Namna bora ya kukata roho

Namna bora ya kukata roho

wewe unataka kila kitu kiandikwe kwenye Bibilia........!!!!!!???? toka ndani ya Duara bro........!!!!Dunia ina mambo mengi..............ikiwemo viumbe visivyoonekana..........
 
Kifo ni mwanzo sio mchakato. Once roho inapoachana na mwili husafiri mamilioni ya kilometers kwenye utupu wa dunia. Ni kama imetoka kifungoni na sasa iko huru. Roho ndani ya mwili uwezo wake huwa wa mipaka mno. Ni mpaka mtu afanye juhudi za kufungua jicho la tatu ndio kidogo unaweza kuona zaidi ya kuona.

Kiingereza tunasema seeing beyond. Bila kujali roho itasafiri kwenda wapi mautini ama katika uhai bado kuna muunganiko usiokoma na mwili husika, hivyo daima hurejea. Watu wale walionusurika vifo, yani wale waliofika hatua ya umahututi. Katikati ya kifo na uzima, wakizinduka hukwambia kwamba wameota ama waliona wanaenda mbali sana. Mbali kabisa angani ama chini ya dunia kusiko na mwisho ama tambarare isiyo na ukomo.

Wanaenda tu lakini hawafiki na walikuwa wanasikia sauti kwa mbali zikiwaita warudi. Kifo ni mwanzo sio mchakato. Death is the state not the process.
View attachment 584381

Kila roho ina asili. Ina makazi asili na makazi mbadala, makazi ya muda ama makazi ya kupita
Mwezi uliopita mwishoni tulipoteza kijana wetu ofisini alianguka umbali wa mita tano toka juu na akatua kwenye zege. Nilikuwa naye mpaka anakata roho. Tulifanya juhudi mbalimbali za kuokoa maisha yake. Tukamkimbiza hospital ya mkoa na baadae Muhimbili kwa ambulance

Muda wote huo niliona alivyokuwa akipambana roho isimuache. Niliingia ulimwengu wa roho kimyakimya kumsaidia uhai, mapambano. Ni kupitia huko nilimuona akielea mbali kabisa na mimi. Alikuwa mwepesi na mwenye kasi ya ajabu. Nilirudi kimwili na kumuona akijaribu kupepesa macho huku madaktari kwa juhudi kubwa wakifanya hand pumping, mashine ilikuwa imeshashindwa kazi.

Nilianza kuchant mantras za mwisho mwema. Nkachant Krishna, nikachant kuan ing pussa. Dakika kumi baadae akapumzika kwa amani. Hana mateso tena. Tunafanya makosa mengi na kushindwa kuwasidia wapendwa wetu kukata roho salama. Kumbuka hata sekunde zile za mwisho unaweza kumsaidia marehemu akawa na mwisho mwema. Kuna vita ya kiroho muda ule, kuna uvutano wa hasi na chanya, kuzimu na mbingu.

Ukiwa mtulivu unaweza kumsaidia asiende upande mbaya I mean roho yake. Sanasana ni roho kutoka na kwenda kuripoti kwenye makazi yake asilia kisha kurudi kwenye makazi yake duniani. Tunaita blissful state. Ukikosea kidogo ana hata yeye mwenyewe basi roho yake huwa ya kutangatanga bila ya kuwa na kikao maalum na kuleta shida kubwa.

Ibada za mwisho kabla ya kukata roho ndio tunazozifahamu zaidi, lakini tukumbuke kuna ibada nyingi tofauti ambazo huwa msaada mkubwa kwa marehemu. Sehemu nyingi za ajali na majanga, tunapoona watu wakikata roho ni sehemu sahihi za kufanya ibada za binafsi sirini, ibada za kuingia ulimwengu wa roho kimyakimya kwenda kutoa msaada wa kuomba njia sahihi kwa wale wafao.

Najua sijaeleweka ngoja jukwaa letu lianzishwe tutaeleweshana zaidi

Jr
Siku hizi unajua kujigeuza kua "Nafsi isionekana"?
 
Kwa muktadha wa Bible takatifu uko sahihi kabisa na nakubaliana nawe kwa asilimia mia moja lakini dunia hii ni zaidi ya uijuavyo
Kuna imani nyingi kuna dini nyingi na nyingine ni za ajabu hasa.... Nakushauri jifunze tu ujue lakini si lazima uamini au u practice... Mungu akurehemu

Jr
Mkuu hata kibiblia hayuko sahihi. roho haifi na ipo mifano mingi sana juu ya hili ukiwemo ule wa Lazaro na tajiri. Lakini pia Eliya na Musa kumtokea Yesu mlimani tukio lililoshuhudiwa na wanafunzi wake watatu.

Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo tunaona roho zilizochinjwa chini ya madhabahu mbinguni zikimlilia Mungu kisasi juu ya waliojuu ya nchi. Kasome uone jinsi walivyokirimiwa huku wakisubiri ule mwisho.

Lakini hicho hicho kitabu cha ufunuo kinasema kimeshuhudia sanduku la agano la kale mbinguni hekaluni! Unafikiri hilo sanduku la agano ni lile box? Ni bikira Maria ambaye ndiye aliyekuwa fumbo la sanduku la agano na akitaka nifafanue zaidi kuwa sanduku la agano ni kivuli juu ya habari ya bikira Maria naweza (agano la kale ni kivuli cha agano jipya lazima uvisome pamoja kupata ujumbe timilifu wa Mungu).

Hivyo wengi wanachanganya ufufuko wa miili wakifikiri na roho zinakufa. Hata Yesu mwili ulikufa ila Roho yake ilishuka hadi kuzimu kwa siku tatu! Wenzetu waliokufa wapo hai, kama ni watakatifu wanaweza kutuombea lakini kama si watakatifu hawawezi kutuombea kama jinsi tajiri kwenye mfano wa kisa cha lazaro alivyokataliwa ombi lake na ibrahim!

Wengi wana nukuu lile andiko kuwa mtu akifa hajui kitu, ni lina fafanuliwa vibaya bila kusoma maandiko kwa ujumla. Mungu mwenyewe anasema yeye si Mungu wa wafu bali Mungu wa walio hai, Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, je akina Ibrahim hawajafariki? Swala la uhai na kifo kibiblia si jinsi tunavyotafsiri kibinadamu.
 
giphy.gif

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom