Namba za matapeli hizi hapa

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Wamezuka watu wanapiga simu na kusumbua kwamba wanauza kemikali mbalimbali za kusafishia maji. Kuweni macho nao. Naamini namba za mawasiliano wanazipata sana katika stationery ambako watu mbalimbali wanakwenda kuchapisha kadi za harusi au za mialiko mbalimbali.

Hivyo ndugu zangu kaa nao mbali watu hawa.
 
halafu wakishakupigia inakuwaje!au wanakuambia nini!!

mmojawapo anakupigia anajifanya kukufahamu pia anaweza kuwa ashakufatilia,anakupa deal kuwa kuna mzungu anatafuta kemikali fulani na deal la million 11-15 au zaidi.mara anakata simu ghafla.

harafu unapigiwa simu na nigga mmoja anajifanya mzungu pia anaongea kingereza anakwambia kwamba amepewa namba yako na jamaa wa kwanza aliokupigia simu pia anakwambia yuko njiani anakuja mkoa uliopo pia anakwambia yuko na cash million 11-15 au zaidi na anajifanya ata kukuuliza hotel gani nzuri karibu na ulipo ( wakat mwingine akuulizi hotel gani)harafu simu inakatika.

baada ya hapo unapigiwa simu na jamaa wa kwanza anakwambia ashapata mtu ambaye anauza hiyo kemikali ila anahiuza laki 3 na anakwambia anakupa namba yake ili umtumie pesa kwa mpesa na ata unaweza ukaongea naye anakwambia yuko mbali kidogo ila utume pesa wakuletee mzigo wakat mwingine anakuruhusu utume ata nusu kwanza yani 150,000 ili hakifika na kukupa mzigo ummalizie,

pia yule mzungu anakupigia tena simu kukuuliza mzigo ushapata maana yuko na cash taslimu million 11 au 15 ata zaidi.

ukituma pesa tu wote hawapatikani simu zao,unakuwa umeliwa,watu wengi wapenda utajiri wa fasta wamelizwa .

mkumbuke kwamba yule jamaa wa kwanza kupiga anakuwa na maneno matamu kwamba yeye amekuona wewe ndio mtu muaminifu na anakupa deal ilo la pesa ndefu sababu anakuamini sana,yani anaongea maneno matamu.

kuweni makini wana JF
 
Hiyo ni staili ya zamani sana ya utapeli,hivi kumbe bado wanapata watu hawa jamaa....
 
Umeweka bandiko mwaga na details zao zote watu waelewe ili unapopaacha na sisi tujazie jazie sasa wewe unakatiza fasta tu ka flash ndo nini?
 
Jamaa wanabadilika kutokana na eneo husika/mkoa husika...wakati mwingine wanasema kuna deal ya vinyago, juzi katapeliwa mtu wangu wa karibu sanaa....
 
Mmoja wao anajiita Victor. Namba yake 0686 inaishia 979. Pia jihadharini na kuacha hovyo orodha za wanakamati wa shughuli za harusi, maana mle mnaandika majina, namba za simu na ahadi zenu. Wale wenye kuahidi ahadi nzito nzito ndo wanafuatiliwa sana! Imeshanitokea, nilipochimba mkwara jamaa akaingia mitini!
 
Engine wanatumia namba hizi 0689814064 ,0757688383 walijaribu kwangu nikawashitukia

mkuu hao wanasajili line ata zaidi ya 500.yani awa watu utapeli ndio kazi yao na wanaaga kwao wanaenda kazin kama kawaida pia muda mwingi wanashinda bar wanakunywa ata asubuh au mchana,yani hawana uchungu wa pesa kabisa,na wananunua adi magari kwa huu uwizi wao
 
Back
Top Bottom