Sasa elimu ni pesa !!!!
kimbembe kinakuja pale tu mnapokutana Advance au chuo Hapo utaona aliezoea kutafuniwa anavyohaha akicheza kidogo tu either kwa kumpoteza mzazi bax ila kuna watoto wa mbwa mtu anapga dili zake anajisomesha na class kama kawa anakimbiza
 
Hehe mkuu umenikumbusha mbali sanaaa... Miaka miwili iliyopita nilikuwa nimetoka malysia kusoma,, nilikuwa huko kwa miaka kadhaa,, nilipo rudi nikakuta mdogo wangu yupo darasa la sita hizi shule ya medium.. Yaaani wamekalilishwaa sanaa aisee,,, one day tulipishana na kauli na huyoo mtoto maaana ni ka jeuri hatari na si unajua hivi vilast born vilivyo...
‘‘ nikamwambia norah bring ur ASS here‘‘

Alinijibu i dnt have a “donkey“

Hehehehe

Mkuu Sasa hapo ulikuwa una test nine?Vocabulary au kwamba dogo anajua matusi kwa kiingereza?
 
Aisee ni kweli kabisa mi nimefundisha moja ya shule hizo. Walimu wengi wanaotoka Kenya na Uganda ni form four liver tu but wanafoji vyeti Vya ualimu. Kuna mwalimu alikuwa mgeni akapewa civics kuna siku alinishangaza tulikuwa tunaangalia sherehe za muungano live (nilikuwa nakaa naye) akaniambia nimuonyeshe kikwete....nilichukia sana. Yaani alikuwa hajui chochote

wakenya wanajua kiinglishi..angalia pekundu utaelewa
 
Jamani msiwe too general ..mleta Uzi haujafanya research ya unachokiongea na hauna haki ya kuweka shule za medium katika kapu moja...though kuna baadhi ya shule wanaiba mitihani ila so zote..
Kafanye research yako na utuambie sample yako ilikuwaje.
.
 
Hehe mkuu umenikumbusha mbali sanaaa... Miaka miwili iliyopita nilikuwa nimetoka malysia kusoma,, nilikuwa huko kwa miaka kadhaa,, nilipo rudi nikakuta mdogo wangu yupo darasa la sita hizi shule ya medium.. Yaaani wamekalilishwaa sanaa aisee,,, one day tulipishana na kauli na huyoo mtoto maaana ni ka jeuri hatari na si unajua hivi vilast born vilivyo...
‘‘ nikamwambia norah bring ur ASS here‘‘

Alinijibu i dnt have a “donkey“


Na wewe nawe hicho cha kusema hapa?! Unatukana mtoto halafu unajichekesha? Ulitegemea shule afundishwe hayo matusi? Hiyo ni kazi yako wewe na wajinga wenzio!!
 
Hii mada ingekuwa ya maana sana kama mleta mada angekuwa ametuletea matokeo ya utafiti (kwa kuzingatia vigezo vinavyokubalika kisayansi) yenye hitimisho alilofikia; na pia kama angeeleza maslahi yake katika hili suala (mzazi, meneja wa shule, mtafiti, nk). Kinyume chake huu mjadala hauna tofauti na porojo za kijiweni. Cha kuzingatia hata hivyo ni kuwa mzazi ndiye mdau nambari wani wa elimu ya mtoto wake. Tusiwafanye wazazi wa watoto katika shule hizi hawajui wafanyalo. Hakika kama ni uchaguzi tu ambao hauzingatii uwezo wa kipato, wazazi wote Tanzania wangepeleka watoto wao hizo shule za Kiingereza. Huu ndio ukweli. Ni matumaini yangu kuwa serikali ijayo itaondoa huu ubaguzi katika utoaji elimu kwa kufanya elimu ya msingi nchini kote kutolewa kwa Kiingereza. Pia natoa onyo kwa wote wanaojaribu kukibeza Kiingereza. Huu ni upofu. Kiingereza ndicho 'Kiswahili' cha dunia!
 
dah hapo kwenye kukaririshwa kama kasuku nakubaliana na wewe asilimia 100. Kuna siku nilikutana na watoto wa shule moja international nikawa nawauliza maswali, yaani ilikuwa ni kioja. Wote majibu ni sawa na yote siyo sahihi, kisha wote the way wanavyoanza kujibu maswali wote ni sawa. Yaani hizi elimu zimekuwa kituko sasa.

well said
aslimia mia moja iko hivyo
 
Simple usiwapeleke wa kwako, just simple. Waache wengine wapotee njias. St Francis, Marian, Feza and the like zote ni bure! ni mbovu kuliko Kayumba

acha kupanic brother. Mtoa mada hajasema shule zote, amesema some of .... English medium schools

St Francis, Marian, Feza and the like
ni English medium schools? Nisaidie
 
Hakika umenena kweli tupu.
Watoto wetu wanachokizungumza kwa kiingereza ukimuuliza kwa kiswahili hajui maana yake. kwa ufupi wanakaririshwa. Pia walimu wengi sio Walimu kiuhalisia bali ni wazungumza kiingereza hivyo hutoa content mbovu kwa wanafunzi.
kuna shule moja wilaya ya same, mpishi aligeuka kuwa mwl wa Jiografia
Inaitwaje? Mpishi aweza kuwa na profession mbili.
 
Inaitwaje? Mpishi aweza kuwa na profession mbili.

Tukubaliane tu kwamba fani ya ualimu imevamiwa. Bongo kila mtu anawezakufundisha sio msingi wala sekondari. Ukijua kusoma na kuandika basi ww mwalimu tayari.
 
Hehe mkuu umenikumbusha mbali sanaaa... Miaka miwili iliyopita nilikuwa nimetoka malysia kusoma,, nilikuwa huko kwa miaka kadhaa,, nilipo rudi nikakuta mdogo wangu yupo darasa la sita hizi shule ya medium.. Yaaani wamekalilishwaa sanaa aisee,,, one day tulipishana na kauli na huyoo mtoto maaana ni ka jeuri hatari na si unajua hivi vilast born vilivyo...
‘‘ nikamwambia norah bring ur ASS here‘‘

Alinijibu i dnt have a “donkey“

Hehehehe

Kwa hilo simlaumu mtoto. Unataka aanze kujua Ass kama unavyojua wewe??
 
Tukubaliane tu kwamba fani ya ualimu imevamiwa. Bongo kila mtu anawezakufundisha sio msingi wala sekondari. Ukijua kusoma na kuandika basi ww mwalimu tayari.

Hahahaha.... Nataman niijue hiyo skuli... maana huko same ni homeland aisee
 
Dadavua vizuri basi mkuu hizo faulo zikoje? Binafsi mimi dogo alipiga 100% nikamuuliza maswali 3 kati ya maswali 25, yote akakosa akasema tunafanyiwa mitihani.
 
Hvi unajua kuwa walosoma kabla ya shule hizi kuwa nyingi nchini ndo wabunifu, wataalam na viongoz wazur? Elimu ya kpindi cha awal ilimuwezesha mtu kuwa mbunif wa uhakka! Kuanzia wanamichezo, wnamzik, waklima, viongoz n.k. Kwa mpango huu wa kkariri utawapata wap watu hao!!
 
hili taifa lilishakufa....eti leo CCM wanawadanganya na mzee wa kukariri magufuli alafu mijitu inashangilia....mnaamini magufuli atafanya lolote chini ya mwongozo wa CCM...mkiamini Magufuli atakuwa huru tu kuamua.....tatizo nchi hii ni CCM.....si mtu....Watanzania watambue hilo.....tusaidiane kuelimishana hivyo....

Tupe mbadala basi wa Ccm maana kulalama haitoshi Mkuu
 
Back
Top Bottom