Namba za vitambulisho vya kupigia kura zinatafutwa sana

Siku moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukamilisha zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwa mfumo wa BVR, imesema mtu yeyote haruhusiwi kutoa kadi yake ya wapigakura au taarifa za kadi hiyo kwa ndugu,jamaa au mwajiri wake.

Mkurugenzi wa NEC, Kailima Kombwey alisema jana kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, hairuhswi na haitakiwi kwa mtu yeyote asiyehusika na kadiya mpigakura kuimiliki kadi hiyo.

Chanzo: Mwananchi ukurasa wa 6
Tanzania bwana!kwani kuna watu wasiojua kuwa kadi ya mpiga kura ni mali ya mpiga kura na kazi yake ni kupiga kura tu.
 
Naanza kupata mashaka na TUME kwa mara nyingine tena! Kwanini taarifa hii wasingeitoa mapema wakati wa kuanza zoezi?

Wamesubiri hadi watu wamedanganywa na kutoa taarifa za kadi zao kwa kutokujua athari zake, leo hii ndio wanatoa taarifa!

Anyway, see October!
 
Siku moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukamilisha zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwa mfumo wa BVR, imesema mtu yeyote haruhusiwi kutoa kadi yake ya wapigakura au taarifa za kadi hiyo kwa ndugu,jamaa au mwajiri wake.

Mkurugenzi wa NEC, Kailima Kombwey alisema jana kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, hairuhswi na haitakiwi kwa mtu yeyote asiyehusika na kadiya mpigakura kuimiliki kadi hiyo.

Chanzo: Mwananchi ukurasa wa 6

Mbona nasikia wale wanaohita jimkopo benk wanambiwa waende na hivyo vitambulisho hasa wale waliojiunga na vikoba au ndio goli lenyewe la mkono na kuna huu mfuko wa kuwekeza sijui unaitwa nini hununui hisa bila kupeleka kitambulisho chako cha kupigia kura.
 
Tanzania bwana!kwani kuna watu wasiojua kuwa kadi ya mpiga kura ni mali ya mpiga kura na kazi yake ni kupiga kura tu.

Mimi naona wameandika ati ni mali ya Tume ya Taifa ya uchaguzi na sio zetu teh. Wehu kweli hawa.
 
Daah ccm washaanza njama zao za hila mchana kweupe pee.

kuna kauli moja ilitolewa na kiongozi mmoja wa CCM majuzi hapa akiiomba tume ya uchaguzi kuongeza siku za kujiandikisha katika jiji la Dar ili wajiandikishe wakazi wengi,kwa kuwa CCM inalitegemea sana jiji hili kupata ushindi.Ni jambo jema,ni haki ya watu kujiandikisha,lakini pia sometimes ukitaka kufanya ubaya kwa siri,unatumia njia zile zile za haki kwa nje halafu ndani yake kuna njama.Kwa jinsi nilivyofuatilia ujanja mwingi uliotumika kupata ushindi ndani ya kura za maoni za CCM,na kwa kuzingatia hali ya kisiasa jijini Dar ilivyo ngumu kwa CCM hivi sasa,najiuliza sana wanatoa wapi confidence ya kusema jiji hili litawapa ushindi na kutaka watu wengi kujiandikisha?Sasa kuna jambo moja hapa kuhusu Dar,watu wake wengi wana tabia ya kuhitaji vitambulisho hivi kwa sababu ya matumizi mengine zaidi ya kupigia kura.Na wakati wa uchaguzi wengi hawajitokezi kupiga kura.Je,idadi hii ya waliojiandikisha halafu wasipige kura haiwezi kutumika details zao kufanya udanganyifu kuwa wamepiga kura na kura zao kuangukia chama fulani?hakuna ujanja unaoweza kufanikisha hili haswa ndani ya tume ya uchaguzi?Mioyoni mwao CCM walitaka watu wajiandikishe tu,au wajiandikishe na kupiga kura?kilichojiri kwenye kura za maoni CCM kimenitisha mno.Sikujua CCM imefikia huku.Ndio maana nawalenga wao zaidi hapa na wao ndio wenye influence kubwa ndani ya tume na serikali,na picha yao ya kura za maoni mmeshuhudia ninyi wenyewe ilivyokuwa.I'm just curious... Yericko Nyerere Mag3 BAK Salary Slip mnasemaje kuhusu hili?zingatia Dar imeleta 2.8 mil voters!
 
Last edited by a moderator:
je kuna madhara endapo mtu au taasisi au idara fulan wakiifaham namba yako ya kitambulisho cha kupgia kura?je kama yapo yanatokea vip?na madhara niyepi?
 
Mkuu wa kituo cha polisi Wilayani Mafia ametumia ukuu wake kuwaamuru askari wake wote wakusanye kadi zao za kupigia kura na hatimae kuchukuliwa namba za kila kadi na hatimae wakarudishiwa kadi zao.

Vipi wanajamii hili sio bao la mkono kweli?
 
Miongoni mwa kazi za ajabu ni "police" yaani unapokea amri kutoka juu kisha hutakiwi kuhoji? Hawa maafande wetu ni maboya sana,haya sasa namba zimechukuliwa ili muondolewe kwny daftar la kupigia kura.
 
Sio Mafia tu mkuu,hii ni Tanzania nzima, nashangaa upinzani wamenyamazia upuuzi huu.
 
Kuna chuo kikuu pia wanafunzi wanapeleka kadi zao za kupigia kura kwa Dean of students halafu wanapewa elfu tatu.

Nilijaribu kuulizia Dean anasema anafanya kuwapa motisha hao wanafunzi ili wajiandikishe kwa wingi. Na wanafunzi walivyokuwa mazuzu walikuwa wanaitana na kujazana vituo vya kura na kuchukua kadi na kuziwahisha ofisi ya Dean na kupewa hiyo elfu tatu!
 
Msikilize hapa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema bara, John
Mnyika alipozungumza na wanachama wa Chadema jimbo
la Ubungo
www.facebook.com/story.php?story_fbid=10153498540114339&id=109362579338&_rdr
 
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vikizuka wakwanza kabsa kuulizwa aulizwe jk,jk ameshatamani kwenda mahakama ya The hague
 
Bank ya KCBL Moshi inasema inatoa mikopo (Fedha za NSSF) kwa Vicoba.....na kila mwanakicoba anatakiwa kutuma namba yake ya Mpiga kura kwao....hata mimi nimetuma....kuna mtu anaweza kufuatilia wanazifanyia nini?
watakusaidia kuchinja hali ni mbaya
 
mashine za BVR tu ni penati hiyo tayariii plus kuchukua number penati y pili na zote zimefungwa... ukimalizia na goal la mkono tayari ni tatu bila.... lowasa ni ngumu kuingia magogoni
 
Back
Top Bottom