Kwa ufupi
Mtafaruku huu umekuwa tukiambiwa unatafutiwa ufumbuzi kwa kufanyika kwa njia ya mazungumzo ambayo yametawaliwa na usiri uliosababisha kutoa tafsiri ya kukwama.
By Salim Said Salim
Zanzibar iliyogubikwa na mtafaruku wa kisiasa kufuatia kufutwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu inaadhimisha miaka 52 tangu kufanyika mapinduzi, Januari 12, 1964.

Mazungumzo haya yamewakutanisha ana kwa ana wagombea wawili wakuu kwa uchaguzi wa rais. Nao ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ambaye kikatiba muda wa Serikali yake na aliyekuwa Makamu wake wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad ulifikia kikomo Novemba 2.
Hata hivyo, Dk Shein anaendelea kuongoza Serikali ambayo sasa ni ya chama kimoja cha CCM badala ya kuwa ya umoja wa kitaifa baada ya washirika wenzao wa CUF, akiwamo Maalim Seif kukaa pembeni kwa maelezo kuwa hawapaswi kuendelea kushika nyadhifa hizo kikatiba kwa vile muda wa maisha ya Serikali hiyo umekwisha.
Viongozi wastaafu wa Serikali ya Zanzibar, Muungano na wawakilishi wa kimataifa, akiwamo Rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan, aliyepewa kazi ya usuluhishi na Jumuiya ya Madola wameshiriki katika mazungumzo hayo kwa nyakati tofauti kutegua kitendawili hicho.
Kwa sasa wakati sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi zikiendelea, lakini siyo kwa kishindo na mvuto kama ilivyokuwa miaka iliyopita kutokana na mvutano kati ya CCM na CUF, haijulikani kilichopatikana au kukosekana katika mazungumzo hayo yaliofunikwa na usiri mkubwa.
Zanzibar njia panda
Kwa muhtasari wa Wazanzibari wanaadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi wakielewa walipotoka na walipo, lakini hawajui wanaelekea wapi na watarajie nini katika mvutano huu wa kisiasa ambao mbali ya kuigawa Zanzibar vipande viwili, umezusha hofu ya usalama na kutengwa kisiasa na kiuchumi na washirka wake wakuu wa maendeleo, miongoni mwao nchi za Marekani na Umoja wa Ulaya.
Hofu nyingine iliyopo ni uwezekano kwa washirika wengine wa maendeleo wa Zanzibar, hasa nchi za Kiarabu nazo kama hazikuitenga Zanzibar basi huenda zikapunguza kasi yao ya kutoa misaada.
Kwa vyovyote vile uamuzi wa kufuta uchaguzi uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, umeipa Zanzibar mtihani mwingine katika historia ya miaka 52 ya Mapinduzi na kwa upande mwingine kuutikisa muungano wake na Tanganyika ulioundwa miezi mitatu baada ya kufanyika mapinduzi.
Tayari Rais John Pombe Magufuli aliyeingia madarakani baada ya uchaguzi uliofanyika pamoja na ule wa Zanzibar katika mazingira sawasawa, ameshaanza kuwekewa ngumu na baadhi ya mataifa yakiongozwa na Marekani kwa kuzuia fedha za misaada kwa miradi ya maendeleo.
Hali hii ni mtihani mgumu wa kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia kwa Magufuli na kwa kutumia kauli yake maarufu, kilichopo Zanzibar ni “ Hapa kazi tu”, tena ngumu na pevu.
Kinachoonekana ni kwa Magufuli kuwa hana wa kumsaidia na zipo taarifa kwamba juhudi za Serikali yake isinyimwe misaaada na ipewe muda kushughulikia suala la Zanzibar zimegonga mwamba.
Taarifa za kidiplomasia zinadai kwamba jibu lililotolewa na baadhi ya washirika wa maendeleo ni kwa wao kutaka wapewe muda kufikiria kutoa fedha za kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo wakati wakisubiri hatima ya Zanzibar.
Marekani na washirika wengine wa maendeleo ya Zanzibar wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa mchakato wa uchaguzi kuendelea na mshindi kutangazwa, lakini pia kusikitishwa na taarifa za vitendo vya ukiukaji wa haki za binaadamu vilivyoshuhudiwa kabla na baada ya uchaguzi visiwani.
Hii ni pamoja na madai ya wapinzani na taarifa za vyombo vya habari juu ya kile kilichoelezwa kama matumizi mabaya ya vikosi vya ulinzi vya Muungano na vya Serikali ya Zanzibar katika siasa za visiwani.
Vitendo vya watu kupigwa hovyo mitaani na majumbani na mashambulizi ya vyombo vya habari, ikiwa pamoja na kuchoma kituo cha radio binafsi ya Hits FM vimetoa taswira mbaya kwa Zanzibar wakati huu ikiadhimisha miaka 52 ya mapinduzi yaliyoung’oa utawala wenye asili ya Omani wa Sultani Jemshid Abdulla El-Busaidy.
Historia ya Mapinduzi
Mapinduzi yalipofanyika watu zaidi ya 500, wakiwamo wanawake na watoto, waliuawa kwa kupigwa mapanga, mashoka, mikuki na bunduki katika Kisiwa cha Unguja, lakini hali ilikuwa shwari huko Pemba.
Watu zaidi ya 2,000 waliwekwa kizuizini na wengine gerezani bila ya kufunguliwa mashtaka.
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 tangu kufanyika mapinduzi, Zanzibar iliendelea kuwa katika hali iliyoshuhudia watu wengi kuuawa kwa kudaiwa kuhusika katika njama ya kuipindua Serikali.
Mara baada ya mapinduzi mamia ya watu walifukuzwa Zanzibar na kupelekwa au wenyewe kwenda nchi za Kiarabu, Comoro na India au kukimbilia Bara, nchi jirani, Ulaya, Marekani na Canada kutafuta usalama au kuanza maisha mapya.
Serikali iliyopinduliwa ilikabidhiwa madaraka na Uingereza iliyotoa uhuru kwa visiwa hivi Desemba 10, 1963. Kila pakifanyika sherehe za mapinduzi familia nyingi za watu wa visiwani na jamaa zao waliopo nje huwa katika maombolezo ya kupoteza wazee, ndugu na marafiki.
Wengi wao hawajui jamaa zao waliuawa katika mazingira gani na wapi miili yao ilifukiwa.
Taarifa za kufanyika mapinduzi zilipatikana asubuhi ya Januari 12 kupitia Sauti ya Unguja, siku hizi inaitwa Zanzibar Broadcasting Corporation (ZBC). Aliyesoma taarifa hiyo alikuwa mmoja wa waasisi wa Afro Shirazi Party (ASP), Mdungi Ussi, aliyeuawa miaka michache baadaye kwa tuhuma za kupinga mapinduzi aliyofurahia kufanyika kwake akiwa madarakani mwaka 1964.
Tangazo hilo lilifuatiwa baada ya kila dakika chache na vitisho vilivyotolewa na John Okello, raia wa Uganda aliyehamia Zanzibar na kufanyakazi za kibarua.
Mpaka wiki chache kabla ya mapinduzi, Okello alikuwa fundi muwashi mjini Unguja na kabla ya hapo alikuwa akivunja mawe Micheweni, Kaskazini Pemba.
Aliletwa Unguja kutoka Pemba na rafiki yake, Ali Lumumba, ambaye alikuwa miongoni mwa waliovamia kambi ya Polisi ya Ziwani (siku zile ikijulikana kama Bomani) kufanya mapinduzi usiku wa Januari 11, 1963.
Mzee huyo aliyefariki dunia akifanyakazi ya kuosha magari eneo la Welesi, mjini Unguja, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa chama cha CUF kutokana na kuamini malengo ya mapinduzi yalipotoshwa na kusikitishwa na ubaguzi waliofanyiwa Wapemba.
Okello ambaye msaidizi wake alikuwa Absalom Engine, raia wa Kenya, aliamuru kukamatwa mawaziri wa Serikali iliyopinduliwa na kukataza watu kutembea usiku.
Baadaye wote wawili walifukuzwa Zanzibar bila ya maelezo na taarifa zilizofuata zilieleza kuwa waliwekwa mbele ili kama mapinduzi yasingefanikiwa ionekane waliotaka kupindua ni wageni.
Karume alishiriki?
Baadhi ya wanasiasa wakongwe wa ASP wamesema mzee Abeid Amani Karume aliyekuja kuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar ndiye aliyeongoza mapinduzi. Upo uthibitisho, pamoja na wa mke wake mama Fatma, kuwa mzee Karume alikuwapo Unguja yalipofanyika mapinduzi, lakini yapo mashaka kama alijua kwa undani mpango huo.
Mzee Karume alikwenda Dar es Salaam siku ya pili baada ya kufanyika mapinduzi kwa kuhofiwa kukamatwa kama mapinduzi yasingefaulu.
Karibu kila siku kabla ya kufanyika mapinduzi nilimuona mzee Karume kwa vile nyumba yake na ile niliyozaliwa mpaka leo zinatazamana katika Mtaa wa Kismamajongoo, mjini Unguja.
Mapinduzi yalipofanyika nilikuwa ninakaribia miaka 18 na nilimuona mzee Karume asubuhi ya Januari 10 akinywa kahawa kwa mzee wa Kiarabu, Sheikh Salim (jina lake la utani Mtefutef, yaani mtu asiyeeleweka) katika baraza iliyokuwa karibu na nyumbani kwetu na nyumba ya mzee Karume.
Siku ile Karume akiwa na majirani na marafiki zake, mjomba wangu marehemu Suleiman Omar Kombo, marehemu Aboud Maalim na marehemu baba yangu alininunulia kashata mbili na kuniambia moja yangu na nyingine ya mdogo wangu.
Nilimuomba mzee Karume aniazime baiskeli yake ya aina ya Raleich na alinitaka nikachukue ya mjomba wangu aliyeishi nyumba iliyokuwa nyuma ya baraza la kahawa.
Wapo waliosema mwanasiasa aliyehusishwa na kuuliwa Karume mnamo Aprili 7, 1972 na kushtakiwa kwa uhaini, Abdulrahman Babu, alikuwa miongoni mwa waliopanga mapinduzi, lakini Babu alikuwa Dar es Salaam mapinduzi yalipofanyika.
Baada ya Karume kuuawa Mwalimu Julius Nyerere alimuweka Babu kizuizini katika gereza la Ukonga katika eneo wanaokaa watu waliohukumiwa kunyongwa.
Itaendelea wiki ijayo.
http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Miaka-52-ya-Mapinduzi-Zanzibar--hatma-ya-mkwamo-wa-kisiasa/-/1597592/3007468/-/etjplbz/-/index.html
Wednesday, December 30, 2015
Miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar, hatima ya mkwamo wa kisiasa
Kwa ufupi
Miongoni mwa watu waliouawa baada ya kupelekwa Zanzibar ni Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi, Abdulla Kassim Hanga na Othman Sharif, msaidizi wa karibu wa mzee Karume katika uongozi wa ASP.
Juma lililopita makala haya yaliishia ‘Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume kuuawa. Mwalimu Nyerere alimweka kizuizini mmoja wa watu waliotuhumiwa kupanga Mapinduzi, Abdulrahman Babu’. Endelea.

Karume na Babu walirudi Zanzibar kutoka Dar es Salaam siku ya pili kwa boti ya Myahudi aliyemiliki Hoteli ya Silversan iliyokuwepo Kunduchi na kufikia Kizimkazi, Kusini Unguja.
Niliwahi kumuuliza mzee Mtoro Rehani Kingo, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa ASP na Meya wa kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi ili kujua aliyepanga na kuongoza.
Sababu ya mapinduzi
Mzee huyu aliyekuwa mlezi wa klabu yangu ya soka ya Ujamaa, iliyojulikana kama Wolverhampton Wanderers aliniambia:” Lengo lilikuwa kufanya vurugu ili ulimwengu uelewe hatutambui uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Desemba, 1963. Lakini ilipoonekana njia nyeupe ndiyo ikaamuliwa kufanya mapinduzi.”
Maelezo juu ya mapinduzi yalivyopangwa ni ya kutatanisha. Mashambulizi ya kuteka vituo muhimu hayakupata upinzani mkubwa isipokuwa katika kituo cha polisi cha Malindi, mjini Unguja.
Hapo kazi ilikuwa pevu na watu wengi waliuawa mpaka waliposhiriki vijana wa Chama cha Umma kilichoongozwa na Babu baada ya kuihama ZNP. Vijana hawa baadaye walikuwa miongoni mwa washtakiwa katika kesi ya uhaini ya kumuua Karume.
Wengi wao walikuwa maofisa wa Jeshi la wa Wananchi wa Tanzania (TPDF) na baadhi yao walipata mafunzo ya kijeshi katika jangwa la Sinai, Misri, kabla ya Mapinduzi na Cuba na Urusi baada ya Mapinduzi.
Askari polisi waliokuwa watiifu kwa utawala wa sultani waliokuwepo Malindi baada ya kuishiwa nguvu walikimbilia bandarini na kuondoka na mfalme kwenda Dar es Salaam na baadaye Uingereza wakiwa wakimbizi wa kisiasa.
Baadhi yao siku hizi hufika Zanzibar kutembelea jamaa zao, lakini Jemshid licha ya Rais mstaafu wa Zanzibar, komandoo Salmin Amour, kumwambia rukhsa kutembelea Zanzibar, hajafanya hivyo. Ila baadhi ya jamaa zake wanafika Zanzibar kwa ziara za siku chache na baadhi yao wamenunua nyumba kwenye fukwe za bahari.
Baadhi ya wanafamilia ya Jemshid ni marafiki wa viongozi wanaojiita Wana mapinduzi waliopo serikalini na wengine hufika majumbani kwao wanapokwenda Omani kwa matembezi au ziara za kiserikali.
Kwa nini Oman ni mshirika wa Z’bar
Omani ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Zanzibar hasa katika sekta za afya, elimu na miundombinu.
Hii inatokana zaidi na maofisa wengi wa ngazi za juu wakiwamo makatibu wakuu na wakurugenzi wa Serikali ya Oman ama wenyewe au wazazi wao kuzaliwa Zanzibar.
Idadi ya watu waliouawa yalipofanyika mapinduzi na miaka michache iliofuata haieleweki kwa uhakika. Kila mmoja anasema vyake, lakini ni kubwa na wamo wanasiasa, viongozi wa serikali, dini, wanawake na watoto. Hata wazee na watu waliokuwa akili zao hazipo sawa walikula shaba kwa kuonekana wanapinga Mapinduzi.
Ninakumbuka mkasa wa bibi mmoja kizee wa Baraste Kipande aliyekuwa mgonjwa wa akili alivyopoteza maisha yake mikononi mwa hao waliojiita wanamapinduzi waliozunguka mitaani na bastola viunoni kama wababe wa sinema wa michezo ya Marekani.
Huyu bibi alipowaona maofisa wa Usalama wa Taifa wakiranda mtaani na bastola zao aliwaita kwa kelele kwakuwaambia: “Niko hapa eeh…”
Wale jamaa walikasirika na kumchukua Baada ya siku mbili, Hanga (ambaye alikuja kuuawa katika mazingira yasiyoeleweka, alifika mtaaani kumtembelea mzee mmoja aitwaye Yusuf Jaha (maarufu kwa jina la Sir George Mooring. Mzee huyu alipewa jina hili kutokana na kumpenda mwakilishi wa mwisho wa Serikali ya Uingereza kabla ya uhuru, Arthur George Rixon Mooring.
Nilimwambia Hanga ambaye alinisomesha Shule ya Msingi ya Mashimoni (hapo ulipo Uwanja wa Mao De dung) aliyefika hapo kwa miguu na kutukuta tunacheza karata na walinzi wake wakiwa pembeni wanakunywa kahawa kuwa kile kizee kilichukuliwa na Wana-mapnduzi kwa kuwaambia: “Niko hapa eeh”.
Hanga aliniambia hata mzee Miraji Othman (baba yake marehemu Profesa Haroub Othman) aliyemtembelea kabla ya kufika hapo alimpa taarifa hiyo na ataifuatilia.
Mzee Miraji alikuwa mwanachama wa ASP wakati wa kupigania uhuru na rafiki wa Hanga na Karume. Lakini mke wake, Bibi Fatma Abubabakar Jamalil Leyl, alikuwa mwanachama na mwana harakati wa Hizbu.
Karibu kila Jumamosi mzee Miraji alihudhuria mikutano ya ASP iliyofanyika Rahaleo (kwenye uwanja wa kituo cha ZBC) na usiku ule ule Fatma alihudhuria mikutano ya Hizbu iliyofanyika Darajani baada ya saa 2 usiku.
Hata watoto wao waligawika kushabikia vyama hivi, lakini hawakugombana. Tulichojifunza vijana wa mtaani ni kuvumiliana kisiasa kwa hawa wazazi wa Profesa Haroub na kuishi bila ya ugomvi.
Kilichonivutia ni kuwa mbele ya nyumba ya wazee hawa kulikuwa na mchoro wa jogoo (alama ya Hizbu) upande wa kushoto na kulia mchoro wa kisima (alama ya ASP).
Ninamini uvumilivu wa kisiasa aliouonyesha profesa wakati wa uhai wake na kuwataka Wazanzibari wasigombane kama tuonavyo sasa kwa sababu ya siasa ni urithi alioupata kwa wazazi wake, ustahamilivu ambao siku zile na hata leo ni nadra kuonekana miongoni mwa Wazanzibari na Watazania wengi.
Baada ya siku mbili Hanga alifika tena mtaani na kueleza kwa masikitiko:” Hiki kizee hakipo gerezani na nimepata fununu wameshamuua. Sijui tunakwenda wapi”.
Mauaji ya aina hii yalipelekea akina mama wengi kuwa vizuka na watoto kuwa mayatima yaliendelea kwa zaidi ya miaka 15 baada ya Mapinduzi. Huu ndiyo ukweli ijapokuwa wapo wanaojifanya wanamapinduzi mamboleo ambao hawapedi haya yasimuliwe.
Karume aliuawa na mawaziri kadhaa
Hata watu waliokuwa karibu na mzee Karume katika Serikali na ASP, wakiwamo mawaziri na waasisi wa ASP, waliuawa.
Miongoni mwao ni Hanga aliyechukuliwa na makachero wa Usalama wa Taifa kutoka jela ya Ukonga, Dar es Salam na kupelekwa Zanzibar.
Wapo wanaosema safari yake ilimalizikia baharini, lakini kilichotokea hakijulikani kwa uhakika. Mtoto wa Hanga anayeishi Urusi ameulizia sana kilichomsibu baba yake na hajapata jawabu.
Mama yake Hanga aliyekuwa anaishi Miembeni, mjini Unguja na mjomba wake, Ali Ngwengwe, aliyeishi Kikwajuni na baadaye Kariakoo Dar es Salaam, walijitahidi kujua kilichomsibu mtoto wao na hawakupata maelezo mpaka walipoiaga dunia.
Siku moja nikiwa Dar es Salaaam nikiwa Mhariri wa Michezo wa Daily News nilikutana na mzee Ngwenge katika klabu ya Yanga na baada ya mazungumzo marefu nilimuuliza kilichomfanya akimbie Unguja.
Alinipa simulizi za kusikitisha na kuniambia alionywa angeuawa kama angeendelea kuulizia au kuzungumzia kifo cha Hanga ambaye ni mtoto wa dada yake.
Wengine waliouawa ni pamoja na Othamn Sharif aliyekuwa akifanya kazi Iringa kama daktari wa wanyama.
Marehemu, huku akilia, aliwanasihi viongozi wa serikali wa Iringa wasimpeleke Zanzibar na kuwaambia watajilaumu wataposikia ameuawa.
Wengine waliouawa
Wengine waliokuwa mawaziri na kuuawa kikatili ni pamoja na Abdulaziz Khamis Twala (fedha) na Saleh Saadala Akida (Mawasiliano na Uchukuzi). Zipo hadithi nyingi juu ya walivyouawa.
Twala aliuawa pamoja na rafiki yake mkubwa, mzee Majura baba wa mwandishi wa habari maarufu Abdulla Majura aliyewahi kufanya kazi TBC na BBC na sasa anamiliki radio binafsi mjini Dodoma.
Wengine kama nilivyogusia awali ni muasisi wa ASP, Mdungi Ussi (aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Sauti ya Unguja), Abdul Nadhif (katibu mkuu), Salim Jinja, Amour Zahor, Jimmy Ringo na Khamis Masoud.
Viongozi wengi wa dini walikamatwa na kuchapwa bakora na baadaye kwenda Dar es Salaam, Mombasa, Comoro na Arabuni kunusuru maisha yao.
Mara nyingi nimegusia umuhimu wa ukweli kutafutwa kwa sababu huu siyo wakati wa kudanganyana kwa kisingizio cha amani na utulivu! Watu hupaswa kusameheana, lakini ni hatari kwa mauaji kama haya kutochunguzwa.
Kufumbia macho yaliyopita kunaweza kuhusishwa na msuguano wa kisiasa unaoendelea Zanzibar hivi sasa, hasa panapotokea watu kurejesha ubabe wa kupigwa watu ovyo na hata kuuawa na wahusika kutoguswa na sheria.
Kama tunataka kuwa wakweli tunapaswa kukubali kuwa Zanzibar ilishuhudia baada ya mapiduzi unyama usioelezeka na tabu kuamini yaliyofanyika kutokana na watu wake kusifika kwa kuheshimu maisha ya binaadamu.
ITAENDELEA juma lijalo