Kiwanda kikubwa cha Dangote Cha kusafisha mafuta Kujengwa East Africa.

Kiwanda kikubwa cha Dangote Cha kusafisha mafuta Kujengwa East Africa.

Xmonster

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2020
Posts
1,646
Reaction score
2,387
Bilionea Aliko Dangote ametangaza mpango wake wa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta (refinery) Afrika Mashariki.Tanga, Tanzania

Akizungumza katika mkutano wa Africa We Build Summit 2026 uliofanyika Nairobi siku ya Alhamisi, Dangote alisema kuwa kiwanda kinachopendekezwa kitakuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku, sawa na uwezo wa kiwanda chake cha Dangote kilichopo Nigeria.
Rais wa Kenya, ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo, alisema Afrika Mashariki kwa sasa inaagiza bidhaa zote za mafuta yaliyosafishwa, hasa kutoka Mashariki ya Kati. Hali hii inaweka eneo hilo katika hatari ya kukatika kwa upatikanaji wa mafuta na kupanda kwa bei.
“Tutaanzisha kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta huko Tanga kwa manufaa ya wote, kwa sababu kiwanda hicho kitapokea mafuta kutoka Democratic Republic of Congo (DRC), Kenya ,South Sudan,Uganda ,”
 
Kwa nchi mwenyeji bado hakuna positive impact kwa wananchi isipokuwa kwa mafisadi ambao watahakikisha bei iko juu kama ilivyo tu kwa sukari, gesi na hata magari ambayo tunaingiza kwa bei kubwa kuzidi nchi kama Rwanda, Uganda na Burundi ambao hawawana bandari na wanayasafirisha umbali mrefu zaidi kuliko Watanganyika.
 
Kumbf D.R.C wana adi mafuta asee yaani neema za madini kwao ni laana na mikosi
 
Back
Top Bottom