Namba za vitambulisho vya kupigia kura zinatafutwa sana

Source????

Mkuu, afande mentor source ukimpata?. Askari ni miongoni mwa makundi yaliyo vulnerable, kazi zao haziwapi uhuru kamili wa kujiamulia. Wao hutii amri tu, tatizo linaanzia pale wakubwa wao wanapo fuja mamlaka juu yao.
 
Mkuu wa kituo cha polisi Wilayani Mafia ametumia ukuu wake kuwaamuru askari wake wote wakusanye kadi zao za kupigia kura na hatimae kuchukuliwa namba za kila kadi na hatimae wakarudishiwa kadi zao.

Vipi wanajamii hili sio bao la mkono kweli?

Sio mafia tu hapa pwani mkuu.
 
Nadhani na wao wanaangalia watu wa kuwaambia huo upuuzi, Kwa wengine huku hatujakutana nao japo nasikia huu mchezo upo.
 
Hivi ninyi mnalichukuliaje hili swala la kwamba kuna namba ya simu inaomba namba ya kitambulisho. Then watu wanajipiga picha wanasambaza kwenye maTV na social network. Sasa kama serikali ya ccm inataka namba hizo unadhani mpaka sasa wamefanya pata ngapi kwa kuchukua hizo namba kupitia mitandao watu wanayotumia kuweka picha zao.
Au hilo ndio goli la mkono?? Nimeona Eatv watu wanajipiga na kutuma picha kamili ya kitambulisho,mawazo yangu tu jamani nimeamua kushare hapa baada kutafakari sana hilo goli la mkono isiwe ndio tunafunga wenyewe kwa vipicha na selfie zetu.
 
Wakuu leo nikiwa arusha maeneo ya shivers hapa nimeshangaa sana kuona chanel five wanarusha tangazo la kuwataka watanzania wapige picha vitambulisho vyao vya BVR kisha wapost katika group la wasap na kwenye tv yao,hatutaki mnakili namba za vitambulisho vya watu
 
atakae kuja kwangu.lazima nimle 0713. tumewachoka hii mijitu isio na huruma na watu.sasa kama kweli hawa wanaitwa balozi mjumbe sijui.mbona wanakua hawana maarifa maana wanaishi maisha magumu.bora ata me maana wanawanufasha wenzao wanajisahau.
 
jamani hili suala la kukusanya vitambulisho huku mtaani ni hatari sana na huu mwaka tukae vizuri maana tunaweza ingia matatizoni
 
Haina haja ya wananchi kupiga kura kama kuna watu wanawapigia kwa niaba yao. Waseme wazi ili tuwapatie vitambulisho wakatupigie wote ili wengine tuendelee na majukumu mingine ya ujenzi wa taifa
 
Sijajua kuwa wananakili namba za vitambulisho kwa sababu gani!!! Ni vema hili likachunguzwa!
 
jamani hili suala la kukusanya vitambulisho huku mtaani ni hatari sana na huu mwaka tukae vizuri maana tunaweza ingia matatizoni
hivi unatishwaje na wajumbe wa nyumba 10 ambao 90% hawajui kusoma na kuandika ?
 
Kadi ya mpiga kura, ni maalumu kwaajili ya kupigia kura tu.

Je, waajiriwa selikalini walio lazimishwa na waajiri wao wapeleke namba za vitambulisho vyao vya kupigia kura ni kwa maslahi ya nani?

No reseach, no data, no right to speak.
 
kadi ya mpiga kura,ni maalumu kwaajili ya kupigia kura tu. Je,waajiriwa selikalini walio lazimishwa na waajiri wao wapeleke namba za vitambulisho vyao vya kupigia kura ni kwa maslahi ya nani? No reseach,no data,no right to speak.

mkuu lisikutishe hilo wapiga kura wapo zaidi ya milioni 20, na wafanyakazi wa serikali hawafiki milioni 1. Na walioambiwa wapeleke namba zao za kura hawafiki elfu 10. Yaani sio wafanyakazi wote walioambiwa wapeleke namba zao za kadi ya kupiga kura.
 
Kadi ya mpiga kura,ni maalumu kwaajili ya kupigia kura tu. Je,waajiriwa selikalini walio lazimishwa na waajiri wao wapeleke namba za vitambulisho vyao vya kupigia kura ni kwa maslahi ya nani? No reseach,no data,no right to speak.
Mkuu hiyo ni moja ya dalili Kwamba ccm inapelekea Kuwa chama upinzani .kulazimisha watumishi wa umma,watuwasiotakiwa kufungamana na chama chochote katika utendaji wao wa kila siku,ni dalili Kuwa mgonjwa ana kata roho.take my word
 
Back
Top Bottom