Namba za Magari TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namba za Magari TZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaniki1974, Sep 3, 2009.

 1. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanamkeka,

  Huu mfumo wa kusajiri namba za magari Tanzania wa sasa una maantiki kweli? Una ubora na manufaa zaidi ya ule wa awali uliokuwa unatambulisha magari kwa maeneo yatokako kama ARS, SHY, MBY, MZA, UF n.k? Mbona ktk nchi zilizoendelea namba zao zipo ktk huo mfumo tuliouacha?

  Siku hizi naona kuna namba eti BAD!? n.k Hebu tujadili labda tutasaidia kwa mawazo kwa hao waamua mambo wetu TZ. Kuna gari nimekataa kununua lina namba ya ajabu.....
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kaka mfumo unamaana kubwa sana!!!
  • Centralization
  • Consolidation
  • One registry.
  • One database.
  • Improved effieciency
  • easy Curb taxi defaulters
  • eliminate unnecessary resource redundancy
  Siku njema.
   
 3. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa,

  Centralisation ilhali move ya nchi kwa sasa ni decentralisation? Angalia Local govt reform/decentralisation programme kwa mfano n.k

  Hayo mengine uliyoorodhesha mkuu yatarahisisha mambo pale watu wote wa TZ watakapomiliki magari? Think of 80m car owners for example? I can't understand....

  Thanks, anyway.
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Aliyebuni hizo numba hakuona mbali au hakujali herufi kama T 666 UKE
  na nyingine za aina hiyo.
   
 5. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi kwiiiiiiiii.....
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  T 666 BOO
  T 666 BUM
  T 666 ASS...etc!
   
 7. S

  ShockStopper Senior Member

  #7
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Poleni sana mtazoea tu, tatizo lililopo hapa ni mfumo mawazo, mindset. Msipende kukaa bongo tu, jaribu kutembea tembea mfike mpaka Japan mtakutana na watu wanaitwa Takauchi, mji unaitwa Kumamoto n.k. Lakini zaidi ni unafiki tu kwa sababu huko Uchaggani majina ya aina hii yapo na wapi kule Morogoro yanakotoka matunda mengi, tajeni wenyewe panaitwaje, mbona hampati kigugumizi kutamka, lo, acheni mfumo ufanye kazi!
   
 8. M

  Makanyagio Senior Member

  #8
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Mkuu umeuwa. Teh Teh Teh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kila chenye uzuri basi na ubaya upo. Mimi naona mfumo huu wa namba una manufaa zaidi kwa nchi kuliko hasara
   
 10. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #10
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  badilini fikra tu,haya mambo ya mat...si katika hizo plate number si kitu muhimu mfumo unaeleweka.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,258
  Likes Received: 21,969
  Trophy Points: 280
  Matombo morogoro na hombolo dododma
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama muungano wa herufi una matatizo labda wakati wa kutamka. Hata hivyo hakuna anayetegemewa kutamka namba za gari kama neno bali herufi moja moja. Kwa hilo sioni tatizo. Ningepata taabu kama huo mfumo hauwezi ki-mahesabu (combination and permunations - kwa wale waliotia mguu ndani ya BAM) hauwezi kukabiliana na idadi kubwa ya magari. Ila kwa kuwa tuna herufi 26 na namba 10 wataalamu wanaweza kutueleza idadi ya magari tunayoweza kusajili kwa kutumia namba tatu na herufi tatu kwa wakati mmoja. Vinginevyo hata tukibadili huu utaratibu tutakumbana na tatizo jingine!
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...mmmm, nahisi kama umedandia Treni kwa mbele, Mkuu! Ni bahati tu kuwa treni lenyewe ni TRL halina saa maalumu ya kuondoka na hivyo umeweza kusalimika bila kukanyagwa! :D

  Nia yangu ya kuorodhesha hizo namba ilikuwa ni kumuuliza tu mdau aliyeshangaa namba ya UKE atafanya nini akiona kama hizo nilizoorodhesha!


  labda tu nikupe kidogo mwanga kuwa unapotoa mfano kuwa Japani kuna watu wanaitwa Takauchi na Kumamoto mfano wako unakosa hoja kwa mantiki kwamba huko Japani majina hayo yanaweza kuwa na maana ya 'Mwenye Bahati' ama 'Aliyezaliwa Jioni' lakini mtu huyo huyo akija nchini na kujitambulisha hivyo hakuna atakayecheka lakini ukweli ni kwamba baadae watu wanaweza kulidiscuss lightly kama vile vile ambavyo watafanya Mtanzania mwenzao akijiintroduce kuwa anaitwa Mr Kumamoto! :D


  Na kuyajua haya si lazima 'kutembea tembea hadi Japan'. Kuhudhuria tu shule ya msingi hapa hapa nyumbani bila kuogopa umande inatosha, Mkuu! :mad:
  Kujua wa-Mongolia wanavyoishi si lazima ukakae kwenye milima yao, ama?
   
 14. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,846
  Likes Received: 23,460
  Trophy Points: 280
  t666 tia
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hii habari nzima ilishawahi kujadiliwa hapa kwa mapana na marefu angalia hapa na ikaendelea kupewa uzito katika bandiko hili.

  Zaidi bandiko hili litaishia kule kwenye jokes-udaku na gossips!
   
 16. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,372
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mh ikitokea nyumba moja ina magari mawili na jingine likiwa:

  T298 KEI
   
 17. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  It's unfortunate majadiliano yanaelekea zaidi kwenye ze usweet type. Muhimu ni kujua kama mfumo huu wa sasa unarahisisha ku trace magari na kuyatambua kwa urahisi zaidi ya mfumo wa majimbo unaotumika zaidi duniani.... nadhani...

  Hiyo avatar kwi kwi kwiiii......
   
 18. GP

  GP JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  uko sawa kabisa mkuu, kula tano!
  tatizo ni kwamba jamaa wa serikalini sijui wanakurupuka??
  wanashindwa kuelewa kila kukicha magari yanaongezeka, ilitakiwa waelewe kwamba wanahitaji kuweka system ambayo namba zitakaa kwa muda mrefu zaidi bila kubadili system.
  sasa twende kimahesabu hapa chini:
  herufi A-Z ziko 26
  namba wanasajili kuanzia 101-999=(999-100)=898

  kwahiyo kwenye herufi 3, yaani T 666 UKE kutakua na
  26*26*26*898= 15,783,248

  sijajua takwimu za magari tuliyonayo kwa sasa, lakini dalili zinaonyesha hii system haitafikisha miaka 10 tangu sasa kua full.
  hali itakua mbaya kwa Zanziberi wao ndo wamepunguza
  Z 666 UK!!

  ila kwenye hizi herufi zile zote zinazofanana na namba hazihusishwi, mfano I, O
  sipati picha gari liwe na namba hii T 666 CCM ligongane uso kwa uso na lingine lenye namba T 999 CUF, duh itakua balaa. (joke)
  [​IMG] [​IMG]
   
  Last edited: Sep 4, 2009
 19. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nasikia pia mchoraji wa hizo namba na mmoja- masasi signs- sijui anapatikana kila mwaka kwa kufuata sheria ya Manunuzi ya umma, au kifisadifisadi?...sina hakika. Mwenye data pse....
   
 20. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha namba ya kwentu DO it was very good numbers jamani esp zile za ZNZ zanzibar nzuri zamani lol....hey hata zile za zamani zingeweza kuwekwa kwenye data base na zilikuwa na maana zaidi

  Point ni kuwa:

  Namba mpya ni mradi wa wakubwa hivi nani anaruhusu kugusa mradi wa munene.....atapingwa mutu humu...heheh ipo siku tutaambiwa tunatakiwa tubasilishe majina yetu tutumie mapya yatakayowekwa kwenye data base pale rita it doesnt make sense hata za zamani zingeingia kwenye data base muwe mnafikiria out of the box nimeimiss sana JF I think baada ya kuwa naangalia tu nitaanza kuchangia...
   
Loading...