Namchukia sana mume wangu!

Jamani nilimpenda sana mume wangu, niliijali familia yangu,nilijitahidi kufanya majukumu yangu kama mke na mama kwa furaha kwa ajili ya familia yangu, naheshimu ndoa yangu, niliwachukia watu waliokua walioniletea umbea kuwa mume wangu hajatulia,maana kila nikimuuliza alinijibu ukisikiliza ya watu utaharibu nyumba yetu.nikachagua kumuamini mume badala ya watu,mwezi wa sita tulienda kwao na mume wangu, nikaambiwa na wadogo zake mumeo mezaa watoto wawili na wanawake wengine na sasa hivi anamwanamke mwingine anamsomesha chuo.

Kwakuwa tulienda kule sababu ya matizo mengine sikupenda kuanzisha ya kwangu nikasubiri tumerudi kwetu nikaamuuliza akajibu nikweli na sikutaka kukwambia kwa sababu ya kulinda uhusiano wetu na familia yetu. Nimeumia sana namuona ndo adui yangu namba moja hapa duniani, niliamua tu kuhama chumba,nikamwambia mimi sitahusiana nae tena ila nyumba sihami maana tumejenga wote na ninawatoto watatu na mchango wangu ni mkubwa sana mpaka leo nakatwa mshahara wangu nilikopa banki kujenga hii nyumba.

Kweli sinampango wa kuhusiana nae kimapenzi tena maana huu mwezi wa sita sasa lakini kila ninapomuona hasira inaongezeka. natamani ahamie kabisa kwa hao wanawake zake nahisi namchukia sana. naomba msaada nifanyeje ili huyu mwanaume ahamie kabisa huko kwa wanawake zake,nibaki kwa amani na machungu yangu na watoto. (hii habari nimeambiwa na rafiki yangu kaniomba ushauri msaidieni jamani afanyeje ameumizwa sana.
Tundatamu mwanangu kwanza pole sana. Una haki ya kumchukia huyo kiumbe anayeitwa mumeo asiyejua maana ya kupendwa. Ila rudisha majeshi nyuma ufanye utafiti ujue tatizo lake ni tamaa, malezi au nini? Kwa umri wako bado wewe ni mdogo sana. Ningeshauri umbane akupe sababu zinazoingia akilini badala ya kuendelea kukaa kimya huku ukiumia zaidi. Pia ufahamu kuwa kupata mwenzi mwenye kukufaa ni kama kushinda mamilioni kwenye bahati nasibu. Waweza kumuogopa mjusi ukapata mwingine ukakuta ni mamba ukaishia kufa kwa presha. Kama atakupa sababu zenye mashiko na akaamua kuachana na ufuska wake si haba kumsamehe. Samehe saba mara sabini ila usilee ugonjwa.
 
Kwa watakaobisha na wabishe kwa manufaa yao. Hapa Tanzania kupata mume asiyepiga nje ni mwiko, kwani naweza sema asilimia 99.8 ya wanaume wenye ndoa wanapiga nje. Kwa kuwa sasa hii imekuwa ni kawaida kwa umma nao kina mama wengi wao wanagawa nje kufidia upungufu wa nyumbani. Mtombo mtamu jamani, tunaoa na kujifunga vitanzi bure tu.
 
Ukimchunguza bata hutamla. Siku zote toka enzi za ndoa changa bata alikuwa mtamu kwani, hukutaka kujua anakula nini. Sasa umejua unasusa kumla. It is not worth anything to leave him at this time. Kinachotakiwa hapo ni kumuongezea viungo awe mtamu zaidi na kusahau anachokula. Wewe ndiyo mke bhana, wengine wote vidudu watu.

Wewe na mumeo mnavyoishi ndani ndiyo future ya wanao. Nyinyi mmeshakula chumvi, wao ndiyo wanaiga sasa life style yenu. Je utapenda wawe na mahusiano ya mashaka kama uliyonayo? Usimchunguze tena bata na chokochoko ya simu ya mumeo utachokolewa wewe.
 
Pooole sana bidada!!!

Kwanza kabisa naomba ujiulize swali moja muhimu sana,kwamba,je..ukiamua kuachana na huyo mumeo,kitatokea nn????si kwako tu,namaanisha kwa watoto,ndugu waukuzungukao n.k..n.k....

Nakwambia hivyo kwa kua mimi,personally ni muhanga wa hiyo kitu...When I was 4 years old,baba na mama walitengana,tena ndoa ya kikatoliki(though si kwa kuzaa nje)...mama akaondoka na mdogo wangu wa kike,na mimi nikabaki na baba......my Gosh....ni mateso makubwa sana..tena sana kwa watoto!!!Sometimes nilikuja kuona kama mama hakuwa akitupenda watoto wake kwa dhati ya moyo...huwa najiuliza,aliwezaje kutuacha kwa mtu aliyemuona ni baradhuli???(though baba hayuko hivyo)..nazungumzia kimantiki tuu...kama wewe mama umemuona baba ni fisadi la mapenzi,kwa nini ukubali kuacha watoto wakae hapo bila uangalizi wako...seriously,mapenzi yangu kwa mama yako impaired...sikuwah ku'feel her love....
Kuna uzi mmoja wa Mtambuzi niliwah kidogo kueleza hata mambo niliyopitia pale dingi alipokuja kuoa tena....its terrible life...!!!ACHA KUFIKIRI KUONDOKA,TETEA ULICHOKIPIGANIA FOR ALL THOSE YEARS.
Ushauri wangu ni kwamba,please usiondoke,kuhusu tendo la ndoa,hiyo ni changamoto....wewe ni mtu mzima utajua jinsi ya kufanya,but please for the sake of your kids,DONT LEAVE!!!
Wamama siku zote wasipo'win mapenzi ya watoto wao,huwaumiza sana!!!
Thanks
 
Last edited by a moderator:
Hello,kwanza kabisa bado na kamba mguuni napenda kuwasabahi nyote!!..mgeni humu lakini c kwenye masuala hayo,..naomba atambue hyo dada kwanza hiyo ndoa ilikua halala au halali???....kama ni halali bac hasisahau vile viapo na kanuni za ndoa,cha msingi akubari kufanya huo mtihani kwani ameshajisajiri....!
 
sasa kwanini umehama chumba, nakushauri kitu kigumu sana, narudia kitu kigumu maana najua kama huna moyo wa Ujasiri hutaweza, nasema hivi, RUDI CHUMBANI KWAKO, MPENDE MUMEO, MPE CHAKULA CHAKE MLE WOTE maana kwa kufanya hivyo utamuumiza sana yeye, atajiona mjinga, atajutia japo hata sema kwa sauti ila vitendo vitadhihirisha. <br><br>Kwa kutengana nae ndio umempa sababu ya kuendeleza ujinga wake, una risk maisha yake na ya kwako pia, nielewe Mama ni ngumu lakini badala ya kumchukia wewe jitahidi kumpenda, muulize tatizo ni nini, inaweza kukusaidia ila kumbuka wanadamu ni WAFARIJI WATAABISHAJI, nitaku=PM tushauriane vizuri

huu ni ushauri mzuri my dear, usiache ndoa yako, sana sana utawapa wengine faida..nyie mchumie juani wenzio walie kivulini..ndio ilivyo..ukiondoka tu wengine watakuja tena bila aibu

we samehe na endelea na maisha ya ndoa..yuko wapi huyo mwanaume aliyetulia hapa duniani? labda ukamtolee sayari ya mars..hawa wote wanafanana tabia..ni kupiga moyo konde na kuendelea na safari..hiyo ni sawa na tairi ya gari kupata pancha njiani, unabadilisha tairi mnaendelea na safari..
sio wewe tu my dear, tuko wengi tuna matatizo kama hayo na bado tupo kwenye ndoa, cha muhimu huyo mwanaume aache sasa huo upuuzi wake ili muanze ukurasa mpya..
 
Maisha ni safari ndefu sana, vikwazo vyakila aina hususani katika maisha ya ndoa maranyingi havikwepeki japokuwa ukubwa hutofautiana. Mpe pole sana kwakutendwa huyo bi mdada, mume amemkosea adabu sana hilo ni kosa limeshatokea, watoto watatu nifamilia kubwa tayari wanayo, suala sio kukimbia nyumba wala yeye aondoke. Hapo suala kubwa nikuangalia familia iliyopo italelewa vipi na wazazi wote wawili. Mkalishe chini akupe msimamo wake juu ya mustakabali wamaisha yenu na hao watoto wanje atawalea vipi, na ikiwezekana amwulize iwapo kama bado anampenda au la! kama la, niwapi pamepungua ili kuweza kuweka mambo sawa. Baada ya hapo nendeni angaza kupima VVU, kama majibu yakitoka vyema, kaeni chini tena namjenge mahusiano yenu upya, zaidi zidisha upendo kwa mume wako kwani inabidi ujiulize, nini anafuata huko nje ambacho hakipati kwako? Hujikwatui kama enzi bado hujazaa watoto, labda alikupendea utanashati ulio kuwa nao sasahivi unajiachia, humdekezi kama ulivyokuwa unafanya awali ndomaana kaamua kwenda pembeni? Jitahidi kujichunguza wapi unakosea, rekebisha na muendelee kuwa pamoja mfurahie maisha.
 
Waaminifu kidogo tupo bhana Mpwa
huu ni ushauri mzuri my dear, usiache ndoa yako, sana sana utawapa wengine faida..nyie mchumie juani wenzio walie kivulini..ndio ilivyo..ukiondoka tu wengine watakuja tena bila aibu

we samehe na endelea na maisha ya ndoa..yuko wapi huyo mwanaume aliyetulia hapa duniani? labda ukamtolee sayari ya mars..hawa wote wanafanana tabia..ni kupiga moyo konde na kuendelea na safari..hiyo ni sawa na tairi ya gari kupata pancha njiani, unabadilisha tairi mnaendelea na safari..
sio wewe tu my dear, tuko wengi tuna matatizo kama hayo na bado tupo kwenye ndoa, cha muhimu huyo mwanaume aache sasa huo upuuzi wake ili muanze ukurasa mpya..
 
Jamani nilimpenda sana mume wangu, niliijali familia yangu,nilijitahidi kufanya majukumu yangu kama mke na mama kwa furaha kwa ajili ya familia yangu, naheshimu ndoa yangu, niliwachukia watu waliokua walioniletea umbea kuwa mume wangu hajatulia,maana kila nikimuuliza alinijibu ukisikiliza ya watu utaharibu nyumba yetu.nikachagua kumuamini mume badala ya watu,mwezi wa sita tulienda kwao na mume wangu, nikaambiwa na wadogo zake mumeo mezaa watoto wawili na wanawake wengine na sasa hivi anamwanamke mwingine anamsomesha chuo.
Kwakuwa tulienda kule sababu ya matizo mengine sikupenda kuanzisha ya kwangu nikasubiri tumerudi kwetu nikaamuuliza akajibu nikweli na sikutaka kukwambia kwa sababu ya kulinda uhusiano wetu na familia yetu. Nimeumia sana namuona ndo adui yangu namba moja hapa duniani, niliamua tu kuhama chumba,nikamwambia mimi sitahusiana nae tena ila nyumba sihami maana tumejenga wote na ninawatoto watatu na mchango wangu ni mkubwa sana mpaka leo nakatwa mshahara wangu nilikopa banki kujenga hii nyumba.

Kweli sinampango wa kuhusiana nae kimapenzi tena maana huu mwezi wa sita sasa lakini kila ninapomuona hasira inaongezeka. natamani ahamie kabisa kwa hao wanawake zake nahisi namchukia sana. naomba msaada nifanyeje ili huyu mwanaume ahamie kabisa huko kwa wanawake zake,nibaki kwa amani na machungu yangu na watoto. (hii habari nimeambiwa na rafiki yangu kaniomba ushauri msaidieni jamani afanyeje ameumizwa sana.

Hapo kwenye Bold, ndipo tunakosea wanawake wengi, inaonyesha ulikuwa unafanya mambo mengi hapo nyumbani, wakati ni majukumu yake yeye, ukamdekeza pale alipokwambia hana pesa, kiasi akawa na pesa nyingi ambazo hazina kazi. Ninasema hivyo kwa sababu angekuwa na majukumu mengi kuanzia kutunza watoto, wazazi wake na mambo mengine asingekuwa na uwezo wa kuwa na vimada nje, na wala asingeweza kumlipia ada ya chuo huyo mwanamke mwingine.
Hiyo ni wewe umesababisha kuchukua na kufanya majukumu yasiyo yako, mwachie majukumu yake.

Ushauri

Usiondoke hapo nyumbani
Rudi chumbani kwako ila usimpe sakaramenti takatifu mpaka hasira zitakapokwisha kwa sababu ukiondoka tu unawapa upenyo hao vimada kuhamia hapo, na watoto watateseka sana.
hakikisha kuanzia Ada za watoto, matumizi yote ya hapo home yeye ndiye anafanya.
chochote kikitokea kama kinahusu pesa usigharamie kwa pesa zako msubiri aje umwambie zinatakiwa pesa.

ukifanya hayo atakuwa hawezi kupeleka pesa nje kwa sababu itakuwa haitoshi kutokana na matumizi ya hapo home kuzidi na wala hatoweza kumlipia ada ya chuo huyo kimada wake.

la mwisho sali sana kumuomba Mungu akutulize makali kwenye moyo wako, ukiona hasira penda kunywa maji .
 
Jamani nilimpenda sana mume wangu, niliijali familia yangu,nilijitahidi kufanya majukumu yangu kama mke na mama kwa furaha kwa ajili ya familia yangu, naheshimu ndoa yangu, niliwachukia watu waliokua walioniletea umbea kuwa mume wangu hajatulia,maana kila nikimuuliza alinijibu ukisikiliza ya watu utaharibu nyumba yetu.nikachagua kumuamini mume badala ya watu,mwezi wa sita tulienda kwao na mume wangu, nikaambiwa na wadogo zake mumeo mezaa watoto wawili na wanawake wengine na sasa hivi anamwanamke mwingine anamsomesha chuo.

Kwakuwa tulienda kule sababu ya matizo mengine sikupenda kuanzisha ya kwangu nikasubiri tumerudi kwetu nikaamuuliza akajibu nikweli na sikutaka kukwambia kwa sababu ya kulinda uhusiano wetu na familia yetu. Nimeumia sana namuona ndo adui yangu namba moja hapa duniani, niliamua tu kuhama chumba,nikamwambia mimi sitahusiana nae tena ila nyumba sihami maana tumejenga wote na ninawatoto watatu na mchango wangu ni mkubwa sana mpaka leo nakatwa mshahara wangu nilikopa banki kujenga hii nyumba.

Kweli sinampango wa kuhusiana nae kimapenzi tena maana huu mwezi wa sita sasa lakini kila ninapomuona hasira inaongezeka. natamani ahamie kabisa kwa hao wanawake zake nahisi namchukia sana. naomba msaada nifanyeje ili huyu mwanaume ahamie kabisa huko kwa wanawake zake,nibaki kwa amani na machungu yangu na watoto. (hii habari nimeambiwa na rafiki yangu kaniomba ushauri msaidieni jamani afanyeje ameu

:israel:yani wewe cool down....muoneshe dharau hivyo hivyo.lala chumba kingine,si alizoea chakula cha usiku atakua hapati,kwa kifupi mpotezee lile tabasamu la mwanzo alilokua anapata alikose,nguo zake na shughuli zoooote zinazomuhusu usiguse km atafanya mwenyewe au amtume dada shauri yake aaalaaaaah.mtu unapendwa upendeki ningekua mm ningemfundisha adabu,sipigani wala simtukani ...nikikaa sitting full kuchat,simu za hapa na palee ili mradi tu ajue kuwa ht mimi kuna watu wananimendea sema kwa kumuheshimu yy na ndoa yangu ndo maaana sitoki nje..outings natoka km kawa ikiwezekana namuacha ndani ila tu usichelewe kurud ukarudi usiku wa manane mmm mmh..we mwanamke lolote laweza tokea...weekend km yuko home sishindi nae ntaenda vishoping vya hapa na pale au matembez na wanangu...kwakifupi NTAMTENGA mpk ashike adabu yake,kunifukuza hawezi nyumba ni yetu soote..mijanaume mingine banaaa
 
Mdada Sikia Ushauri huu Ndugu yangu...Kubali kujishusha Sana Kwa Mumeo..Ujue Si ni Binadamu,unapojishusha,lazima Mwanaume ajione Mjinga Tuu,hata kama Hatasema...Ila ukijifanya wewe ni Mbabe,hakika hutopata Amani katika Maisha yako..Pia Mpe Style nzuri za Mapenzi Mumeo..Kukimbia kitanda,sidhani kama ni Suluhisho la Matatizo yako..Mwenzako anaendelea Kula Uloda na watu tofauti tuu kwa raha zake..Tena anashukuru sana,kwani hatachoka sana Kimapenzi,kwani yuko Huru..

Kumbuka kuwa,wewe umeshakuwa Mama kwa Sasa,na Soko lako kwa wanaume,kwa hakika Limekuwa Dogo,kama sio kwisha Kabisa...Mdada,kuwa Na Maamuzi magumu ya Kujishusha kwa Mumeo.lazima ataajiona Pimbi tuu...Katu katika Maisha,huwezi kushindana na Mwanaume..

Kumbuka kuwa,hata kama Utaondoka ktk Ndoa yako,amini kwamba,utakuwa Shangazi siku moja..Yaani utakuwa uanfugaa Watoto wadogo wa Kukuridhisha kimapenzi,kwani nawe ni Binadamu,unahitaji Nahiiiiiiii....

Acha upimbi Mdada,jishushe kwa Mumeo wewe,mumeo mpaka kutoka nje,inawezekana humridhishi Kimapenzi wewe,au kama ni asili yake,basi Jishushe kwake,usikubali kushindana naye kwa kutaka kumkomoa kwa kumnyima Unyuma..

Kwa wasio oa au kuolewa...Kaeni kwenye Uchumba kwa muda ambao mtakuwa Mmeshajuana Vizuri sana...Mdada huyu inawezakana alikurupuka tuu kuolewa kwa Nia ya kupata Sifa kwa Jamii...Kwa hakika hakujua Tabia ya Huyu Jamaa,ndio maana anajutia hivi sasa...Pole mdada,AMANI YA NDOA INATATULIWA KWA WANA NDOA WENYEWE,NA SI MTU MWAINGINE!!!!!
 
hii kitu imani mbaya sana,ukimwamini mtu kosa,usipomwamini ni kosa pia!
 
ni kweli mume wako amefanya kosa tena kubwa lakini watu wengi tunashindwa kuelewa kwamba reaction tunazomfanyia mtu aliyefanya kosa pia ni kosa jingine tena kubwa zaidi hata lile lililofanywa awali.kitendo cha wewe kwenda kulala chumba kingine ina maana uhusiano kati ya mke na mume umeanza kufa/au haupo kabisa,hivyo basi kwa hali yeyote mnakaribisha mazingira ambayo yanaweza kuleta madhara makubwa baadae kama familia kusambaratika,watoto kukosa malezi mazuri kutoka kwa baba na mama,HIV ikiwa mmoja kati yenu ataona mwenzake hana muelekeo wa kujenga upya kilichoharibika nk nk.

kitu cha msingi kaeni pamoja myaongee,muombane radhi,msameheane.kama we mwenyewe hauwezi basi shirikisheni wazazi kwasababu kwa ridhaa yao mlioana

naomba MUNGU awasaidie manake so ishu ndogo kama inavyoonekana
 
The best way ambayo ni ngumu kidogo, kuhandle mume aliyecheat ni kuendelea kumpenda, kuwapenda watoto, kuwa msafi wa mwili na roho na chumba chenu cha kulala, halafu muombee. kusamehe hakumsaidii aliyekukosea bali ni muhimu sana kwa afya yako ya mwili na ya kifikra, na kihisia. kumbuka sex pia huwa ni dawa ya kupunguza hasira, so kuamua kuhama chumba, ni kuongeza stress, ambayo inaweza kukuathiri kiafya.
 
Jamani nilimpenda sana mume wangu, niliijali familia yangu,nilijitahidi kufanya majukumu yangu kama mke na mama kwa furaha kwa ajili ya familia yangu, naheshimu ndoa yangu, niliwachukia watu waliokua walioniletea umbea kuwa mume wangu hajatulia,maana kila nikimuuliza alinijibu ukisikiliza ya watu utaharibu nyumba yetu.nikachagua kumuamini mume badala ya watu,mwezi wa sita tulienda kwao na mume wangu, nikaambiwa na wadogo zake mumeo mezaa watoto wawili na wanawake wengine na sasa hivi anamwanamke mwingine anamsomesha chuo.

Kwakuwa tulienda kule sababu ya matizo mengine sikupenda kuanzisha ya kwangu nikasubiri tumerudi kwetu nikaamuuliza akajibu nikweli na sikutaka kukwambia kwa sababu ya kulinda uhusiano wetu na familia yetu. Nimeumia sana namuona ndo adui yangu namba moja hapa duniani, niliamua tu kuhama chumba,nikamwambia mimi sitahusiana nae tena ila nyumba sihami maana tumejenga wote na ninawatoto watatu na mchango wangu ni mkubwa sana mpaka leo nakatwa mshahara wangu nilikopa banki kujenga hii nyumba.

Kweli sinampango wa kuhusiana nae kimapenzi tena maana huu mwezi wa sita sasa lakini kila ninapomuona hasira inaongezeka. natamani ahamie kabisa kwa hao wanawake zake nahisi namchukia sana. naomba msaada nifanyeje ili huyu mwanaume ahamie kabisa huko kwa wanawake zake,nibaki kwa amani na machungu yangu na watoto. (hii habari nimeambiwa na rafiki yangu kaniomba ushauri msaidieni jamani afanyeje ameumizwa sana.
wewe ndo uhame umpishe au uwapishe wenzako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom