Nalia na wanasiasa na watendaji serikalini: Kwa heri Ndugai

Nalia na wanasiasa na watendaji serikalini: Kwa heri Ndugai

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
869
Reaction score
1,282
Kila nikiangalia ni kwa kiasi gani hii nchi ikebarikiwa rasilimali ila wananchi wanaishi maisha duni na ya dhiki, moyo unauma.

Ila najua shida zote tunazopitia wananchi ni zakutengenezwa na kikundi cha watu wachache wasiokuwa na huruma hata punje.

Watu hawa WANATUFANYIA ROHO MBAYA UTADHANI DUNIA NI YA KWAO.

1. Wanajichagua kuwa viongozi, wabunge n.k alafu wanatunga sheria za kutukomoa sisi ila wao sheria haziwahusu. Mfano: Mafao ya mifuko ya hifadhi ya Jamii. Mtu wa kawaida mkataba wake ukiisha Itabidi asubiri miezi 24 kupewa michango yake. Ila wao ni kila baada ya miaka mitano wanalamba chao. Mtu wa kawaida akistaafu kuna kikokotoo cha ajabu-ajabu unapigiwa na kupewa hiyo pesa ni mbinde. Ila wao ni haraka sana.
Fao la kustaafu kwa kada zingine ni kufuru. Wao waendelee kula anasa, sisi tule shida.😭😭😭😭

2. Mishahara wanajipakulia minono na marupurupu kibao; ila wengine ni unapakuliwa kwa kijiko. Ni mwendo wa kula usife.

3. Huduma: Mtu wa kawaida unajichanga-changa unalipia kuunganishwa na Huduma ya maji. Cha kushangaza na kusikitisha, kumbe maji yenyewe hakuna. Kila siku magari yanazunguka kusambaza maji. My country!!!!

4. Bima ya afya: Unalipia bima ya afya ya mwaka mzima, ila ukiukwa hata magonjwa ya kawaida sana, wewe ni wakutibiwa na dawa za hali ya chini. Kuna dawa hupewi. Dr. anaishia kukuambia hizi haturuhusiwi kutoa, nenda kanunue.

5. Elimu: Kuna watoto wengi wanaachwa maksudi ile wakifeli mitiani ya darasa la saba, Form 4 na 6. Huku ni kutengeneza umasikini kwa lazima. Mnaonaje ikiwa mtu kagombea ubunge au urais akifeli mara ya kwanza asiruhusiwe kugombea tena? Tutumie akili tunapofanya maamuzi yanayohusu maisha ya watu.
Mitaala yenyewe ya elimu, nayo majanga. Watoto wao wanasoma mitaala ya nje. Sisi wengine tunalazimishwa kubaki daraja la chini. UMASIKINI WA KUTENGENEZWA.

6. Nalia na viongozi: Duniani sisi ni wapitaji; ukilijua hilo utafanya kila uliwezalo kupafanya pawe mahali salama na pazuri kwa binadamu na viumbe wengine kuishi. Usijilimbikizie mali tena kwa kupora rasilimali za watu masikini.
  • Wanalipwa mafao makubwa, lakini bado haziwatoshi wote wanataka wajazane bungeni na nafasi zingine.
  • Wanafanya biashara kubwa, lakini bado haziwatoshi, lazima wawaumize wanyonge.
  • Nafasi za kula kwa Urefu wa Kamba yako, bado hawatosheki.

Umeendoka, unajua mwenyewe uliacha wapi nchi itakayolinda watoto na ndugu zako wengine pamoja na watanzania wote kwa ujumla.
 
Sisi watendaji wa serikali, kwa mfano mimi na walimu wenzangu hapa SM Sabasaba tunahusika vipi na hizo querries ulizozianisha hapo juu ?
 
Sisi watendaji wa serikali, kwa mfano mimi na walimu wenzangu hapa SM Sabasaba tunahusika vipi na hizo querries ulizozianisha hapo juu ?
Wewe wala haupo tunapoongelea watu wa serikalini. Wewe mnyonge mwingine tu.
 
Wewe wala haupo tunapoongelea watu wa serikalini. Wewe mnyonge mwingine tu.
Una maana gani kunitoa katika watendaji wa Serikali wakati kila siku nipo shuleni nafundisha watoto niliokabidhiwa na viongozi wangu kwa niaba ya Daktari Samia ?
 
Back
Top Bottom