Namchukia mzee wangu!

Namchukia mzee wangu!

Maisha ya wazazi wako siyo maisha yako. Wewe andaa maisha yako na wanao. Usisahau kuwa kulalamika hakubadilishi chochote kwenye familia uliyotoka.

Halafu naona kama familia yenu ina baba bora. Shukuru hata kwa hicho kidogo ambacho mzazi wako alijinyima ili mfanikiwe.

Kamwe usimuone mjinga, siri ya hayo yote anayo na hataki kuwashirikisha. Huenda ni uamuzi sahihi zaidi kuliko kuwashirikisha.

Usichoke kujifunza kuhusu maisha ya kuitwa baba.
 
Nimezaliwa katika familia ya kawaida tu iliyokidhi mahitaji ya msing mwaka 1988. Baba yangu alikuwa mwalimu ila baadaye akaacha bila kutoa sababu za msingi. Sababu yake kubwa ninapomuuliza ni "walikuwa wakinionea wivu na walikuwa wananiroga hasa mkuu wangu wa kazi".

Huwa nachukia nikisikia majibu haya na huondoka upesi kwani naweza hata kumpiga(japo naomba isije kutokea).
Mama yangu ni wale mama wa nyumbani, alikutana na huyu mzee kwenye biashara, alikuwa akiuza viazi vitamu. Ni darasa la saba.

Tangu utoto tumeishi maisha naweza kusema hatukutakiwa kuishi maisha hayo, ukizingatia mzee alikuwa mfanyakazi na from nowhere akaacha kazi.

Najiulizaga mno je, hakufikiria kuwa atakuwa na familia? Je alitoka mwanafunzi na hivyo akakimbia hasira za wanajamii?

Hatukuwahi kulala njaa, tulikuwa tunakula na niseme ukweli toka najitambua mzee alikuwa akitupenda mno kwa kidogo alichonacho, alijitahidi mno wanawe tusipate shida kwa kutupa kila tulichotaka ndani ya uwezo wake.

Alikuwa akitutoa out n.k, katika hili naweza kusema familia yetu ni zile familia za kawaida ila tuliishi maisha ya kizungu huenda kuzidi hata baadhi ya watoto wa matajiri.

Tatizo likaja kwenye nyumba tuliyoishi, ilikuwa mbovu kulinganisha na maisha tuliyoishi. Mzee sijui alikuwa kachanganyikiwa au la, nyumba ndani haina sakafu ni vumbi tu, na wakati huo bado ilikuwa ya nyasi.

Mama alikuwa akimshawishi wakarabati nyumba, alichokuwa anajibu "mtoto anayeona hapa hapamfai basi ahame" (hapo ni tayari ni mtu mzima kidogo najitambua), nilikuwa nachukia na namchukia mno kwa kaulo hizi.

Mbaya zaidi uwezo alikuwa nao kwa wakati huo kwani alikuwa mlinzi wa shirika la serikali fulani, tena wa kudumu wa kuajiriwa na serikali. Nilikuwa naona aibu mno nilipotembelewa na classmates wangu hasa wa kike(nilizidi kumchukia mzee).

Mama alikuwa akisema hutu baba yenu hanishirikishi chochote na hela zake sijui zinaishia wapi, na mzew akiulizwa kuhusu hilo alikuwa mkali mno(kwa hili chuki yangu iliendelea kukua).

Siku moja akaniambia, "mimi nimesgajitoa mhanga na maisha haya, naishi pabovu wakati wafanyakazi wenzangu wana nyumba, nataka nyie wanangu muwe mnaheshimika na mjenge ninyi hizo nyumba bora zenye sakafu kama mnavyodai".

Nilimuelewa kwa kauli hii japo kidogo. Nilimuuliza kama haoni aibu akajibu " sioni aibu ni maisha niliyochagua, kama hamtaki muhame". Nilichukia mno kwa marudio ya kauli hizi.

Sasa ni mtu mzima na nimefanikiwa kidogo ila si kama ninavyotaka, naendelea kupambana.

Mzee katika masuala ya ada alikuwa hasumbui kabisa, alikuwa analipa ada mpaka inabaki change na naidai shule, kwenye mambo ya elimu kwa kweli hakutaka masihara. Ila shida ni maendeleo home ikiwemo nyumba.

Nina kaka zangu wote alipoteza hela nyingi kuwapigania, acha dada zangu pia( japo walipuyanga na hela zilipotea). Katika hili nampongeza kwa 5%.

Simuelewi huyu mzee na namchukia niseme wazi, kwa sababu anasababisha aibu kwa familia, nakumbuka nyumba ndani vumbi yeye anataka kuweka king'amuzi, huu niliona upuuzi tu.

Mfano kuna wakati alishindwa kusave hela za maandalizi ya mimi kuingia chuo, muda umefika wenzangu wanakwenda chuo mimi naranda randa tu home kwenye kibanda kibovu chenye vumbi(shame), halafu tunaanza kuhangaika kuomba omba kwa mkuu wa wilaya na mbunge msaada mimi na yeye, tulikuwa tunatembea ofisi zote na kukumbana na dharau tu(shame).

Nikitakiwa kujiunga jkt mujibu, alininunulia vifaa vyote kama ilivyoelekezwa(nampongeza kwa 10% kwani alinunua vyenye bei na ubora mkubwa), ila kwa nini ashindwe kukarabati nyumba? Ambayo inabeba heshima za mtu?

Nimeaibika mno na inatosha, nilishindwa hata kulete demy ghetto kwa upuuzo huu huu, mazingira mabovu yapo hovyo hovyo... Niishie hapa.

Sitaki kuongea mengi naona nitakufuru na mimi sitaki kukufuru, kikubwa ni hayo tu, jamani nishaurini kwani inafika wakati hata kuonana naye sitaki.

Wewe ndo una shida! Tena sana! Sisi wenzio tumelelewa na wazazi ambao hata hilo darasa sijui la saba hawalijui na hawakufika! Hizo ada unazosema sisi wenzio tulipambana kwa kufanya vibarua nk hadi tukatoboa! Hata kwa hayo yote we are still so very proud of our parents!!! Badala ya eti kuendelea kumchukia baba, pambana wewe na ulete hayo mabadiriko ambayo unayataka na ulikuwa unayatamani hapo nyumbani kwenu!
 
Kama wewe sasaivi una kauwezo kidogo kwanini usimjengee mzee wako hiyo nyumba ya ndoto yako
 
Kuna muda bora upige punyeto yaishe..kuliko kuzaa mtoto ako na akili kama hii
 
Wewe ni kijana mpumbavu babako ni mpambanaji tena tubu na ukamwombe msamaha huyo babako kulipia tu ada,msosi anahitaji tuzo wababa wengine wametelekeza familia kabisa
 
Sasa kumchukia inamaanisha simheshimu? Soma tena!
Wewe ni kenge hakuna tofauti. Huoni tu members karibu wote walivyokuona wewe ni zuzu? Ulitaka baba yako afanye nini zaidi? Kuna zawadi nzuri kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto kuliko elimu? Kama ni nyumba kwanini usikaze misuli ujenge wewe?
 
Nilitegemea kuona labda mzee ni mnyanyasaji, mtesaji lakini maskini baba watu hajaweka sakafu tu.

Kweli kuzaa unaweza zaa kizaazaa..watoto hatuna shukrani
Fikiria hawa ndiyo vijana wa familia zetu.[emoji116][emoji116]
Nilikuwa naona aibu mno nilipotembelewa na classmates wangu hasa wa kike(nilizidi kumchukia mzee).

Kama walimpenda kwa kuangalia maisha ya familia yako ujue hao si marafiki.
Hata familia za kitajiri zinayo mengi ya kusimulia yenye maumivu.

Bahati nzuri baadhi zimelelewa katika namna ya kuchagua maneno ya kuongea.
Nimeaibika mno na inatosha, nilishindwa hata kulete demy ghetto kwa upuuzo huu huu, mazingira mabovu yapo hovyo hovyo... Niishie hapa.
Hii nayo kali asee.

Labda siyo biological father , naona tofauti ya akili ni kubwa sana.
 
Wewe ni kenge hakuna tofauti. Huoni tu members karibu wote walivyokuona wewe ni zuzu? Ulitaka baba yako afanye nini zaidi? Kuna zawadi nzuri kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto kuliko elimu? Kama ni nyumba kwanini usikaze misuli ujenge wewe?
Na aelewe kwamba kumiliki nyumba si sawa na kumiliki makalio kwamba kila mtu anayo.Baba mwenye nyumba oyeeee!😂😂😂😂
 
Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na HERI duniani. Kwa chuki hii uliyonayo juu ya mzee wako ambaye ametimiza majukumu yote kama Baba naona wewe bado akili yako ni changa sana.

Majukumu yote ya mzee wako kama Baba naona umeyaorodhoresha kwamba aliyatimiza vema bado unampongeza kwa 5%, huu binafsi naona ni uchanga wa fikira na udumavu wa akili.

Suala la kujenga nyumba ndo lisababishe chuki kiasi hiki kwa mzee, napata hisia kama angejenga nyumba nzuri bado ungemlaumu na kumchukia kwa kutonunua GARI.

Mwaka 1988 you’re now 33yrs please try to think and act like a mature folk! Wengine tulivyopata kazi jukumu la kwanza lilikuwa kuwajengea nyumba wazee wetu kwani tulijua vema kama wasingetumia rasilimali zao kutusomesha pengine wangeishi maisha ya kifahari.

Kumtuhumu mzee wako kwamba pengine alichepuka na mwanafunzi ni ushahidi tosha kwamba akili yako ni duni kwani hata kwa usilolijua you only think negative

Mwisho, nachokiona baada ya kusoma btn the line, mzee wako angeweza kukwambia sababu ya yeye kuacha kazi ila tatizo anaona akili yako bado ni ndogo kwani kama ulivyosema akianza tu kuzungumzia suala hili kwa chuki zako za kijinga unaondoka.

Muombe msamaha mzee wako, tubu dhambi na omba shetani huyo unayembeba moyoni mwako kwa miaka mingi akuache. Mungu ni mwema atakusamehe uovu huo ataondoa moyo wako wa jiwe na atakupatia moyo wa nyama.

“La Aquila Non Capit Muscas”
Umri wote huo anamlaumu mzee wakati yeye anatakiwa ajenge kwake kabisa
 
Hata kama bado namchukia tu! Nyumba mbovu halafu ... Sitaki niendelee, nisije tukana.
Wewe nipopoma yan mzee akusomeshe halafu akujengee nanyumba nzuri ili ulete mademu unazan huyo babako hana ambition zake binafsi au unazan kila mtu ndoto yake nyumba. Wewe sema tu unasubiri mzee afe ulithi
 
Wewe ni kenge hakuna tofauti. Huoni tu members karibu wote walivyokuona wewe ni zuzu? Ulitaka baba yako afanye nini zaidi? Kuna zawadi nzuri kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto kuliko elimu? Kama ni nyumba kwanini usikaze misuli ujenge wewe?
Hili toto jinga Sana lishukuru hata Hio nyumba ya nyasi na vumbi sie wengine tumekulia porini na tunadunda tu na hua tunajivunia home sweet home
Mtoa mada Jenga kwako Ndio usakafie na sementi Acha kumpangia babaako Ako Kwa nyumba ya vumbi la Kongo!
Shwain!
 
Hili toto jinga Sana lishukuru hata Hio nyumba ya nyasi na vumbi sie wengine tumekulia porini na tunadunda tu na hua tunajivunia home sweet home
Mtoa mada Jenga kwako Ndio usakafie na sementi Acha kumpangia babaako Ako Kwa nyumba ya vumbi la Kongo!
Shwain!
Ni kweli kabisa. Baba yake kamfanyia vingi eti yeye anaona haya mademu wake wakija kwao nyumba siyo nzuri. Hili ni toto hasara.
 
Pumbavu kabisa...nimepoteza ATP zangu kusoma utopolo
 
Back
Top Bottom