Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
Dah! Nahisi mpenzi wangu ni wa sample hii, hana uhakika kama anataka kuolewa au la
 
Nkamu; deep down unatamani kufunga ndoa na huyo kaka; kinachokukwamisha ni hiyo fear yako tu. Whatever happened with your ex hubby; bado kinaishi ndani yako na kukusumbua. It is more of a psychological issue: "Fear of failure".

Kinachokuumiza sasa hivi ni hilo wazo kwamba "itakuwaje hii ndoa ikivunjika pia"?. Jaribu kujiuliza je umeshaanguka mara ngapi kwenye maisha yako; lakini ukajaribu kufanya tena hicho kitu kilichokuangusha na eventually ukafanikiwa? Kwa nini uamini tu kuwa utashindwa badala ya kuamini kwamba this time ndoa yako itadumu? Unapopata nafasi ya kufanya kitu fulani na ukashindwa kuifanyia kazi; je hutokuja kujilaumu kesho? Can you afford to lose that guy? Can you bear the cost of not giving it a try?

Nina rafiki zangu wawili ambao walipitia divorce na wote wana ndoa tena sasa hivi. Kwa nikichokiona tu wakikipitia; aisee divorce ain't a joke; haijalishi wewe ndiyo umetaka divorce au umepewa. It takes a toll on a person. But I'm glad waliweza kukubaliana na kila kilichotokea na wakasonga mbele.

*Ulijifunza nini kwenye ndoa yako ya kwanza. (Maybe we should never ignore the red flags). Usiangalie tu mumeo alikosea wapi; angalia na wewe ni wapi ulipokosea then parekebishe. Kuna watu unakuta kila siku anaumizwa tu; lakini ukija kuangalia shida kubwa zaidi ipo kwenye choices zake. Ni lazima ujue exactly ni nini unakitaka.

*Kubali kwamba kilichotokea kimeshatokea. Jipe nafasi ya kupenda na kupendwa tena kwa uhuru. Chochote kitakachokuja kutokea kwenye ndoa yako ya pili; accept it wholeheartedly.

*Usiignore any red flag ambayo unaona kabisa huku mbeleni utakuja kuwa-cost. Second divorce itakuumiza na kukugharimu pakubwa

*Usiingie kwenye ndoa na Ile dhana kwamba "you want to prove people wrong; so no matter what hutoki kwenye hiyo ndoa". Kama unavyotujua walimwengu; sisi ndoa ikivunjika tutamchamba tu mwanamke bila kujua wala kujali nini haswa kilitokea. As a result mtu akija kuolewa tena anakuwa na mzigo wa kuhakikisha haachiki tena ili tusije msema tena "huyu ndiyo tatizo, ndiyo maana ndoa zote zinamshinda".
Ndoa inahitaji kujitoa na kuchukuliana na kubebana sana; lakini ikifika hatua ukaona kabisa maisha yako yapo rehani (physically or emotionally); please toka tu (God forbid). Tutasema mchana, usiku tutalala. Maisha yako yana thamani sana kwako, kwa watoto wako na kwa wazazi wako.

*Overcome your fear. Otherwise utaingia kwenye ndoa; afu ikitokea issue kidogo tu; unagive up maana ulishaiona divorce hata kabla hujaingia ndoani. "Aonavyo mtu nafsini mwake; ndiyo alivyo"

*Usione kama mtu amekuhurumia au amekufanyia favor kukuoa kwa sababu tu ni divorcee au single mom of 2. Kuna kitu huyo mwanaume amekiona ndani yako ndiyo maana akawaacha wanawake wote huko wabichi; akakufuata wewe. Mtu asikushushe thamani Wala usijishushe thamani.

*Angalia ni kwa kiasi gani mwanaume wako ana msimamo juu yako. Unatujua ndugu wa mume ma mawifi/wakwe. Tena awe alishaolewa na ana watoto wengine huko; maneno na visa haviishi. Na hakikisha emotionally upo vizuri sana; ili hata wakikutikisa wakute hutikisiki. Plus Mungu azidi kuyaimarisha malango yako ya kiuchumi; uwe tu na hela nkamu.

*Uwe na open communication na mzazi mwenzio. Ukivunja trust ya huyo mumeo, utakiona cha mtema kuni.

La muhimu zaidi; omba Toba na rehema na ujitenganishe kabisa na ndoa yako ya awali. Usije ukaingia kwenye ndoa mpya na garbages za ndoa yako ya awali. Divorce isiishie tu kwenye makaratasi; hadi spiritually m-divorce kwa sababu the two of you are/were "one in soul". Cut all the soul ties
Kila la kheri nkamu.
Mamaa magazeti. Unaandika gazeti refu halafu lote limejaa points za uhakika. Hiki ni kipaji,you should do something about it. Maybe an Instagram page of your own....called 'A PIECE OF ADVICE FROM HEAVEN SENT'
Think about it.
 
Mamaa magazeti. Unaandika gazeti refu halafu lote limejaa points za uhakika. Hiki ni kipaji,you should do something about it. Maybe an Instagram page of your own....called 'A PIECE OF ADVICE FROM HEAVEN SENT'
Think about it.
Boy dad; this means a lot. Hakika; nitalifanyia kazi. Thank you🙏🙏
 
Ndagha Fijo ghwangu...kyala andule Papo indumbula jikali jikahobhokela😪
Nkamu, angalia na usikilize moyo wako unasema nini juu ya hilo na mwisho wa siku wewe mwenyewe ndiye utakayekabiliana na matokeo yake kulingana na maamuzi yako na hakuna mwingine.

Lingine nkamu, watoto uwe pamoja nao, wasiwe mbali nawe.

Narudia tena kukushauri, usifanye haraka kuhusu maamuzi yako, Mungu amekupa watoto hao ndio zawadi yako na uwalee kwa karibu sana.
 
Nkamu, angalia na usikilize moyo wako unasema nini juu ya hilo na mwisho wa siku wewe mwenyewe ndiye utakayekabiliana na matokeo yake kulingana na maamuzi yako na hakuna mwingine.

Lingine nkamu, watoto uwe pamoja nao, wasiwe mbali nawe.

Narudia tena kukushauri, usifanye haraka kuhusu maamuzi yako, Mungu amekupa watoto hao ndio zawadi yako na uwalee kwa karibu sana.
Ubarikiwe sana nkamu...nimeshafanya maamuzi aisee 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
 
Back
Top Bottom