Namchukia sana mume wangu!

tundatamu

Member
Nov 26, 2012
12
0
Jamani nilimpenda sana mume wangu, niliijali familia yangu,nilijitahidi kufanya majukumu yangu kama mke na mama kwa furaha kwa ajili ya familia yangu, naheshimu ndoa yangu, niliwachukia watu waliokua walioniletea umbea kuwa mume wangu hajatulia,maana kila nikimuuliza alinijibu ukisikiliza ya watu utaharibu nyumba yetu.nikachagua kumuamini mume badala ya watu,mwezi wa sita tulienda kwao na mume wangu, nikaambiwa na wadogo zake mumeo mezaa watoto wawili na wanawake wengine na sasa hivi anamwanamke mwingine anamsomesha chuo.

Kwakuwa tulienda kule sababu ya matizo mengine sikupenda kuanzisha ya kwangu nikasubiri tumerudi kwetu nikaamuuliza akajibu nikweli na sikutaka kukwambia kwa sababu ya kulinda uhusiano wetu na familia yetu. Nimeumia sana namuona ndo adui yangu namba moja hapa duniani, niliamua tu kuhama chumba,nikamwambia mimi sitahusiana nae tena ila nyumba sihami maana tumejenga wote na ninawatoto watatu na mchango wangu ni mkubwa sana mpaka leo nakatwa mshahara wangu nilikopa banki kujenga hii nyumba.

Kweli sinampango wa kuhusiana nae kimapenzi tena maana huu mwezi wa sita sasa lakini kila ninapomuona hasira inaongezeka. natamani ahamie kabisa kwa hao wanawake zake nahisi namchukia sana. naomba msaada nifanyeje ili huyu mwanaume ahamie kabisa huko kwa wanawake zake,nibaki kwa amani na machungu yangu na watoto. (hii habari nimeambiwa na rafiki yangu kaniomba ushauri msaidieni jamani afanyeje ameumizwa sana.
 

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,710
2,000
Mhhhhhhhhh! Alichokiunganisha Mungu Binadamu na Asikitenganishe!!!!!!! Nitarudi, ngoja nijicosult kwanza kwenda kinyume na bible!!!!!!

Sister Ciello ushauri wako unahitajika huku!
 
Last edited by a moderator:

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,710
2,000
Kuna uzi humu humu MMU wangu wa Mumeo amechit na huondoki, The must Do's embu upitie ule uzi kuna mawazo mengi sana mule. utapata picha!
 

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,786
1,225
Hata kama ni wewe usiogope kusema ni wewe,Kwa ufupi hamna mume hapo ni ugonjwa wa moyo tu,ningesema neno lakini SINA MAMLAKA YA KUWATENGANISHA
 

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
hiyo adahbu uliyompa ishamtosha we kauka tu kwenye hicho chumba ulichohamia ila ungekua mjanja zaidi kama ungehama kitanda within a rum iwe kimyakimya hilo la kuhama chumba watoto watashtuka bana nt gud for them
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Jaribu kupunguza hasira na utafute uwezekano wa kukaa na mmeo muyajadili, maana kwa kiasi fulani inaonekana hata mmeo hapendi ndoa yenu ivunjike. Naamini ni mtu anayeonyeka huyu na akatulia. Sasa hivi kuamua kuachana naye hakutakusaidia wewe wala yeye sana sana utakuwa umewapa faida hao vimada wake. Onyesha kwamba wewe ndiye mwenye mme uliyefunga naye ndoa. Badala ya wewe kukimbia nyumba, watimue hao vimada wake. Ikiwezekana shirikisha watu wa karibu ili wampe karipio. Wazo la kwamba yeye ahame linaweza lisiwe na maana kabisa. Maana kwa hakika hatahama, na yeye anaipenda heshima ya ndoa. Ndiyo maana kila siku anakuja hapo.
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,051
2,000
sasa kwanini umehama chumba, nakushauri kitu kigumu sana, narudia kitu kigumu maana najua kama huna moyo wa Ujasiri hutaweza, nasema hivi, RUDI CHUMBANI KWAKO, MPENDE MUMEO, MPE CHAKULA CHAKE MLE WOTE maana kwa kufanya hivyo utamuumiza sana yeye, atajiona mjinga, atajutia japo hata sema kwa sauti ila vitendo vitadhihirisha. <br><br>Kwa kutengana nae ndio umempa sababu ya kuendeleza ujinga wake, una risk maisha yake na ya kwako pia, nielewe Mama ni ngumu lakini badala ya kumchukia wewe jitahidi kumpenda, muulize tatizo ni nini, inaweza kukusaidia ila kumbuka wanadamu ni WAFARIJI WATAABISHAJI, nitaku=PM tushauriane vizuri
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
Na kuna wenzio wanasali 'eweh shetani waendelee kugombana niendelee kulipiwa chuo'...kazi kweli kweli.

Tukirudi kwenye mada bidada mumeo ulimfuga...hao wambea japo inawezekana walikuwa na nia ya kukucheka walipokuwa wanakupa news za matabia ya mumeo...wewe umekuwa mzembe mara 100 kwa ku ignore habari ulizoletewa...yani mtu mi aniletee umbea afu niupotezee...hell No...lazima niufanyie kazi nijiridhishe; na katu simtaji mbea wangu (hiyo iwe principle maana utamfunga mdomo next time hasemi). Leo hii watakuwa wanakucheka; na nadhani ndio kinakufanya uendelee ku pretend as if everything is okay (kwa kuendelea kuishi nyumba moja na mumeo)

Sasa ungechukua hatua mapema za kumrudi mumeo wala kusingekuwa na watoto huko nje. Huyu mumeo ameshakuwa sugu...watoto wawili vimada tofauti na mwingine analipiwa chuo...mmmhhhh...hapo sina hata ushauri. hata mie ningemchukia aisee.


Eeh mungu tunusuru na ndoa zetu!
 

muhanga

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
873
195
kwani huyo mumeo ni kichwa kusema ukikikata utatembeaje? hebu amua kwa busara, mueleze mapungufu yake kwanza jadilini na bila shaka mtaelewana na kusameheana, hakuna lisilowezekana. lakini ikishindikana amueni muachane tu kuliko kuendelea kupotezeana muda bure.
 

Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,047
0
Moja ya vipindi vigumu apitiavyo mwanadamu, ni kuona mwenzi wake anatoka nje ya ndoa. Iwe mwanamke katoka au mwanaume, haijalishi jinsi, ni wakati mugumu. Wana jf, tutakuwa hatuna maana, kama hatutafarijiana katika nyakati ngumu kama hizi, hasa pale mwenzetu, kwa imani kabisa, anapoamua kutushirikisha magumu kama haya. Hili si la mzaha, kama kweli mwenzetu yamekupata. Kwanza kabisa nakupa pole.
Zaidi ya hapo, naomba nikutie moyo kuwa magumu hayana budi kutupata wanadamu, kwa kuwa taabu zipo ili zitupate.

Imani za kidini zinatofautiana, kwani kwa uislamu, mkataba wao ni wa wake wengi, ila kwa wakristo, mkataba wao ni wa mke mmoja - mme mmoja. Inapotokea mmoja akakiuka, basi hapo huwa anavunja haki ya mwenzake na inauma sana.
Iwapo yamekupata, basi, mwombe Mungu, akupe moyo wa subira, akujalie umsamehe makosa yake, kwani kujitenga naye si dawa. Mungu akujalie hayo.
 

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,787
2,000
Mwambie huyo rafiki yako ajiunge jf ili ashauriwe zaidi. Maana hii c/o siyo nzuri. Amekutuma uje umsemee?
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
45,088
2,000
(hii habari nimeambiwa na rafiki yangu kaniomba ushauri msaidieni jamani afanyeje ameumizwa sana.
Tutajuwa tu kama ni wewe au Rafiki yako, kuna maswali hapa utakavyokuwa unajibu yataeleza yenyewe ukweli kama muhusika ni nani.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
45,088
2,000
Mwambie huyo rafiki yako ajiunge jf ili ashauriwe zaidi. Maana hii c/o siyo nzuri. Amekutuma uje umsemee?
Na wewe kwani mgeni hapa MMU, hiyo ndiyo style yao, kama una la kumshauri wewe mpe tu ushauri huyo ndio muhusika mwenyewe na hakunac/o hapo.
 

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
20,412
2,000
Hii sector ya ndoa ni ngumu sana mwenzi anapocheat,msamehe tu atajutia siku moja
 

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,545
1,250
nadhani pia una tatizo la kutokujiamini,binaadamu yeyote alokamilika na anayejiamini huwa hatumii chuki,hasira na visasi kumweka mwengine mbali nae,hebu ingia ndani yako na uwe wewe halafu jiambie unajiamini uone kama hizo chuki zako zitaendelea kuwepo,kama zikiwepo basi hujiamini mara milioni zote.
 

neggirl

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
4,836
2,000
Daa nimeshindwa kusema kitu as hii inaumiza sana na inahitaji BuSARA unapotoa ushauri.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom