Namba za vitambulisho vya kupigia kura zinatafutwa sana

kadi ya mpiga kura, ni maalumu kwaajili ya kupigia kura tu.

Je, waajiriwa selikalini walio lazimishwa na waajiri wao wapeleke namba za vitambulisho vyao vya kupigia kura ni kwa maslahi ya nani?

no reseach, no data, no right to speak.
ungefanya research tukajua hizo namba ni za nini.
 
majina mengi ya wapiga kura hayaonekani ktk orodha ya wapiga kura.huu ni mchezo kati ya tume na ccm kufunga bao la mkono
 
Hili ni kweli, juzi Wife alienda kuhakiki kadi yake akakuta jina lake halipo, akaambiwa aende kwa mkurugenzi ili kurekebisha, jana kaenda kwa Mkurugenzi akaambiwa wako kwenye kikao warudi kwenye vituo vyao na kadi zitarekebishiwa huko(HAIJULIKANI NI LINI ZITAREKEBISHWA)!!!

Kwakweli inatia simanzi sana Taifa langu!!!
 
Kwa hali hii bora uchaguzi wa kupiga kura kwa kujipanga nyuma ya mgombea
 
Wataionja chungu ya wananchi endapo watathubutu kufanya hako kamchezo kakutapeli haki yetu ya msingi.Wasidhani hii ni nchi yao wao pekee yao na kina tunu...
 
Kuweni Makini.
Jana Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa
mlongo aliitisha kikao na waendesha boda boda
wa MWANZA hotel ya GOLD CREST, Boda boda
hawakujua lengo la kikao hicho ingawa baadhi ni
dhahiri walijua, kikao kilifunguliwa na mkuu wa
wilaya nyamagana na mazungumzo yalianza...
Boda boda waliahidiwa kupewa BIMA ya AFYA,
Na kusaidiwa kujiunga na mifuko ya jamii, pia
walipewa elfu 5000 kwa kila boda boda na ahadi
ya chakula kwa siku hiyo ilitolewa, jumla ya boda
boda waliohudhulia ni zaidi ya 500, Baadae
wakaambiwa wakabidhi vitambulisho vyao vya
kupigia kura, hapo ndipo mzozo ulipoanza, boda
boda baadhi wakahoji nia ya wao kukabidhi
vitambulisho hivyo lkn mkuu wa mkoa akaanza
kuwafokea na kuwatisha ndipo mlango
ulipofungwa, boda boda wakatishia kujisaidia
ndani ya hotel hiyo ndipo mlango ulipofunguliwa
na wengine wakatoka bila kukabidhi vitambulisho
vyao lakini wengine walikabidhi kwa ahadi kuwa
ijumaa hii wataenda kukabidhiwa BIMA ZA AFYA
nk.
Mpango huu ni wa Nchi nzima na ni maagizo kwa
WAKUU WOTE WA MIKOA Na WILAYA na
watendaji wa chini yao.
share ujumbe huu kwa haraka na kwa watu mbali
mbali na mpigie simu mwendesha boda boda
yyte unayemfahamu kumtahadhalisha juu ya
mpango huu haramu wa CCM na serikali yake.
 
Hizi ni dalili za Handball!

Bodaboda wa Mwanza tunaomba taarifa ya kina kuhusu tukio hili. Kama ni kweli, huu sasa ni ukiukwaji wa haki za raia. Bima ya afya inahusiana vipi na kitambulisho cha mpiga kura? kama ni utambulisho kwa nini basi wasiwaombe leseni za udereva (maana natumaini wengi kama si wote walikuwa nazo). Hao waliotishia kumwaga uharo hotelini ili kujiokoa kifungoni nawapa big-up sana!
 
Bodaboda ni mtaji wa wanasiasa mfilisi.!

Nimeongea na mtu wa Mwanza jambo hili ni kweli na aibu kubwa! Wenje alifanyie kazi hili jambo maana jamaa kaniambia eti wanapokuja kurudishiwa vitambulisho wanapewa feki! Wavichunguze hivyo vitambulisho kama ni genuine! wawafundishe kuwa wakiombwa kukusanya vitambulisho wanakili namba za vitambulisho vyao na vikirudishwa walinganishe kama namba ziko sawa!
 
ni kweli hicho kitu kipo na kuna makada uchwala wanafanya hiyo kazi! natafute mtego wa huyo MTU akiingia anga zangu ntapga balaa! hakuna goli LA Mkono hapa tukutane kwenye sanduku LA kura
 
Jamani usitishwe na wao kuchukua namba, labda kama wanenda kukufuta kwenye database ya tume
 
Kuna watu wanazunguka mitaani kuomba kurekodi taarifa za kitambulisho chako, usiwape.

Imetokea hapa Mwanza balozi wetu kaja nyumbani kuomba kurekodi taarifa za kitambulisho changu, nimemkatalia kaondoka, watu tuwe makini na watu hawa, yawezekana ndo maandalizi ya goli la mkono.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom