Kwa hiyo mnataka asifurahie ndoa yake, aishi kwa machale hadi ndoa ifikishe miaka 20 ndo aanze kuenjoy? What if wasipofikisha hiyo miaka 20? Kuna watu ndoa zao zilivunjika masaa machache after kufungwa, wao wanahesabu miaka, je sio baraka ya kumshukuru Mungu? Na usipoiona siku moja katika ndoa kuwa ni neema, unadhani ndo utafikisha miaka 20 kwa furaha? Kila siku moja ndo inakuja kutengeneza hiyo miaka 20+, yes labda ni miaka michache kwa kuhesabu ila hata maandiko yamesema tushukuru kwa kila jambo. Na usipojifunza kuthamini na kufurahia miaka 3, hata hiyo 20 utaona kama ni kitu cha kawaida tu, kumbe ni kwa neema tu. Muacheni tu amfurahie mke wa ujana wake, ndo inampa na motisha ya kufight zaidi kuijenga ndoa yake imara . Mbona biashara zenu zikisimama tu hata kama ni ka mwezi, mnazifurahiaaa na kuzitangaza, si mngesubiria zifikishe miaka mingi ndo mzifurahie?
Ambiele Kiviele, nimejisikia raha sana as if nimeandikiwa mimi jamani. Mungu azidi kuwatunza na kuwapigania. Endeleni kuinenea mema ndoa yenu, na ndivyo itakavyokuwa sawasawa na maneno yenu.