Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,059
- 2,499
Nchi za Namibia na Botswana zinatarajiwa kuwa na kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta( Oil Refinery) ili kupunguza kiwango cha mafuta wanachoagiza kutoka nje.
Hatua hiyo imetajwa ikiwa ni baada ya ziara ya Rais wa Namibia nchini Botswana.
Pamoja na kupunguza uagizaji wa bidhaa za mafuta kutoka nje , kiwanda hicho pia kitakuwa chanzo kipya cha mapato kwa nchi hizo zinazojitahidi kupunguza utegemezi wao kwa almasi ambayo inakumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa almasi zinazotengenezwa maabara.
Nchi za Botwana na Namibia zimegundulika kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta na zinategemea kuwekeza katika sekta hiyo kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi.
CHANZO: BUSINESS INSIDER AFRICA