Nalililia kaburi la Kiyeyeu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nalililia kaburi la Kiyeyeu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gama, Feb 5, 2012.

 1. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikisoma taarifa mbalimbali juu ya maajabu yanayoonekana kwenye kaburi la Chifu Kiyeyeu pale Iringa. Nimepokea kwa masikitiko habari za kuwa kaburi hilo limehamishwa ili kupisha upanuzi wa barabara na kupitisha waya wa umeme. Nimesikitishwa kuona kiuwa nchi hii ina taasis nyingi zinazojihusisha na mambo ya kale lakini hakuna taasis hata moja iliyokemea kitendo cha kulihamisha kaburi hili. Binafsu kama mwana historia nilidhani taasis mbalio mbali kama makumbusho ya taifa, wizara ya utamaduni, ofisi ya utamaduni ya wilaya, ofisi ya mkuu wa mkoa na NGOs wangetia juhudi kuona kuwa kaburi hili linaorodheshwa katika moja ya maaajabu ya dunia na hata kuwa kivutio cha utalii. Kukubali kuliondoa kaburi hili kwa ajili ya mambo yaliyokuwa na mbadala ni ukosefu wa hekina na busara na kutokuwajibika kwa taasisi zetu ambazo kutwa kucha zinaogelea katika kodi za wananchi. Natoa wito kwa serikali kuacha vitendo vya uharibifu wa mambo muhimu yanapaswa kuwepo ili hata vizazi vijavyo viweze kuona.
   
 2. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Uchawi kivutio cha watalii?
  Wenzetu wanasumbua vichwa kugundua vitu vinavyo tusaidia na kurahisisha maisha,
  Si tunabaki kuabudu uchawi unao rudisha maendeleo.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi barabara ikipita juu ya ilipokua kaburi la kiyeuyeu ajali nyingi zitakua zinatokea
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ndio nani huyoo? na anamaajabu gani maiti?
   
 5. m

  mareche JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kama unataka kuangalia mmbo ya kale nenda olduvai achana na uchawi
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kwanza wangefukua mifupa wakaiweka museum!
  Aisee ww jamaa umenikumbusha kazi moja niliifanya rufiji ya feasibility ya investment flani. Yaani tunawauliza wananchi mnataka mwekezaji awanufaishe vipi, ati asiguse makaburi ya wazee wetu kule porini! Yaani nilitamani kuwalamba vibao, mashati yamechanika, ndevu kama vichaka, afu wasiwasi wao ni barabara isiathiri makaburi! Duh!
   
 7. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Ww una akili sana.Miafrika tunacho jua ni kujivunia uchawi.
   
 8. Hagga

  Hagga Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi na watu wake waliofilisika kimawazo hutegemea zaidi miujiza kujiletea maendeleo.Sikuona ajabu watu wengi kumiminikia Loliondo kipindi kile.Sitaki kugusa imani ya mtu, ila hata yaha makanisa yanayo-mea kama uyoga ni dalili ya kutafuta miujiza badala ya kutumia akili na maarifa tuliyopewa na Mungu kujiletea maendeleo.

  Tanzania haitajengwa kwa miujiza wala uchawi wa makaburini.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Yaani afadhali umesema! What to be proud of? Haya mambo yanayotu lostisha? Unajua mpaka leo hii kuna watu wengi wanaotuongoza wasiofuata ushauri wowote wa kitalaamu zaidi ya waganga na hawa walozi?
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Unauhakika gani kuwa kushindwa kupitisha umeme juu ya kaburi la kiyeyeu ni nguvu za uchawi?!, mimi siamini kuwa ni uchawi, nihakikishie kuwa hakuna scientific description- inaonesha wewe na elimu yako yote unafikiria uchawi kwanza!!!!. Kwanini tusingewaita wanasayansi wakatuhakikishia kuwa wamekosa scientifuc description ndiyo tujiridhishe kuwa kaburi hili ama tukio hili halina maana?!. Ndiyo maana waafrika hatusongi mbele kwani kila tukio la ajabu la afrika kwetu ni ushenzi na backwardness. Nasubiri kanisa la kakobe livunjwe ili umeme upite. Mbona ulaya kunavitu visivyo elezeka lakini vimekuwa documented kama vile UFO, maajabu ya namba 13 kwenye mahoteli na majumba makubwa na bermuda triangle?! Sisi kwa nini tunakimbilia kuvunjwa?!
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,098
  Likes Received: 6,562
  Trophy Points: 280
  Mm naungana na wewe. sikupenda walivyofanya. kwani njia kwa kupita ni pale kaburini tu.R.I.P kiyeyeu.
   
 12. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wakati Tanesco wanataka kupitisha waya pale kwenye makaburi,wali waomba ukoo wa wenye makaburi wahamishe.
  Ukoo ukasema utahamisha kwa kiasi kikubwa cha pesa.Tanesco wakaona isiwe tabu waka pindisha waya mchezo ukaisha.
  Sisi na imani zetu tuna danganyana eti uchawi.
  Kwani ufo ni uchawi? Kama kweli ipo ni watu wakutoka sayari nyingine.
  13 kwenye hoteli nayo ni kudanganyana na imani potefu.Kuna watu wana Guest house ina namba 13 na hamna lolote linalo tokea.
  Bemuda ni si uchawi ni hali ya nature pale pana mikondo ya maji yanakutana.
  Tatizo letu mtu akifikiri akakosa jibu anatafuta njia rahisi ya kuto umiza ubongo na kusema nguvu za giza.
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Mkuu, asante kwa kuchangia, but kuna mambo mawili naomba kutofautiana na wewe. Kwanza ni hili la Tanesco kuombwa fedha nyingi kwa fidia au gharama ya kuhamisha kaburi: miradi mikubwa inapofanyika gharama za kuhamisha kaburi ziko kisheria hivyo fidia hufuata sheria hii so sioni sababu ya njia ya umeme kipindishwa ati kwa sababu wenyewe wanataka pesa nyingi. Kuhusu maajabu ya namba 13; ujue kuwa moja ya imani ni kuwa chumba namba 13 hakifai kwa biahsra ama kina ambatana na mikosi na mabalaa mengi kwa hivi hakuna corporate co au person atakaye fanyia shughuli zake ndani ya #13.
   
 14. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  nimewai kufanya kazi na kampuni ya siemens ya german kuweka nguzo za umeme kati ya dar na kidatu kuna maeneo wale wazungu walisimamia mazoezi ya kuchinja kondoo na damu umwagwa kwenye maeneo korofi
   
 15. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Umeniacha feri, maeneo korofi kulikuwa na kaburi la kiyeyeu?!
   
 16. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hapa mkuu kuna mnara ilikua zege alikauki
   
 17. S

  Shada Member

  #17
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kama kaburi hili la Kiyeyeu lingekuwa na jambo muhimu la kistoria,-hata mimi ningependelea libaki, lakini umaarufu wa kaburi hili ni mambo ya ushrikina au kwa lugha nyingine uchawi.-Hapa naoan tutakuwa tunarudi nyuma sana kimawazo na fikira.
  Mimi kaburi ambalo linanisikitsha sana ni kaburi la SHABANI ROBERT,-kwa kweli huyu bwana ilibidi kulienzi kaburi lake kwa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na sasa,-cha kusikitisha sana kaburi hili limepotea,-imebaki alizikwa maaeneo haya hakuna mwenyewe uhakika na sehemu halisia ya kaburi hilo.
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kiyeyeu hajawahi kuwa Chifu...!!! Alikuwa ni mshirikina aliyekubuhu tu...!
   
 19. Frank Sojo

  Frank Sojo JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2015
  Joined: Mar 1, 2013
  Messages: 341
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo maajabu ni uchawi?
   
 20. m

  multmandalin JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2015
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 1,951
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmmhhhhhhhhh!
   
Loading...