Naliona anguko la Kibanda



Ndugu yangu Halisi moto ni upi na petroli ni ipi? Hivi Nimesoma sana na kukaa kimya muda mrefu wakati watu wakiweka thread zenye majina yetu. Kimsingi nimesikia ushauri wako ulionipa kwa maandishi na kwa mdomo. Kila ninapoamua kuchangia nafanya hivyo nikitumia maneno laini. Hata hivyo upo wakati wa jiwe kuitwa jiwe badala ya kumung'unya maneno.

Niko tayari kupokea tuhuma za kweli na kimsingi niko tayari kuomba radhi hata katika mambo yangu ambayo pengine yanawakera Watanzania wenzangu wanaoipenda nchi yao kwa dhati.

Tuache wenye hoja za kweli wazitoe hata kama kwa kufanya hivyo tutaumizwa. Siwezi nikawa mtu wa kufanya uchambuzi katika gazeti halafu nikawa mwoga wa bakora. Maji nimeyavulia nguo sina budi kuyaoga.

Hata hivyo siko tayari kuona watu wanajaribu kuosha wenzao kwa maji taka halafu Halisi ukategemea mimi nikae kimya kwani hata Mzee Sitta ambaye aliwaasa wanasiasa kuwa na ngozi ngumu, yalipomfika yeye mwenyewe aliweka kando kijikanuni chake hicho na kuamua kupambana. Huo ndiyo ukweli. Nimeshindwa kuisoma private msg yako kwangu. Haikufunguka.
 

Ndugu Kibanda, msalimie rafiki yangu Lwitiko.
 
masatu,
i hope taswira ya hilo ''ANGUKO'' imepotea kabisa kwa sasa.
karibu kesho kwenye maandamano ya amani yenye dhima ya ''mshikamanol ndani ya chama''
ubarikiwe sana mkuu
 

Kama hoja za kweli alivyozitelemsha Zitto na jiwe kuliita jiwe yani UMANGIMEZA.

safi sana.
 
hAKUNA ALIYESEMA KUWA RAILA ANAFANYA BIASHARA NA ROSTAM AZIZ. Tulizungumzia fedha zilizopelekwa kusaidia kampeni za ODM kwenye uchaguzi wa kenya kutoka kwa Rostam Aziz. Tunajua Rostam hana fedha nyingi hivyo lakini zile alizokwapua kwenye EPA alizitumia kufadhili chaguzi mbalimbali ukiwemo uchaguzi wa Kenya. Watu wengi wangetaka kujua habari hizi za Rostam na kupenyeza fedha kwenye chaguzi akijipendekeza kwa kivuli cha kusaidia viongozi wenye muelekeo wa kimaendeleo. Viongozi aliowasaidia kwa namna hiyo hawawezi kukana huu ukweli. Ni christopher Mtikila pekee aliyejaribu kumkana Rostam akaumbuliwa kwa kuchapishwa hata risiti aliyopokelea fedha hizo.
mimi naliona zaidi anguko la Tanzania kuliko la Kibanda na Zitto kama hatutabadilika.
 
Mbona inasemekana kwenye hilo gari moja kuna mkono wa RA hata mkanunuliwa magari ya kufanana na Muhingo?


Mbona inasemekana kwenye hilo gari moja kuna mkono wa RA hata mkanunuliwa magari ya kufanana na Muhingo, na namba zinafuatana?

Mi nimesikia tu naomba jibu
 
masatu,
i hope taswira ya hilo ''ANGUKO'' imepotea kabisa kwa sasa.
karibu kesho kwenye maandamano ya amani yenye dhima ya ''mshikamanol ndani ya chama''
ubarikiwe sana mkuu

Baba mkwe karidhia maandamano?
 
Mbona inasemekana kwenye hilo gari moja kuna mkono wa RA hata mkanunuliwa magari ya kufanana na Muhingo, na namba zinafuatana?

Mi nimesikia tu naomba jibu

Uwiiiiiiiiiiiii.... Bongo ni zaidi ya uijuavyo!!!, au jungu tu hili???
 
Duh, sasa ikiwa wewe ni mwandishi na umefanya mazungumzo na huyo Mnyika na Mrema, kwa nini usinukuu (quote) maelezo yao wao badala yake wewe ndiye msemaji mkuu....
Uandishi gani huu tena mkuu wangu yaani wewe unashika nafasi tatu za watu kwa wakati mmoja!...
 
 
Mbona inasemekana kwenye hilo gari moja kuna mkono wa RA hata mkanunuliwa magari ya kufanana na Muhingo, na namba zinafuatana?

Mi nimesikia tu naomba jibu


Swali hili lilikuja katika thread ya 'Naliona Anguko la Zitto Kabwe' na nikalijibu tena. Soma. Huu ni uzushi mtupu. Tumefikia hatua ya kumfanya RA kuwa ni Mungu Mtu ambaye kila kitu yuko nyuma yake. Ninalifahamu gari la kaka yangu na rafiki yangu Muhingo na namba hazifuatani. Uongo 100%. Si utafutwe uongo mwingine ninyi vijana wa CCM?
 
Mimi naona anguko la Tanzania kwa jinsi njaa zetu zinavyotawala misimamo yetu kuliko anguko la Kibanda na Zitto Kabwe. Wewe Fikiria, kama Fisadi mmoja anweza akanunua viongozi wetu kwenye vyama vya siasa kwa kuwasaidia kwenye chaguzi zao, unategemea nini???? Tena huyu bwana anajua anachofanya maana anaamini katika kumwagilia miche yote kwani hajui mche utakao chipua!!
 
 
Kibanda,
Kama si wewe uliyeandika makala zile kwa pen name basi uliruhusu gazeti unaloliongoza kumshambulia mtu aliyetoa changamoto za kusaidia nchi yake. Gazeti lako, magazeti ya serikali ya sisiem na magazeti yake RA yalikuwa ndiyo vinara wa kumshambulia RAM. Ni lazima ujisafishe, vinginevyo umma unajua kuwa wewe uko kwenye payroll ya Fisadi yule. Na rangi yako halisi itaonekana hivi karibuni.
 

He is not genuine...na wala hana nia njema ya kuisaidia Chadema.......alichokifanya anakijua na njaa yake imemponza, ni msaliti. Na nilishawahi kuandika ...Chadema wako makini wanajua wanachokifanya, wamemtoa kidiplomasia na ikibidi asipewe uongozi.
 
 
..Wazee wa Chadema watafute mbinu ya kuwaondoa hawa vijana wao taratibu.

..binafsi nadhani Zitto, Mbowe, na makundi yao hawafai kuongoza Chama wala nchi.

..Chacha Wangwe niliona ana matatizo, lakini kwamba walikuwa wanatumia njia chafu kupambana naye inaonyesha kwamba wao wana matatizo zaidi.

..nachukia sana watu wanaoshiriki kwenye siasa chafu-chafu za majungu-majungu.
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…