Uchaguzi 2020 Namkubali Dkt. Magufuli, siikubali CCM lakini ni propaganda potoshi kumuita Lissu kibaraka wa Wazungu

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,584
15,354
Nimekuwa nikimfuatilia Lissu kabla na baada ya tukio la kujeruhiwa.

Wengi wanaompinga kwa kisingizio cha ukibaraka wenda wanafanya makusudi, au wanataka kuwaokota watu wasio na ufahamu au ni kukidhalilisha chama cha Mapinduzi kwa kutumia mbinu za kizamani.

Zamani za CUF tulitishiwa udini.
CHADEMA na slaa tukaambiwa vita na machafuko.
Lowasa fisadi huku Mahakama ya mafisadi ikibaki inapiga mihayo bila wateja.

Leo Lissu Jamii inaaminishwa ni mtu Hatari na Kibaraka Mkubwa wa wezi wa madini, wazungu na mabeberu kwa Aina zao.

Kwa CCM hii ni Kete nzuri ya kuhadaa wananchi lkn miaka ya 2015 kurudi nyuma sio Leo.

Wengi tunataka facts sio porojo.

Napenda kumpinga sana Lissu, na niliumia aliposadikiwa kupigwa risasi, nilimuombea sana apone haraka ili nimpinge akiwa mzima kwa facts ila hilo la kumuita kibaraka sio sawa.

Mnamuonea wakuu
 
Propaganda za kizamani sana hizi
Zinaliabisha Taifa. Tunaonekana wote hamnazo.

Mbona kuna mambo mengi tubya kumpingia Lissu.

Kwanza adui wa taifa sio beberu. Ni ujinga maskini, maradhi CCM inauzoefu na hawa maadui. Kuongeza Beberu na kupakazia watu ni kukwepa Majukumu au kukwepesha vita
 
Ile tu AMSTERDAM kumtolea matamko Lisu juu ya uchaguzi inaonesha ni jinsi gani alivyo kibaraka!

Kwani ulitaka ajioneshe wazi wazi kama yeye ni kibaraka?

Au unafikir mabeberu wanatumia watu wajinga kuwa vibaraka wao?
 
Mkuu dunia kijiji. Kama haivunji Sheria hata tamko litoke mwezini haina shida.

Thibitisha pasiposhaka tushirikiane kumkosoa na ubeberu wake.
Propaganda hiyo ni ya kichovu sana aisee
 
Na wote hamnazo kweli kwani uongo mmekaa kinafiki nafiki tu na mitunguliyenu

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu dunia kijiji. Kama haivunji Sheria hata tamko litoke mwezini haina shida.

Thibitisha pasiposhaka tushirikiane kumkosoa na ubeberu wake.
Propaganda hiyo ni ya kichovu sana aisee
Mkuu, Lisu ni kibaraka wewe jua hilo...

Hivi Amsterdam anakuwa msemaji wa Lisu juu ya uhuru wa NEC kama nani hasa katika nchi hii?

Tunajua ni mwansheria wake kwa yaliyomsibu sawa. Lakini huku kwenye uchaguzi yeye kama nani hasa?
 
Ukiishiwa na sera ndo unabakia na vitisho vya kizamani tu,zanzibar chaguzi zote wanatishia watu nyau ya cuf itarudisha waarabu,ni kufanya watu mataahira tu
 
Ile tu AMSTERDAM kumtolea matamko Lisu juu ya uchaguzi inaonesha ni jinsi gani alivyo kibaraka!

Kwani ulitaka ajioneshe wazi wazi kama yeye ni kibaraka?

Au unafikir mabeberu wanatumia watu wajinga kuwa vibaraka wao?
Una ushahidi? Wenye ku support hoja zako kuwa ni kibaraka?na nazumzia ushahidi concrete
 
Sio lazima kuikubali ccm. CCM ni chama kama vyama vingine tu. Kuvikataa au kukubali ni choice ya mtu binafsi.
Si kwamba anatumika. Hayo ni matakwa ya mtu binafsi
Aah wapi, wewe itabidi umulikwe sawasawa,yaani unachukia chama kilichokukuza na kukusomesha kweli?
 
Back
Top Bottom