NAKUPENDA, USINIEKE FRIENDZONE

NAKUPENDA, USINIEKE FRIENDZONE

Kugegedana ndiyo kitu kinachotambulisha kwamba hawa ni wapenzi. Hivyo vingine ni urafiki tuu na ni kawaida mtu kumfanyia rafiki yake.
Ni kweli lakini huyu kazidi bhn afu ukitegemea me ni chalii ya Moshi sijazoea mazoea yaliyipitiliza na mwanamke
 
Mbona mnapenda kutumia dini kuhalalisha ujinga? Kama unatembea kwenye dini si umwambie kwamba mimi nina girlfriend ila nakutaka na wewe wa pili, watatu au wa nne? Pumba.vu
Kiukweli mimi kama mwanaume mwenye mipango ya kuoa hapo baadae, siwezi kutulia na demu mmoja kwa sasa... Lazima niangalie yupi atanifaa, hivyo najaribu bahati yangu kila napoona huwenda patanifaa
 
Mwanaume mwenzetu unatuangusha,urafiki gani huo usio na faifa,akija geto charuka na makofi juu kula mambo kisha mpe shetani kesi kwa kuomba msamaha
 
Rafiki wa kike anahitajika.
Vigezo awe mrembo na mwenye mvuto. Mapenzi hayatoruhusiwa....karibuni.
 
Kuna demu ananishobokea sana, ila kila nikimgusia maswala ya mapenzi anabadilika kama chui..

Yani tukikaa week hatujaonana, basi siku akiniona anachangamka anani-hug na mabusu mengi mengi ... Yani hapa ndio nina data kabisa.. Tatizo ni moja tuu "hataki maswala ya mapenzi"

Kila siku kuniletea vizawadi na kunishukuru et hajawai kutana na rafiki wa kweli kama mimi.

Ni mwaka wa pili sasa naingiza gia lakini haingii kwenye line, mbaya zaidi kuna siku kanitongozeshea rafiki yake makusudi kabisa.. Anasema hapendi kuniona mpweke.... ila mimi simtaki rafiki yake namtaka yeye

Kiukweli naona ni bora kukatisha urafiki kabisa ili nisimuone ....
Weka na picha mkuu
 
Hawa viumbe ni wa ajabu.
Nina mtu alikuwa rafiki yangu tuu, ghafla akanitongoza nikakataa.
Basi kaninunia hamna hata salamu.
Sijui wana shida gani kazi kuwaza ngono tuu.
Binafsi ninaamini hakuna urafiki wa aina hiyo duniani.

Na kama upo basi lazima ukuletee matatizo kwenye ndoa yako.

If you violate the rules of the nature
The nature will convict you!
 
Back
Top Bottom