Namna English Medium zinavyoua elimu yetu

Namna English Medium zinavyoua elimu yetu

Wizara ya Elimu isipuuze hoja iliyoletwa na Mdau.Hali ni tete,Elimu yatu tumeitelekeza mikononi mwa wasio na Taaluma ya Ualimu.Arusha ifanywe kama case study na waletwe wataaluma toka nje ya Arusha ili kuondoa mazingira ya RUSHWA kubaini ukubwa wa Tatizo
 
Aisee ni kweli kabisa mi nimefundisha moja ya shule hizo. Walimu wengi wanaotoka Kenya na Uganda ni form four liver tu but wanafoji vyeti Vya ualimu. Kuna mwalimu alikuwa mgeni akapewa civics kuna siku alinishangaza tulikuwa tunaangalia sherehe za muungano live (nilikuwa nakaa naye) akaniambia nimuonyeshe kikwete....nilichukia sana. Yaani alikuwa hajui chochote

mkuu kwani we ni univasite LIVER?
 
Elimu ya mtoto haipati shule au kwa mwalimu peke yake.

Elimu ya mtoto inaanza nyumbani kwa mzazi.

Je, mzazi unakaa meza moja na mtoto kila jioni kumsaidia homework?

Unamzoesha kusoma na kumnunulia vitabu mbalimbali au unamwacha kuangalia TV?

Unampeleka mbuga za wanyama na nyumba za makumbusho ili ajue nchi yake vizuri?

Unaenda na mtoto wako camping milima ya Morogoro ili ajue chakula chake kimetoka wapi, ajue maisha ya wakulima na taabu zake?

Umemnunulia telescope ili awaze kuona nyota na kujifunza na kuona vitu vidogo kama "milky way" ?

Unamchukua madukani ili afahamu hesabati na gharama za maisha?

Unampeleka mtoto maktaba kusoma vitabu mbalimbali au umekusanya nyumbani vitabu mbalimbali ili aweze kusoma vitu mbalimbali zaidi ya masomo yake?

Umemnunulia mtoto darubini ili aone ndege katika miti?

Una tabia ya kukaa na mtoto na kuzungumza vitu kama habari mbalimbali za siku?

Unamwonyesha matumuzi mazuri ya mazingira kama ya kutupa taka sehemu yake?

Umemnunulia mtoto mnyama kama mbwa, kasuku au paka ili ajue jinsi ya kulea kiumbe kwa mapenzi?

hapana yote hayo sijafanya kwasababu maisha hayo yanapatikana kwenye tamthilia tu
 
mleta uzi uko too general. Mbona hzo hzo english medium ndo znazoongozea katika mitahani ya taifa
 
kuna watoto wa international school flani hivi ipo Arusha nilishangaa kuona eti hawajui ng'ombe ana miguu mingapi, moja kwa moja ikanipa picha kuwa yawezekana hata ng'ombe mwenyewe hawamjui... inasikitisha sana.

hii ni chungu kumesa yerro,,, watoto ya arusa hapana chua ng'ombe??!! yani watoto ya kigoma hapana chua migebuka ana miguu ngapi?
 
Tanzania imejaa watu wengi wenye mtazamo kama yako.
1.hamkubali kuwa kenya na uganda wako mbele kielimu
2.hamkubali kuwa hata watumishi wa kitanzania ni wavivu na wezi ndiyo maana makampuni ya nje inapenda kuajiri wakenya na waganda.
3.kama mnaamini kwa dhati kuwa mko sawa kielimu kwa nini msifanye kama european union raia wa east africa waruhusiwe kufanya kazi kokote bila permit?halafu muone hizo degree zenu za tumaini university mtapeleka wapi?wako poor kwa hata grama.
4.hamkubali baba yenu wa taifa alikuta elimu nzuri kutoka ukoloni akavuruga.
5.viongozi wote wa serikali ya tanzania kwa nini watoto wao hawakuwaacha wasome shule ya kawaida kama walikuwa wanaamini kama nyerere?ulikuwa ukienda st constantine na arusha school unakuta watoto wa vigogo wote from nyerere family,karume,sokoine.kama wakina namelo sokoine,amina na halima karume,kevin na matare nyerere.
6.Tanzania hamna tabia ya kusoma ni porojo nyingi ukipanda basi au treni nchi zenye tabia ya kusoma utakuta abiria karibu wote na vitabu wanasoma,tanzania porojo njia yote.
7.raia wenye uwezo wengi watoto wao wanasoma kenya au uganda na hao ndiyo wako kwenye uhalisia (reality)
8.hizo shule zenu za serikali ya waalimu waliofeli ndiyo inauwa elimu ambayo ina wanafunzi asilimia 95 nchini

jibwa koko weee
 
Kwanza naomba mnivumilie wale nitakaowakwaza. Nataka nizungumzie kuhusu elimu yetu ya msingi haswa kwenye hizi English medium schools ambazo tumetokea kuziamini sana.

Hizi shule zinaua elimu ya nchi kwa sababu kubwa zifuatazo.

1. Watoto wanafanyiwa mitihani ya ndani mpaka ya mwisho. Mitihani ya ndani inafanywa na walimu ili kuwaonyesha wazazi kuwa watoto wanafanya vizuri, hii inavutia biashara ya shule. Pia mitihani ya mwisho haswa ya standard 4 na 7 inafanywa chumba cha mtihani yote ni sababu matokeo mazuri yanaitangaza vizuri shule.

2. Walimu wa kigeni haswa Wakenya na Waganda, hawa ni tatizo kubwa sana kwenye elimu yetu, najua hawa watu wa huko ni wazuri sana kwenye lugha ya kingereza hivyo hata wamiliki wa shule na wazazi wanawapenda sana, mwanzoni waliingia kama walimu wa English na science kidogo, ila sasa wanafundisha mpaka somo la kiswahili. Unashangaa mwalimu wa geography kutoka Kenya hajui hata ziwa Manyara lipo wapi, hajui hata kama Tanga ni jiji.

Mwalimu wa civics hajui hata TANU wala ASP, hamjui hata Waziri kawawa. Mwalimu wa history hajui hata Amboni caves ipo wapi. Hapa unategemea nini zaidi ya mtoto asiyejua vitu.

3. Watoto wanakaririshwa kama kasuku.

Matokeo yake ni nini.

Watoto wanamaliza elimu ya msingi wanaongea na kuandika kingereza lakini hawana uelewa kiundani wa mambo mengi. Fanyeni majaribio ya kuwatahini watoto majumbani muone matokeo yake mlinganishe na wanayopata darasani.

Watoto wanapofika secondary schools wanaonekana wameshuka baada ya kuachwa mbali na wanaotoka Kayumba. Kiukweli hawajashuka ila hicho ndio walichovuna huko English medium schools baada ya kulipia mamilion ya pesa.

Mwisho, Naomba Serikali ifanye ukaguzi wa kina kwenye hizi shule japokuwa nyingi ni za wakubwa. Kuna walimu wengi sana sio walimu ila ni waongea kingereza wazuri hawa ndio wanageuka walimu wa kutumainiwa bila kujali content zao.

Hizi ni shule ni bomu ambalo wazazi wengi na Serikali litawalipukia.

Unayosema ni kweli ila hata kama mimi ni Mkenya ama Mganda napata ajira ya uhakika Tanzani japo hata sijuwi history ya TZ vizuri nitakuja tu kufanya kazi. After all, hao watoto si wangu na hata elimu ya TZ ikishuka kwangu si ishu maana nchi itabaki kuwa ya wajinga na wageni kama mimi na wenzangu ndio watakaopata ajira kwa siku za usoni. Kosa ni la serikali ya TZ kutojali.
 
Hehe mkuu umenikumbusha mbali sanaaa... Miaka miwili iliyopita nilikuwa nimetoka malysia kusoma,, nilikuwa huko kwa miaka kadhaa,, nilipo rudi nikakuta mdogo wangu yupo darasa la sita hizi shule ya medium.. Yaaani wamekalilishwaa sanaa aisee,,, one day tulipishana na kauli na huyoo mtoto maaana ni ka jeuri hatari na si unajua hivi vilast born vilivyo...
‘‘ nikamwambia norah bring ur ASS here‘‘

Alinijibu i dnt have a “donkey“

Hehehehe

sasa haya ya kusoma malaysia yanahusiana nini na stori yako? ata ivo haichekeshi na najua hakuna ataenukuu hii stori yako
 
English medium schools mtihani wa mwisho darasa la saba wanafanya wa taifa kama shule za kanumba. Fuatilia. Na matokeo yao yanachanganywa na shule za kawaida na wanapangiwa shule za secondary vile vile. Sasa hoja ni kwamba wanafaulishwa kuwapendezesha wazazi madarasa ya chini. Labda kweli. Kwa nini na mitihani ya darasa la saba ya wizara wanafanya vizuri? Mengine uliyoongea ya walimu wa Kenya yaweza kuwa sahihi.
 
Labda namba 1 yako ni ya kufanyia kazi lakini kwani hata wa Kiswahili anaweza kufanyiwa mitihani; 2 na 3 hakuna point kabisa i.e. illogical kwa sababu mimi nimesoma mambo katika ngazi zote bila kufika maeneo hayo ya dunia wala kuwaona wahusika. Nafikiri ulivyosema 'kuwajua' una maanisha 'kuwaona au kuwashuhudia'. Mfano, kwenye Historia nimesoma pre-colonial societires wala sikuwa nimezaliwa. Nimesoma vita kuu za dunia na akina Hitler wala sikuwahi kuwafahamu. Haya kwenye Geography nimesoma coffee kulima Brazil wala sijawahi kufika huko. Kagera kwenyewe sijawahi kufika. Physics - laws of motion wakati sijawahi kuonana na Isaac Newton.

sasa umeongea nini tena na wewe?
 
hapana yote hayo sijafanya kwasababu maisha hayo yanapatikana kwenye tamthilia tu

Siyo kweli.

Leo, wewe ukitaka, unaweza kusikiliza lecture za maprofesa mbalimbali wa vyuo vya nje bure. Wanafunzi wa Ivy League Marekani wanatozwa $50,000 kwa mwaka kusomeshwa katika masomo hayo hayo.

Kama huna vitabu nyumbani au hamna maktaba karibu yako, unasoma vitabu vya aina yote bure kwa kutumia mtandao.

Unaweza kumfundisha mtoto namna ya kutengeneza redio, simu, kompyuta, gari na vitu vingine kama hii ni hobby yake kwa kutumia mtandao.

Unaweza kusoma lugha zote bure katika mtandao leo.

Unaweza kumfundisha jinsi ya kutafuta station za redio za nchi mbalimbali ili asikilize taarifa mbalimbali na kuboresha uwezo wake wa kusikiliza lugha mbalimbali na papo hapo kuzidisha msamiati wake.

Telescope na binoculars $30 used.
Tablets zinashuka bei kila miezi sita. ASUS memo pad 7 ni $80 used leo.

Hamna maisha ya tamthilia hapa, ni maisha yanayowezekana kumpa mtoto kwa wazazi wenye uwezo wa kawaida. Unaweza kuchanga polepole.

Fedha hizi Watanzania wengi wanazo leo, (siyo wote) ila wengi wanazitumia katika starehe.

Kama askari wa nyumba anaweza kununua simu na mtandao kwa mshahara wake wa chini, wewe unaweza kukidhi haya mahitaji ya mtoto. Labda uwe mvivu au mlevi.

Ona picha ya mtoto masikini wa Ufilipino. Kwao hamna umeme, yeye anakaa chini, katika dirisha la duka ili apate mwangaza wa kufanya homework yake.

ImageUploadedByJamiiForums1437256359.823727.jpg

Nothing is impossible.
 
Hakika umenena kweli tupu.
Watoto wetu wanachokizungumza kwa kiingereza ukimuuliza kwa kiswahili hajui maana yake. kwa ufupi wanakaririshwa. Pia walimu wengi sio Walimu kiuhalisia bali ni wazungumza kiingereza hivyo hutoa content mbovu kwa wanafunzi.
kuna shule moja wilaya ya same, mpishi aligeuka kuwa mwl wa Jiografia
 
Siyo kweli.

Leo, wewe ukitaka, unaweza kusikiliza lecture za maprofesa mbalimbali wa vyuo vya nje bure. Wanafunzi wa Ivy League Marekani wanatozwa $50,000 kwa mwaka kusomeshwa katika masomo hayo hayo.

Kama huna vitabu nyumbani au hamna maktaba karibu yako, unasoma vitabu vya aina yote bure kwa kutumia mtandao.

Unaweza kumfundisha mtoto namna ya kutengeneza redio, simu, kompyuta, gari na vitu vingine kama hii ni hobby yake kwa kutumia mtandao.

Unaweza kusoma lugha zote bure katika mtandao leo.

Unaweza kumfundisha jinsi ya kutafuta station za redio za nchi mbalimbali ili asikilize taarifa mbalimbali na kuboresha uwezo wake wa kusikiliza lugha mbalimbali na papo hapo kuzidisha msamiati wake.

Telescope na binoculars $30 used.
Tablets zinashuka bei kila miezi sita. ASUS memo pad 7 ni $80 used leo.

Hamna maisha ya tamthilia hapa, ni maisha yanayowezekana kumpa mtoto kwa wazazi wenye uwezo wa kawaida. Unaweza kuchanga polepole.

Fedha hizi Watanzania wengi wanazo leo, (siyo wote) ila wengi wanazitumia katika starehe.

Kama askari wa nyumba anaweza kununua simu na mtandao kwa mshahara wake wa chini, wewe unaweza kukidhi haya mahitaji ya mtoto. Labda uwe mvivu au mlevi.

Ona picha ya mtoto masikini wa Ufilipino. Kwao hamna umeme, yeye anakaa chini, katika dirisha la duka ili apate mwangaza wa kufanya homework yake.

View attachment 269206

Nothing is impossible.

mkuu naona bado unanisimulia tamthilia tu,, anyway kama wewe una uwezo huo mshukuru mungu tu watanzania wengi hatunao
 
mkuu naona bado unanisimulia tamthilia tu,, anyway kama wewe una uwezo huo mshukuru mungu tu watanzania wengi hatunao

Muda uliotumia kusoma na kunijibu mara mbili, ungeweza kusoma kitabu cha bure katika mtandao na mwanao.

Kama huu ni mfano wa tamthilia, basi ichukulie tu hivo hivo. Haina ugomvi.
 
Kama huna fedha za kupeleka mtoto English medium acha umbea omba msaada ili na mwanao akasome huko!!! Maana marafiki zake sio wale wanaogawana pipi moja, andazi moja, kiatu kimepasuka upande, nguo haijanyooshwa pasi!!! Tafuta pesa umtafutie mwanao marafiki wenye upeo mkubwa na sio marafiki wa mtaani wa kuchezea vumbi na midoli!!!! Watoto wa English medium hukuti amechafuka kama watoto walio katika shule zetu tulosoma enzi hizo!!! Sasa elimu ni pesa !!!!
 
Umesema kweli, Mkuu.
Pesa anayo, lakini ya kunywa bia kila siku / weekend na ya kuhudumia mademu sita nje bila kusahau na simu mbili za mkono.

Starehe tumeweka mbele sana.
 
Mleta thread umeweka Sawa Sana. Tunawapokea huku vyuo vikuu ni shida. What they know ni slang English, uvivu, na tabia za mashaka kijinsia moja fulani.
 
International Schools ziko chache Tanzania
ISM, IST, Feza International, Savannah High,HOPAC, Academic....
Hizo nyingine zote ni english medium, huko english medium ndo kuna uozo mkubwa sana
 
Kama huna fedha za kupeleka mtoto English medium acha umbea omba msaada ili na mwanao akasome huko!!! Maana marafiki zake sio wale wanaogawana pipi moja, andazi moja, kiatu kimepasuka upande, nguo haijanyooshwa pasi!!! Tafuta pesa umtafutie mwanao marafiki wenye upeo mkubwa na sio marafiki wa mtaani wa kuchezea vumbi na midoli!!!! Watoto wa English medium hukuti amechafuka kama watoto walio katika shule zetu tulosoma enzi hizo!!! Sasa elimu ni pesa !!!!

eeeh mkuu nisaidieni basi kusema kweli uwezo huo sina
 
Back
Top Bottom