Namfananisha JPM na Salmin Amour

Namfananisha JPM na Salmin Amour

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
19,364
Reaction score
68,454
Wengi mnamkumbuka aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Salmin Amour kwa utawala wake wa mkono wa chuma, kiasi cha kupachikwa jina la 'Komandoo'

Wapinzani wake walikiona cha mtema kuni, hadi baadhi yao waliwekwa kizuizini kwa kosa la Uhaini.

Sasa naiona Nchi yangu ikiwa imepata Salmin Amour "mpya" kwani kitabia Rais mteule naona anarandana kabisa na Kamandoo wa Zanzibar ile.

Hakika tutakuja kumkumbuka sana JK kwani tulikuwa na uhuru uliopitiliza mpaka tukajisahau, magazeti yaliandika yalivyotaka, tulimsema na kumkosoa tulivyojisikia. Lakini kwa awamu hii ya tano, chonde chonde jamani, kila abiria achunge mzigo wake.
 
COVID-19 INATISHA NIPO HOME
 
Hapana uyu ni rais mshauri wa dunia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Uzi ulikosa wachangiaji sababu time huu uzi unaandikwa Jamaa alikuwa kabeba matumaini makubwa sana ya watanzania,mimi hadi kufikia 2016 mwezi wa tano bado nilikuwa namuona jembe kwelikweli tena hotuba alikuwa akitoa watu wanajazana kwenye tv kusikiliza nini kasema akimaliza ni shangwe tu alikuwa akiongea na msisitizo tukamuona mzalendo
Ila......Ila..........tumejionea wenyewe...MIAKA 5 MIBOVU KABISA,SUCH A WASTE utadhani tupo kwenye kambi ya mateso,KWANI LAZIMA YEYE NDO AWE RAIS?BORING
 
"Watanzania muniombee". Hilo ndio jibu la dua zetu.
 
Amewatoa machozi ya uchungu wa Tz, kuanzia mijini mpaka vijijini, chama tawala mpaka wapinzani, nafikiri huyu Mungu aliruhusu apate iwe shule kwa watanzania wote kutidhia katiba mpya endapo nafasi itajitokeza tena. Mateso haya ni kwa sababu ya kuwa na katiba isiyoweza kumdhibiti Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlimuita Kikwete anacheka cheka,na yeye akaamua kuwaletea mtu asiechekacheka kwa sababu hamkutaka anaechekacheka,sasa twendeni kazi kwanza,mengine tutasemezana taratibu mbele ya safari.
 
Ulishindwa nini kutabiri ujio wa Coronavirus??
 
Back
Top Bottom