VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Nimekatisha safari yangu ya kwenda nyumbani Songea, Ruvuma. Nimegeuzia Masasi, Mtwara. Nimeamua kuingia mstari wa mbele bila kelele kuhakikisha kuwa Mama Samia anaukwaa Uenyekiti wa CCM bila vikwazo vyovyote. Nikiwa Masasi, nilipokea taarifa za kiintelijensia kuwa kuna baadhi ya makada wabobezi na wa kawaida wa CCM wanajipanga wakiwa Dodoma na kwingineko kuhakikisha kuwa Mama anakwama au anayumba.
Kwasasa nakaribia Morogoro Mjini. Nakwenda Dodoma kwa 'kazi maalum' ya kichama. Nakwenda kumsafishia njia Mama Samia ili mwishoni mwa mwezi huu aukwae Uenyekiti wa CCM bila mawaa wala balaa. Mama Samia anaweza. Mama Samia anafaa. Ni msikivu; mwenye huruma na haki. Mama Samia ni mwenye kusikia na kusikilizwa; kutafiti kabla ya kusema na kufikiri bila kuhema. Mama Samia anaipenda demokrasia.
Akiwa Mwenyekiti wa CCM atafungua uwanja wa demokrasia ya vyama ili wanasiasa wa zamani na wa sasa tuingie kucheza bila kuumiza. Wanasiasa tuingie uwanjani kuoneshana ukomavu wa hoja za haja na mbinu katika medali za kisiasa za kisasa. Atafungua mikutano ya hadhara yenye hadhira bila hasira na maandamano ya kutokukubaliana bila hiyana. Mama anaweza kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini.
Kesho asubuhi, naanzia ndani Bungeni kumsikiliza mubashara akilihutubia Bunge na Taifa kwa ujumla. Watanzania wanasubiri maneno yake yatakayofuatiwa na matendo yake. Baada ya hapo, Uenyekiti wa CCM unafuata. Safu mpya itasukwa. Chama kitasonga mbele bila kelele. Mapambano yataendelea.
Wabunge waachwe wademke hadi wachemke!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kuelekea Dodoma)