Nakusihi jumapili ya Leo kama Mwenyezi Mungu amekubariki basi, umguse mwenye uhitaji Alie karibu yako

clearmind

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
498
959
Habari za Leo Wana MMU?

Nakusihi jumapili ya Leo kama Mwenyezi Mungu amekubariki basi, umguse mwenye uhitaji Alie karibu yako. Wapo wengine tunao wafaham pia wanapitia changamoto za kimaisha. Tuwatie moyo na kuwasaidia pale tunapoweza.

Duniani tunasafiri. Hatuna budi kufarijiana, kusameheana, kutiana moyo na kupendana. Mungu wa mbinguni atujalie Neema na upeo wa kuona shida za wenzetu na kuwasaidia Kwa huruma.

Waombee wagonjwa pia na walio katika shida za vita na matetemeko.

Ubarikiwe pia na uendelee kuwa na afya njema, uchumi imara na amani katika familia yako.
Amina!.
 
Back
Top Bottom